wilbald
JF-Expert Member
- Dec 17, 2007
- 1,810
- 1,377
Hebu angalia tu..ndugu mliozaliwa na wazazi wamoja lakini mmoja no professor mwingine ni mwl wa shule ya msingi..je hapo kuna mlinganyo?Kiimani na hata mahala pengi tu utawasikia Watu wakisema kwamba Mwenyezi Mungu hakosei, hajakosea na kwamba huwa hakosei na wengi wetu ama Kiuwoga au ' Kimbumbumbu ' tu au kwa kuwa wa ' hovyo hovyo ' katika Kufikiri tayari tumeshaaminishwa hivyo.
Sawa kama kweli Mungu hakosei sasa inakuwaje kila mara huwa tunaisikia hii Kauli ambayo nainukuu hapa " Hakuna Binadamu aliyekamilika chini ya Jua, Mwezi au Dunia hii ". Je hapa tushike lipi au tuelewe lipi?
Na kama Wote tunakiri kwamba Mwenyezi Mungu hakosei katika ' Uumbaji ' wake na Sisi Wanadamu ni mfano wake tosha iweje tena leo tunasema hadi kwa msisitizo kabisa kwamba Binadamu wote hatujakamilika?
Tujadili na Karibuni katika huu ' mjadala ' ambao nawahitaji tu wale ambao wamebarikiwa Critical Thinkig na Logical Reasing ya kutosha wachangie na nimetahadharisha mapema tu katika ' Headline ' kama unajijua au kujihisi huna huo uwezo tafadhali tusichoshane na pita zako tu mia.
Nawasilisha.
Hivyo hapa mungu amempa kila mja watu baraka zake kulingana na uwezo wa malaika mlinzi wake aliyepewa jukumu la kuwa naye hadi amalize safari yake hapa duniani..
Tungekuwa tumekamilika ama wote tungekuwa kama bill gates au Ronald au trump au matonya au mrema au G jelly..madhara yake sasa kusingekuwa na wakumsaidia mwenzake yaani bwana na mtumwa wasingekuwepo.
Na siyo wanadamu tu hata wanyama na mimea ya jamii moja siyo saw a..hebu angalia kule Serengeti dume moja la simba linavyojimilisha mademu kibao na ikiwezekana kuyapiga madume mengine..cc.chibu D.