Kama ulikuwa hujui, Waisraeli wana haki ya kuichukua Gaza! Ushahidi huu hapa

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, amedhamiria kuitwaa Gaza yote bila kujali kelele za mataifa yanayompinga. Ujasiri huo anaupata wapi? Katika kupitia pitia Maandiko nimegundua kumbe ni halali yake kibiblia. Waisraeli wana haki kabisa ya kuimiliki Gaza, kwa sababu ni sehemu ya eneo ambalo Mungu aliwapa kuwa urithi wao tangu enzi za Ibrahimu!

Mungu aliwaahidi wazao wa Ibrahimu kuwa atawapa eneo linaloanzia Mto wa Misri hadi Mto Frati (Mwanzo 15:18). Eneo hilo linajumuisha Gaza!

Ukisoma Maandiko kwa makini utaona kuwa Gaza iko ndani ya nchi ya Kanaani. Yoshua alipowaongoza Waisraeli kuingia Kanaani, Gaza ilitajwa kama moja ya miji waliyopewa kuimiliki (Yoshua 13:2-3). Hata hivyo hawakuweza kuimiliki kikamilifu wakati huo, lakini bado ilikuwa sehemu ya urithi wao.

Kama umesoma habari za Wafilisti, basi Gaza ilikuwa ndiyo ngome ya Wafilisti, maadui wakuu wa Israeli. Biblia inasema Wafilisti waliipinga Israeli mara kwa mara (Waamuzi 16, 1 Samweli 6). Kwahiyo Netanyahu ameamua kuitwaa Gaza kutoka katika mikono ya maadui zake wa zamani kwa kuzingatia ramani/mipaka ya eneo ambalo Mungu aliwapa kuwa urithi wao.

Nabii Amosi na Zekaria ni manabii walioitabiria Gaza hukumu kwa sababu ya uovu wake, lakini pia walionyesha kuwa siku moja itakuwa chini ya utawala wa Bwana (Amosi 1:6-7, Zekaria 9:5-7). Kinachoendelea sasa huko Gaza ni dalili ya kutimia kwa unabii huo.

Wasiosoma Biblia hawawezi kuelewa sana jambo hilo. Kwa nje linaonekana la kisiasa zaidi, lakini kwa ndani ni jambo linalotimiza mpango kamili wa Mungu wa kuwapa Israeli ardhi yote aliyowaahidi.

Inasikitisha kuona jinsi majengo ya Gaza yalivyogeuka vifusi, watu wanavyouawa Gaza kwa mabomu, na utapiamlo unavyokuwa tishio kwa watoto wa Gaza. No way out, Waisraeli wanachukua kilicho chao. Laiti Wapalestina wangeujua ukweli huo wakakubali kuhamia katika nchi zilizokubali kuwafadhili.
 
Do you mean Hamas ndio Wafilisti wanaotajwa kwenye Biblia?
 
Wale wapalestina walioko Gaza waende wapi?
Israel wametumwa na nani kuwaua wale na njaa?

Is the policy sustainable for the future of Israel and the mankind?
Ukiambiwa hapo unapoishi ni kiwanja cha mtu, hama, utajibu " niende wapi?"

Netanyahu na IDF sio Wakristo. Sisi Wakristo tukipigwa shavu la kushoto, tunageuza la kulia. Wao bado wanaongozwa na sheria ya Agano la Kale ya jino kwa jino. Kwahiyo hawaoni vibaya kulipa kisasi. Si unakumbuka Hamas iliwaua Waisraeli 1200 na kuteka wengi? Ndio sababu wanapiga majumba na wala hawajali wanaokufa kwa njaa!!
 
It sums up everything....little knowledge about how things are made in the universe.

Mpaka leo mnaleta hadithi za kufikirika. Kwanini wasiishi pamoja kama ndugu na kila mtu akaendelea na 50 zake?
 
Mpango Wa Israel na Ulichokiandika ni Vitu viwili tofauti Israel Mwisho wake upo karibu sana Pale gaza Wanataka Kuchimba Ben Gulion Canal pale siasa ya uchumi inataka Ku take place Yani kiufupi huyo Israel has nothing to do na hiyo mistari yako ya kibiblia halafu hata wayahudi wanakushangaeni ninyi Wakristo wao Mambo Yao ni Mbali sana na tamaduni za kikristo
 
Uyahudi na uzayuni ni mambo mawili tofauti.

Hawa wakristu wa mwendo kasi, ambao wanajaza gasi kwa kupuliza mitungi kwa mdomo, hawajitambui

Mazayuni hawana lolote na wakristu. Wana agenda zao wanazijua wenyewe
 
Waafrika tunapenda sana mambo ya kukariri na tukishamaliza kukariri, tunajiita wasomi. Na kuleta ujuaji mwingi.

Theodore Herzl, ambaye ndio muasisi wa uzayuni, hakuleta mambo sababu ya dini...alileta sababu ya kupinga udhulumati dhidi ya wayahudi

Kinachoendelea sasa ni tofauti na malengo ya kuanzisha Israel
 
It sums up everything....little knowledge about how things are made in the universe.

Mpaka leo mnaleta hadithi za kufikirika. Kwanini wasiishi pamoja kama ndugu na kila mtu akaendelea na 50 zake?
Hahaa. Umekaa kwenye kiwanja cha mtu, mwenyewe anakuja, anakuambia umpishe unamjibu kwanini msikae pamoja?

Bado unadanganyika kwamba Biblia ni hadithi za kufikirika?! Kama huiamini Biblia, waamini Archaeologists na historians waliotoa vielelezo vinavyothibitisha kuwa Biblia sio hadithi za kutungwa.

Israeli ni taifa special sana mbele za Mungu ndio sababu linafanikiwa katika mipango yake. Hujiulizi kwanini mataifa yote makubwa na UN wanaona kinachoendelea Gaza lakini wameshikwa na ganzi. Mungu yuko upande wa Israeli. Anawapigania.
 
Mpango Wa Israel na Ulichokiandika ni Vitu viwili tofauti Israel Mwisho wake upo karibu sana Pale gaza Wanataka Kuchimba Ben Gulion Canal pale siasa ya uchumi inataka Ku take place Yani kiufupi huyo Israel has nothing to do na hiyo mistari yako ya kibiblia halafu hata wayahudi wanakushangaeni ninyi Wakristo wao Mambo Yao ni Mbali sana na tamaduni za kikristo
Unaota ndoto mkuu. Israeli wanajiandaa kumpokea Masihi wewe unasema mwisho wao uko karibu?!
 
Kabla ya Kupewa Kanaan Nchi ya Ahadi. Waisrael walikuwa Wanaishi wapi??

Na kabla ya wao kufika Kwenye hiyo nchi yao waliyoahidiwa kama unavyodai Hiyo nchi ilikuwa Tupu au ilikuwa na Watu wanaishi?? Kama walikuwepo Ni kina Nani.
 
Ume-comment bila kusoma mada? Kwani Trump anavyowafukuza wahamiaji, anafukuza kitimoto?
Ushasema Wahamiaji. Means kwamba Wanatambulika kuwa hawana asili ya Marekani na Waliingia Marekani wakitokea mataifa mengine. Even though sihalalishi anachokifanya Trump.

Lakini mfano wako hauendani na Uzi wako. Waisrael pale Palestine wao ndio wakimbizi kwa sababu wametoka huko walipotoka Wamevamia Ardhi ya Watu Huku wakidai kuwa wameahidiwa.

Mfano Tanzania waje Watu katika Majirani zetu waseme hii Tanzania tumepekuwa Vitabu vyetu vya kale tumekuta ni nchi yetu tumeahidiwa kwaiyo mtupishe. Jee hilo litatuingia akilini??
 
Ume-comment bila kusoma mada? Kwani Trump anavyowafukuza wahamiaji, anafukuza kitimoto?
TPRFr78ZU3v7iDFs7a_rlD5aKz164AMlEpcfTa0sR4c.jpg

Kwa hapo nani mhamiaji?
 
Kabla ya Kupewa Kanaan Nchi ya Ahadi. Waisrael walikuwa Wanaishi wapi??

Na kabla ya wao kufika Kwenye hiyo nchi yao waliyoahidiwa kama unavyodai Hiyo nchi ilikuwa Tupu au ilikuwa na Watu wanaishi?? Kama walikuwepo Ni kina Nani.
Shida mnaipuuza Biblia. Hayo maswali mbona majibu yote yako wazi kwenye Biblia?
 
Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, amedhamiria kuitwaa Gaza yote bila kujali kelele za mataifa yanayompinga. Ujasiri huo anaupata wapi? Katika kupitia pitia Maandiko nimegundua kumbe ni halali yake kibiblia. Waisraeli wana haki kabisa ya kuimiliki Gaza, kwa sababu ni sehemu ya eneo ambalo Mungu aliwapa kuwa urithi wao tangu enzi za Ibrahimu!

Mungu aliwaahidi wazao wa Ibrahimu kuwa atawapa eneo linaloanzia Mto wa Misri hadi Mto Frati (Mwanzo 15:18). Eneo hilo linajumuisha Gaza!

Ukisoma Maandiko kwa makini utaona kuwa Gaza iko ndani ya nchi ya Kanaani. Yoshua alipowaongoza Waisraeli kuingia Kanaani, Gaza ilitajwa kama moja ya miji waliyopewa kuimiliki (Yoshua 13:2-3). Hata hivyo hawakuweza kuimiliki kikamilifu wakati huo, lakini bado ilikuwa sehemu ya urithi wao.

Kama umesoma habari za Wafilisti, basi Gaza ilikuwa ndiyo ngome ya Wafilisti, maadui wakuu wa Israeli. Biblia inasema Wafilisti waliipinga Israeli mara kwa mara (Waamuzi 16, 1 Samweli 6). Kwahiyo Netanyahu ameamua kuitwaa Gaza kutoka katika mikono ya maadui zake wa zamani kwa kuzingatia ramani/mipaka ya eneo ambalo Mungu aliwapa kuwa urithi wao.

Nabii Amosi na Zekaria ni manabii walioitabiria Gaza hukumu kwa sababu ya uovu wake, lakini pia walionyesha kuwa siku moja itakuwa chini ya utawala wa Bwana (Amosi 1:6-7, Zekaria 9:5-7). Kinachoendelea sasa huko Gaza ni dalili ya kutimia kwa unabii huo.

Wasiosoma Biblia hawawezi kuelewa sana jambo hilo. Kwa nje linaonekana la kisiasa zaidi, lakini kwa ndani ni jambo linalotimiza mpango kamili wa Mungu wa kuwapa Israeli ardhi yote aliyowaahidi.

Inasikitisha kuona jinsi majengo ya Gaza yalivyogeuka vifusi, watu wanavyouawa Gaza kwa mabomu, na utapiamlo unavyokuwa tishio kwa watoto wa Gaza. No way out, Waisraeli wanachukua kilicho chao. Laiti Wapalestina wangeujua ukweli huo wakakubali kuhamia katika nchi zilizokubali kuwafadhili.
Siko hapa kuhalalisha mauaji ya watu hasa watoto aisee. Nina watoto na kinachoendelea hapo Gaza naomba Mungu awape amani.
 
Usichoelewa ni nini, mkuu. Mungu ndiye aliyewaambia Waisraeli wakaishi Kanaani(including Gaza). Ramani na mipaka ya eneo lao nimekwambia imewekwa na Mungu mwenyewe kama ilivyoelezwa kwenye Biblia. Ndio sababu wana ujasiri wa kuwatimua hao Wapalestina. Wewe unaonesha ramani ya 1947BK wakati mipaka ya eneo walilopewa Israeli iliwekwa wakati wa Ibrahimu(2000KK). Wapalestina wanatakiwa wakubali tu ukweli mchungu kwamba eneo wanalokalia ni urithi wa wana wa Israeli. Kushindana na Israeli ni kushindana na Mungu. Ndio maana wanafeli maana hakuna anayeweza kuzuia makusudi ya Mungu.
 
Siko hapa kuhalalisha mauaji ya watu hasa watoto aisee. Nina watoto na kinachoendelea hapo Gaza naomba Mungu awape amani.
Israeli bado inafuata sheria ya Musa ya jino kwa jino, walichokozwa na Hamas, watu wao wakauliwa. Sasa wanajibu mapigo. Wataendelea hivyo mpaka Yesu atakapokuja kuwaokoa kutoka katika giza hilo la kutoamini kwamba Yesu ni Mwokozi. Watakuja kutubu
 
Back
Top Bottom