ilikuwaje tupeane uzoefu mkuu
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ni story ndefu saana but ngoja nikupe kwa ufupi
Kuna binti niliingia nae kwenye mahusiano tukiwa primary darasa la 5 secondary yeye alifaulia shule ya taarafa (alikuwa na akili saana)
Mm nikaenda shule ya kataa then kuna shemeji yangu akaona kabisa hiyo shule siwezi kufaulu ikabidi anipeleke shule ya kulipia mkoa mwingine
Tukaendelea mahusiano hasa nikiwa narudi home likizo (huyu binti alikuwa ananipenda saana)
Then advance mm nikapangiwa bwiru boys baada ya kumaliza form six nikarudi mkoani kwetu na tukaendelea mapenzi
Muda wa kwenda chuo ulipofika huyu binti alikuwa anataka MD na kwao hakuna hela ikabidi aende education (alipata mkopo 100%)
Mm sikupata mkopo na shemeji yangu akanishauri niende nikasome diploma ya mechanical engineering
So one day before binti hajaenda chuo nikamuomba kibumbu (alikuwa bado ni bikra) baada ya wiki mbili toka tusex na kumtoa bikra akajigundua ni mjamzito
Nikahudumia mimba mpaka mtoto alivyozaliwa (kipindi chote hichi cha mimba hakurudi kwao na hakuwaambia kuwa ana mimba ila aliendelea na chuo)
Mm nilivyomaliza tu chuo shemeji yangu aliupiga mwingi saana nikapata kazi kwenye mamlaka moja chap chap na mzazi mwenzangu yeye baada ya kumaliza hakupata kazi hivyo basi nikawa namuhudumia yeye na kwao kiujumla (so hapa alizidisha unyenyekevu saana)
Kulingana na mamlaka nayofanyia kazi nikajuana na watu mbali mbali kama wafanyabiashara,tiss,walimu,wajeda,polisi,wavuvi N.K
Katika kujuana na watu huko nikawa nimempatia connection ya kazi shule moja ilikuwa wilaya tofauti na kwao na ilikuwa rahisi kumpatia nafasi sababu ya masomo yake (chemistry and physics) hii shule alikuwa analipwa laki nne na bado akawa mnyenyekevu saana kwangu
Baada ya muda wa miezi 9 toka apate kazi kuna mmiliki wa shule nyingine nilifahamiana nae nikamuombea kazi pia akapewa kazi masomo yake yalimbeba plus jinsia hii shule wakawa wanamlipa laki 7 na nusu na baada ya miezi 4 akawa academic (academic wa hii shule aliacha kazi so akateuliwa yeye kushika cheo) lakini bado akawa mnyenyekevu saana kwangu
Hii shule mpya na cheo vikamuweka busy saana mimi nikaona kama anateseka vile alafu malipo laki 7 so nikaanza mchakato wa kumtafutia kazi kwenye mashirika kuna mama mmoja nilikuwa na mfahamu ana cheo kikubwa saana UN nikawa nimemwambia kuhusu kumtafutia nafasi kwenye mashirika
Huyu mama akamtafutia NGOs moja ndogo saana ambayo walikuwa hawana mradi wowote so hapakuwa na malipo (alifanya hivyo makusudi ili apate uzoefu na asibanwe na shule kule)
Baada ya mwaka mmoja Yule mother wa UN akaupiga mwingi mzazi mwenzangu akapata kazi IRC so mshahara ukawa mkubwa plus posho nyingi taizi la kwanza akaenda kupanga nyumba ya laki 6 kwa mwezi (kwa kibondo hii nyumba ni classic saana) taizi la pili akaniambia masuala ya ada ya mtoto nimuachie yeye (alifanya hivi ili ampeleke boarding alijua kabisa siwezi kukubali mtoto wa prepo ll kusoma bweni)
Pigo la mwisho ni hii siku ya siku ya mtoto wa Africa aliniomba ruhusa aende dodoma (Alitaka amlete mtoto kwangu hii ni likizo mtoto yupo ili yeye aende huko dodoma) nikawa nimekataa lkn akamleta kwa nguvu mm natoka kazini namkuta mtoto wangu home
So hichi kitendo kikanipa mashaka saana sababu kwenye hii siku IRC wao hawakuwa na ulazima wa kwenda plus umbali aliutumia kumleta mtoto kibondo to kigoma mjini kwa gari ni masaa 5(kwa kutumia mbinu za majasusi wa jamii forum nikahisi tu hapa kuna kitu)
Mzazi mwenzangu alifika kibondo Jumamosi jioni mm jana jumapili asubuhi nikampeleka mtoto kibondo so nilishinda pale na nilimpekua simu yake nikakuta sms ambazo zinaashilia ngono na ndio sababu kubwa iliyompeleka huko