Kuna fukuto kati ya makonda na Gambo kugombea Ubunge jimbo la Arusha mjini, maneno na maoni ya wananchi na wanachama muhimu wa CCM yamekuwa mshale mkali dhidi ya makonda.
Nimezunguka kutaka kufahamu maoni ya wanachama waandamizi wa CCM mkoa wa Arusha kuhusu mkuu wao wa Mkoa na hamu yake ya kutaka kugombea Ubunge jimboni; Watu wengi hawafurahishwi kabisa na kijana huyu wa kisukuma ambae hata miaka mitano hajafikisha mkoani hapo.
Watu wa Arusha wamenyooka saana, hawapendi siasa za kinafiki na za Kukandamizana.
Kiasili Gambo anakubalika ndani ya CCM kwakuwa ni kijana walomlea Arusha, lakini mstaarabu na sio mropokaji.
Hata hivyo akiwa mkuu wa mkoa amefanya mambo yanayoonekana mkoa wa Arusha hasahasa sehemu zilizoko watu wasikini kama Murieti, Dampo, Usw ahilini, Unga ltd, Ngarenaro, Sombetini, Morombo, Intel nk.
Kiufupi Makonda hapendwi kabisa hata na wafanyabiashara, kwasababu shughuli zake nyingi za kisiasa zimekuwa mwiba kwa wafanyabiashara wa maeneo ya mijini.
Kufunga barabara, kuongeza foleni za magari kusiko sababu, kuzuia baadhi ya vituo vya mafuta kufanya kazi, maduka kufungwa nk. Hivi vimekuwa vikimpunguzia uhalali wa kuwa muwakilishi wa kero za wananchi bungeni kwani yeye mwenyewe MAKONDA ni kero
Makonda afikirie kugombea jimbo la usukumani na sio Arusha. Kwasababu kama MAKONDA ATARUSHA KETE YA KUGOMBEA UBUNGE NA KUOMBA RIDHAA JIMBONI NA UCHAGUZI NDANI YA JIMBO UTAKUWA HURU NA HAKI, MAKONDA HATOBOI