Kama ulikua hujui kuwa DAR ES SALAAM kuna TAPELI WA JUICE wacha nikufahamishe;-

Bro labda hujaishi mikoa ya Dar na Pwani.
Nilipita hapo akanipigisha story na juice nilikataa. Kinachoniokoaga mara nyingi na utapeli ni kauli mbiu yangu.

"NEVER GET DISTRACTED."

Yani nikiwa na safari mtaa wa Congo sipotezi zaidi ya dakika moja hapa katikati hata ulete kujuana mimi huwa nafocus na destination yangu.

Huyo bwana ananiongelesha huku anaandaa juisi nkajua tu walewale!
 
Ila mambo ya Dar bwana yanachekesha, huyo mtu nimeanza kumsikia miaka na miaka, lakini hakuna hatua zozote mnazomchukulia. Mtu yupo, mnamjua, mna ushahidi wa uhalifu, alafu kikubwa mnaweza kufanya ni kulalamika mitandaoni, serious?
Haha inachekesha sana, kuna vitu ukifikiria inabidi ucheke tu, ila wakiita mwizi kwa mpita njia tu haraka haraka bila kuuliza wanajichukulia sheria mkononi.
 
Unaanzaje kusimama au kupokea kitu hovyohovyo kutoka kwa mtu msiyefahamiana?Acheni uroho na kupenda dezodezo.
 
Unaanzaje kusimama au kupokea kitu hovyohovyo kutoka kwa mtu msiyefahamiana?Acheni uroho na kupenda dezodezo.
 
Inashangaza sana. Yaani unapita tu barabarani unapewa juice na wewe unakunywa tu bure bure!
 
Mimi kama sijahitaji huduma hata ukinipa bure sipokei nitajuaje usalama wake, lengo lake
 
Aisee.

Sijui kwa nini mpaka leo hachukuliwi hatua.
 
Uwezi amini nishawahi kukutanaye mmoja , anajifanya kama anakujua hivi

Sasa Mimi nikahisi kama amenifananisha

Sema pesa nilikua nayo, baada ya kunywa juice nilimlipa
Hata mimi na mshikaji wangu ilinitokea hivyo, alianza kama anamjua yule mshikaji wangu, eti ahaa nimeachana na bodaboda bhna nipo huku sasa hivi.

Bahati nzuri hela nilikuwa nayo nikamlipia na yule mshikaji ndio tulipotoka pale tukaanza kujicheka tulivyotapeliwa kipumbavu namna ile.

Mimi si mtu wa kutumia juice za matunda za njiani au za kutemebeza ila siku hiyo ni kama nilirogwa alafu juice yake ina rangi nzuri ila ukiiweka mdomoni ndio akili inakurudi kwamba mbona kama unabeba kipindupindu kwa kujitakia
 
Jamaa ni mbunifu....
 
Yaani mpaka mtu nisiyemjua anisimamishe aanze kuniuliza huo muda sijui nitaupata wapi, halafu sina utaratibu wa kula kula njiani ni either niingie restaurant nikishiba nitoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…