Daaah! nakumbuka miaka ya 2000 tulikuwa tunaishi mtaa mmoja na msaani mmoja anaitwa VOICE WONDER huyu jamaa alikuwa peace na kipindi hicho nipo shule ya msingi Tabata nilikuwa nawatambia sana mademu kuwa voice wonder ni broh angu, niliopoa sana mademu sababu ya huyu jamaa.
Baadae nikahamishwa shule na kuhamia shule ya msingi MABIBO ile mabibo ya MAKUBURI, daah huku pia nikapata rafiki mmoja darasani anaitwa ISSA ABDALLAH sasa hivi huyu jamaa anacheza mpira IHEFU anatumia jina la ISSAH NGOAH basi bwana kumbe huyu mshikaji kaka ake alikuwa ni MB DOG aisee nikatamba tena mtaani kwangu kuwa MB DOG ni broh angu maana mdogo ake nipo nae darasa moja , alafu kipindi hicho MB DOG walikuwa wanakaa mtaa mmoja na ZOLA D na msaani mwingine alikuwa anaitwa SHELEA MAN, Nakumbuka siku moja ISSA alikuja nyumbani kufata samaki wa kufuga wale way back sana alikuja na kaka ake MB GOD aisee mtaa mzima ulihamia nyumbani, nikaopoa sana mademu [emoji14]
Baada Issa kumleta kaka ake nyumbani baadae jamaa (Mb dog) alikuwa anakuja mwenyewe tu kuchukua samaki, nilipata sana fame mtaani siku nyingine alikuwa anakuja na ZOLA D jamaa alikuwa mbavu kinoma basi mtaani na mimi nikawa super star, nikawa nagonga pisi kali tu kipindi hicho, wakawa wanakuja hadi kina SQUEZAR, DATAZ, MADEE, JAFARAY
Baadae kabisa nikawa najulikana na wasanii wengi tu sababu ya kuuza samaki wa mapambo hawa na hadi leo hii nina connetion na wasanii kama wote kina mr blue, songa, grace matata, damian soul, G nako, babu wa kitaa na mdogo ake country boy, dogo janja, madee, jay moe na wengine sababu ya samaki wa mapambo na ndio biashara yangu kubwa inayonikutanisha na watu maarufu hadi leo [emoji1431]