Kama ulishawahi kunywa chai ya kuunguza Sukari tukutane hapa

Acha tu haya Maisha tulipo toka Mungu anajua, unasubir sukar iungue ndio unaweka maji yachemke
 
Noma sana enzi hizo za unga wa Yanga kitu cha njanooo lakini maisha yalikuwa matamu sana jioni bibi anawapoza kwa Hadithi tamu tamu mnasahau yote.
 
Mambo ya pizA ,bagger wenyewe watoto wa kidigital wanaona wameyapatia kumbeee.
 
Touching story aisee nimeyafanya haya hapo kale, kuchoma sukari kama mbadala wa majani, kupaka sabuni daaa haya maisha haya
 
Mkuu we Acha tu wanaosema dunia inatembea siyo kama gari bali vitendo vinavyofanyika ndani yake
Kuna watu huwa nawaangalia siku hizi za usoni nasikitika tu, nimekua ugali na maji ya sukari aisee ndo maana nikijiangalia hapa nilipo sasa naamua kula maisha maana huko nyuma wazee ndo wanajua
 
Ha ha ha![emoji16] Foleni za RTC! Huko ndio kwa mara ya kwanza kuona mtu anaweka jiwe kisha kuna my yuko kwenye mstari anamsogezea, ole wako uruke jiwe la mtu![emoji3] Tatitzo ni pale jamaa anapokuwa na mawe matatu hivi anayasogeza....mjini bwana. Ndio tulivyoishi miaka hiyo. Viatu mzee alikuwa ananipeleka jamaa fulani hivi Wapare pale soko kuu Arusha, unapimwa mguu kwa kuweka mguu chini juu ya karatasi halafu jamaa anazungusha kalamu kufuatiza mguu-hapo inachongwa Safari Boot(Buti)[emoji3] Hiyo unavaa mpaka inakauka na kupinda katikati hapo inaitwa "Mbwa", ile ngozi inababuka na kuisha nywele, ukisikia mbwa wanacheka manake zimefumuka mbele vidole vinachungulia[emoji38][emoji38]
 
Enzi hizo primary ilikuwa kawaida sana
 
Nimeinywa sana na kuipika saba R.I.P babu Yangu akikosa majani faster kaunguza sukari.
 
Ile chai mbona ilikua tamu sana, Mimi nimeinywa sana toka miaka ya 1984 kwani ndio kipindi ambacho nilikua nawai shule kama hakuna majani, mother anakaanga sukari faster kitu na box, umesahau pia ugali wa mboga ya kitunguu kitupu kinakaangwa, duh maisha haya yametoka mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…