Leo mbunge Musukuma akichangia Bungeni, amesema moja kati ya sababu za mradi wa bwawa Hilo kukwama, ni kwamba ujenzi wake ni substandard (chini ya viwango).
Ningekuwa na enough time, ningeweka Ripoti ya CAG (for Development Projects) ya 2019/2020. Katika ripoti ile, kwa kuangalia muktadha huu, CAG ali-highlight mambo yafuatayo:-
1. Wakati tenda inatolewa, moja ya sharti lilikuwa ni kwa Contractor kuto-subcontract kazi yote, na kazi atakazo-subcontract zisizidi 50% of Contract Price!
Kwenye uchunguzi wake ule CAG akagundua, by the time kulikuwa na 21 Subcontractors na 9 Subconsultants. Kilichomtia hofu CAG ni kwa hao Subcontractors kupewa kile alichoita ALL MAJOR PROJECT COMPONENTS.
Kutokana na hilo, CAG akaeleza wazi kwamba HII INAWEZA KU-IMPAIR THE QUALITY OF WORK hata kama the quality risks inaangukia kwa Contractor.
2. Wakati sharti la mkataba lilikuwa linamtaka Contractor kuto-subcontract more 50% of the Contract Price, kwa bahati sharti hilo lilizingatiwa na kuona ni around 37% of the Contract Price ndiyo ilikuwa subcontracted!
Hata hivyo, disclosure ya hyo subcontracted price haikuwa kazi ndogo kwa sababu Contractor aligoma kutoa na ikabidi ifanyike jitihada ya ziada kuhakikisha anatoa!!
Sasa ndipo unajiuliza kama Subcontracting yake imefuata masharti ya mkataba, ni kwanini basi alikuwa hataki kutoa!
3. Contract and Project Design Requirements ilikuwa inataka Contractor ajenge 2 Diversion Tunnels. Kwa mshangao wa CAG, Contractor akajenga ONLY ONE Diversion Tunnel!
Matokeo yake, iliponyesha mvua na mto kujaa, maji yakafanya mambo yake!!
What happened next day? Wakati mnaambiwa mambo ni FIRE kumbe uhalisia project ilikuwa DELAYED FOR 5 MONTHS!!
Na wakati akina Msukuma wanashangaa kuona Mradi hutaki kwisha na hivyo kuona ni ubabaishaji wa Makamba, Ripoti ya CAG ya Masharika ya Umma ambayo ilitolewa March 2021
Ndugu yangu
residentura...
Nimeona post yako lakini amini usiamini, tatizo kuu la nchi hii sio CCM wala mawaziri wao bali ni WANANCHI...
Be the worst leader EVER... bado itatokea millions of MISUKULE hai itakayokuwa inakushangilia na kukutea na uovu wako!
Na tatizo letu kubwa ni kwamba, HUWA HATUFUATILII mambo kwa undani na matokeo yake tunakuwa Victim wa Uongo wa Viongozi wa CCM!!
Amini usiamini, anayosema Makamba mengi kama sio yote aliyokuta pale TANESCO ni ukweli mtupu!!
Sio kwamba Makamba ana tofauti na viongozi wenzake wa CCM, la hasha! Kwa sababu zilizo wazi kabisa inaonesha bado ana kinyongo na JPM Administration.
Kwahiyo kwa kutumia kinyongo hicho alichonacho, ndipo nae anaamua kutumia nafasi yake kuonesha ni namna gani JPM Administration ili-handle power sector kwa uovyo kabisa!!
Yaani ni kama anamwaga mboga vile! I doubt kama angekuwa anayasema haya kwa uwazi endapo angeendelea kuwa kwenye JPM's Circle.
But trust me, mengi anayosema ni ya ukweli na yapo kwenye Ripoti za CAG za tangu wakati JPM yupo madarakani! Sema kwavile huwa hatufuatilii, ndo maana leo yakisemwa tunaona uongo tu!!
Kwa mfano, suala la watu kutoruhusiwa kufanya maintenance, LIPO KWENYE RIPOTI YA CAG. Ipo baadhi ya mitambo pale Ubungo tu ambayo ilifanya kazi kwa zaidi ya saa 10K nje ya muda ambao ilitakiwa ziwe zimefanyiwa maintanence.
Yaani, kama mtambo ulitakiwa kufanyiwa maintanence baada ya kuwa umepiga mzigo kwa saa 15K, basi CAG aliukuta ukiwa umepiga mzigo kwa saa 25K bila maintanence!!
Wakati huku mtaani tunaambiwa MAMBO NI FIRE kiasi kwamba hata ndugu yangu
MALCOM LUMUMBA akashawishika kwamba inawezekana kuna hujuma kweli pale JNHP, lakini Ripoti ya CAG inasema, as at December 31, 2020 Mradi ulikuwa umeendelea kwa ONLY 28.61% wakati kwa tarehe hiyo walitakiwa wawe wamekamilisha 47%!
Yote hayo wananchi hatukujua, na wengine tulipojaribu kuweka uhalisia, tena with facts from Govt Sources, tukaambiwa tuna chuki na JPM!!
Leo hii wanaona mradi upo bado, wanalia hujuma dhidi ya JPM bila kufahamu kwamba, ingawaje tulikuwa tunaimbiwa nyimbo tamu za maendeleo ya mradi lakini hadi JPM anatangulia mbele za haki, sehemu kubwa ya mradi ilikuwa haijafanyika!
And guess what... moja ya sehemu ya ripoti inasema, 2 years baada ya kutangazwa kuanza kwa mradi, TANESCO walishindwa kutoa PROOF ya kuwepo kwa pesa za kuendeshea mradi kwa sababu walishindwa kuonesha bajeti ya mradi!
Lakini pamoja na yote hayo, huku mtaani tulikuwa tunashangilia uongo tunaoambiwa ambao unaweza kuifanya CCM iendelee kubaki madarakani kwa miaka kadhaa kwa sababu they're good in telling lies, na wananchi wanafurahia kudanganywa kwa sababu hatufuatilii na matokeo yake tumekuwa ndo agents of Lies Protections!!
Leo hii Makamba anatembelea madhaifu ya past administration as defensive mechanism but nobody believe him coz' we already believed in lies.
Makamba nae itafika wakati ambapo hatimae defensive mechanism ya kutumia JPM Administartion itakuwa No More Applicable kwa sababu atalazimika kuonesha Results and no more Updates!
Na kwavile possibly nae HATAWEZA kuonesha results, nae ataanza kutoa NEW LIES, and we'll believe him from his new lies, na atapata New Lies Defenders... it's vicious circle!!