Kama tunaaminishwa kuwa Mungu hakosei inakuwaje hakuna kiumbe mkamilifu chini ya jua?

Kwa ufahamu huu, tayari umekili ukamilifi ambao unatakiwa kuwepo. Yaani Mungu mwenyewe aliye mkamilifu. Basi Mungu ndiye.
 
Wanadamu hawajakamilika kutokana na choices..... Mungu amewapa uhuru wa kufanya mema au mabaya.... kwa upande mwingine sisi tunakuwa na weakness ambazo zinatufanya tusikamilike..
 
Kwa hiyo mkuu unataka tujadili mapungufu ya Mungu ama mapungufu ya binadamu ambao ndiyo wanasema sisi binadamu tuna mapungufu...
Kwanza kama kuna maandiko maandiko yoyote yale ambayo yanasema sisi binadamu tuna mapungufu ningependa kushirikishwa..
Pili kama una amini katika biblia na maandiko yake jibu ni rahisi tu. Binadamu wa kwanza aikuwa ni Adamu pekee ambaye Mungu alimuumba bila mapungufu yoyote.. Hawa aliyefuatia alitoka kwa huyu Adamu na wengine wote tukafuatia kutoka kwa binadamu wenzetu..
Kumbuka pia Hawa kwa sababu hakuwa na 100% kutoka kwa Muumba alidanganyika kwa yule nyoka pale Eden kuanzia hapo kila kitu kilibadilika na Muumba alituacha tuwe na uwezo wa kutambua mema na mabaya na ndipo dhana ya mapungufu yetu inakotoka.
 
Wewe na wale wliosema binadamu ametokana na nyani, hamna utofauti, kiukweli kiburi cha uzima ni mbaya sna.
 
Unawazungumziaje watu waliozaliwa na hormone imbalance , unazungumziaje mapacha walioungana ,unazungumziaje watu waliozaliwa na viungo nusu nusu ,unazungumziaje watu walio zaliwa na jinsia mbili kwa pamoja?
 
We ni me au ke?
 
Mkuu Gentamycin ngoja tu nikudaie , Yesu anasema haya," nakushukuru Mungu kwasababu mambo haya uliwaficha wenye akili na hekima ukawafunulia watoto wadogo " mstari utapewa ila maneno hayo yapo kabisa. Kwa maana hiyo Mungu hujifunua zaidi kwa wenye imani, kumbuka mtoto mdogo hana akili wala critical thinking and logical reasoning
 
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. mwanzo 1:26
Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.
Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.isaya 55:9-10
 
Unawazungumziaje watu waliozaliwa na hormone imbalance , unazungumziaje mapacha walioungana ,unazungumziaje watu waliozaliwa na viungo nusu nusu ,unazungumziaje watu walio zaliwa na jinsia mbili kwa pamoja?
Hapa ndipo wengi mnapochengana na Mungu maana mnataka maswali yenu ya physical yajibiwe spiritually wakati hivi vitu vya physically vinaanzia rohoni kwanza. Je mnafahamu chochote juu ya spiritual revelation? Maana kabla ya kuja mwilini mna lolote mnalolijua juu ya supernatural world? Au mmeng'ang'ania tu kwenye physical world kwenye malogic na facts ya akina Aristotle kusiko na ukweli wowote kuhusu maisha ya rohoni?

Ni sawa na yai la kuku linapovunjika na nguvu ya kulivunja ikatokea nje basi huo ndio utakuwa mwisho wa uhai wa hilo yai..lakini nguvu la kulivunja hilo yai ikitokea ndani basi ndio mwanzo wa uhai na kifaranga utotolewa na maisha huanzia hapo. Je unaelewa kwanza nguvu ya ndani ya binadamu? Spiritual awakening? Huwezi kuelewa ndio maana unatumia logic and facts za physical world zisizo Na ukweli wala uhalisia.

Kwa vile huko mwilini zaidi... Nakushauri ujifunze spiritual arguments ili tutembee barabara moja.

Kiranga kawaharibu sana! Mnafuata tu mkumbo....mnakuwa wabishi na wajuaji msiojielewa.
 
unasema mwenye critical thinking ndo achangie, heading umeitumia kama defence mechanism kwa atakaye kupng bas hana critical thinking, inferiority complexity ndo inakuendesha, nilhc umebadilika wewe jamaa kumbe bado bichwa lako limejaa mabunda na pepeta. Mada yako ingekua nzur sana kama usingetia ujuaji wako wewe mkimbizi
 
Wewe jamaa haujui unasimamia upande upi.

Huko juu umeanza kusema Mungu anaumba binadamu na hakosei kila kitu kinakaa mahala pake na ukatolea mfano makalio ,

Sasa hapo nimekutolea cases tofauti tofauti ambazo watu wanazaliwa wamekosewa.
 
Msemo wa hakuna aliyekamilika ni msemo wa kipagani. Kila binadamu ni mkamilifu mbele ya muumba ispokuwa kila mtu ni wa kipekee "unique". Hakuna anayeweza kufanana na mwingine kimaumbile, kitabia , hulka nk. Tunaposhindwa kuheshimu mpango wa Mungu wa kuumba watu tunaotofautiana nao ndipo tunatunga misemo kama hiyo
 
Reactions: Cyb
Wewe jamaa haujui unasimamia upande upi.

Huko juu umeanza kusema Mungu anaumba binadamu na hakosei kila kitu kinakaa mahala pake na ukatolea mfano makalio ,

Sasa hapo nimekutolea cases tofauti tofauti ambazo watu wanazaliwa wamekosewa.
Sibishanagi kuhusiana na Dini.

Baki na msimamo wako..niache na msimamo wangu. Nasikitika kwa vile sina muda wa kuchezea.

Namuamini Mungu sana, na wewe endelea kutomuamini Mungu Sana. simple as that!
 
Sibishanagi kuhusiana na Dini.

Baki na msimamo wako..niache na msimamo wangu. Nasikitika kwa vile sina muda wa kuchezea.

Namuamini Mungu sana, na wewe endelea kutomuamini Mungu Sana. simple as that!
Wapi nimesema simuamini Mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…