GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Katika maeneo ambayo Watanzania wameonesha ushirikiano wa hali ya juu mno, ni kwenye masuala ya sherehe. Wengi wanaoshirikishwa wamekuwa wakitoa ushirikiano murua kuanzia kwenye uuandaji kamati, kuchangisha michango na hata kula na kunywa.
Miongoni mwa shughuli za sherehe ambazo zimekuwa zikifanyika kwa mtindo huo ni pamoja na harusi na birthday.
Kwa baadhi ya mikoa, hasa yenye Wakristo wengi, kumekuwepo mpaka na sherehe za ubatizo na ubarikio, na mara zote ushirikiano wa wanajamii umekuwa ukihusika.
Kwa nini tusiurekebishe huo utaratibu, badala ya kuchangishana fedha za sherehe, tukafanya hivyo kwa ajili ya maendeleo?
Sidhani kama kuna ulazima wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kula na kunywa, ila kuna faida kubwa sana endapo hilo litafanyjka kwa jambo la kimaendeleo ama kwa ajili ya kutatua tatizo ambalo mhusika ameshindwa, kama matibabu n.k.
Naamini, ni jambo jema endapo tutajijengea utaratibu wa kuwa na harambee kwa ajili ya kuchangishana fedha za kimaendeleo kama vile:
1. Mtaji wa biashara
2. Kugharamia masomo
3. Kuukamilisha ujenzi wa nyumba
4. Kununua gari
5. Kununua shamba au kiwanja
6. Kuvuta umeme na maji, n.k.
Simaanishi sherehe zisiwe zinafanyika, badala yake, zikifanyika, zigharamiwe na wahusika pekee kulingana na uwezo wao. Kama mtu hana uwezo, aachane na masherehe. Hata kama ni anaoa si lazima afanye sherehe, na hata akihitaji sherehe, anaweza akaifanya ambayo ni very simple. Asipike mapilau na makuku, badala yake, aandae chai na karanga, kila mhudhuriaji apate kikombe cha chai na vijiko vitatu vya karanga zilizokaangwa.
Kuna maana gani mtu anayeishi kwenye chumba cha kupanga kutumia zaidi ya milioni moja kwa harusi?
Kwa mtazamo wangu, huoni ufujaji.
Tubadilikeni! Tufurahie kusaidiana katika mambo yatakayokuwa na matokeo ya kudumu kuliko sherehe.