Mungu ametuumba kwa ukamilifu mkuu wa kimaumbile mapungufu ya mwanadamu yanatokana na ubinadamu wake.
Mungu ametupa hekima kuu kupita viumbe vyote, mwanadamu ajua jema na baya pasipo kufunzwa, ila yeye hutenda maovu kwa kiburi na jeuri ilhali akijua matokeo yake yalivyo.
Mkamilifu ni Mungu pekee kwa maana yeye hutenda kwa haki na kwa upendo mkuu jambo ambalo mwanadamu haliwezi, nalo ndilo lampunguzia ukamilifu mwanadamu aliye kiumbe cha Mungu.
Kutokukamilika kwa mwanadamu kunadhihirika kupitia maovu anayotenda na si kwa maumbile. Tunaposema binadamu hajakamilika tunazungumzia mapungufu kupitia matendo yake na si vinginevyo.