LGE2024 Kama umekuta kituo cha Kuandikisha Wapiga kura hakina Wakala wa Chadema Toa Taarifa kupitia uzi huu, nitafikisha kwa Wahusika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mawakala wengine mpaka wanasusa, ule ubinadamu tu hakuna? Inakuwaje mtu anakuja saa mbili hapati hata chai na anakuja kuletewa chakula tena kidogo sana saa 9 alasiri na hiyo ni Kinondoni huko mikoani Peramiho, Lituhi, Nyasa, Bugarama,Kakola, Kanadi, Ikindilo hali ikoje ? Watu wanataka mabadiliko lakini viongozi sijui ni viongozi wa taifa, mikoa,wilaya au kata ndio wanafanya huu ukatili? Mtu amejitolea kuwa wakala kwanini hapati milo kamili? Refreshments yaani hata maji tu ? Mawakala wa CCM kituo kimoja wapo wanne wanakunywa Supu, maji baridi wwngine soda na juice. Mchana Chipsi na Mishikaki lakini Wakala wa CHADEMA mpaka wanatia huruma midomo imekauka mpaka anatia huruma unatoa sh 2000 anywe hata juice. Kuweni serious aisee, maana Wananchi wana hasira sana na ujinga uliokuwa unafanywa na hawa viongozi wa serikali za mitaa. Wanataka kuwakomesha lakini Wakala hana hata ile morali ya kazi.
 
Ndio maana tumeleta uzi huu
 
Huku vijijini specifically umalila _MBEYA vituo vyote tumewekwa sisi watumishi wa umma na kiukweli sisi wote ni CCM isipokuwa Mimi .

Adha ninayopitia hapa kituo Cha chisonta ni kuwa chakula Sina Wala nauli ya kunitoa hapa chisonta mpaka Ilembo katika kituo changu Cha kazi na ninapoishi ishi hivyo naomba wambie wakuu wetu wanikumbuke nisije fia hapa kwa siku zilizobaki dada
 
Chadema inapeleka mawakala kwenye vituo vya kujiandikisha bila kuwapa hata posho ya chakula mtu anakaa kwanzia Asubuhi hadi jion bila kula chochote huu si ukatili
 
Ndio maana tumeleta uzi huu
Anzeni kufuatilia kwa ukaribu aisee inawavunja moyo na hakuna Wakala wa Chadema ambaye ni mjinga mjinga lakini wanapitia maisha magumu sana na watu wana upendo na chama lakini wanachokipitia Mimi nakional inasikitisha. Ile kufanikisha jambo lazima gharama zitumike kuna meseji whatsapp nimetumiwa aisee, ikabidi niwaforwadie hao viongozi wa jimbo na kata hata kujibu hakuna. CCM wanajiona wanatupiga bao kwa sababu inaonekana uongozi haujali hata mawakala?
 
Ndio maana tumeleta uzi huu
Anzeni kufuatilia kwa ukaribu aisee inawavunja moyo na hakuna Wakala wa Chadema ambaye ni mjinga mjinga lakini wanapitia maisha magumu sana na watu wana upendo na chama lakini wanachokipitia Mimi nakional inasikitisha. Ile kufanikisha jambo lazima gharama zitumike kuna meseji whatsapp nimetumiwa aisee, ikabidi niwaforwadie hao viongozi wa jimbo na kata hata kujibu hakuna. CCM wanajiona wanatupiga bao kwa sababu inaonekana uongozi haujali hata mawakala?
 
Chadema inapeleka mawakala kwenye vituo vya kujiandikisha bila kuwapa hata posho ya chakula mtu anakaa kwanzia Asubuhi hadi jion bila kula chochote huu si ukatili
Inauma sana Mkuu halafu Mawakala wenye uelewa na elimu ya Secondary na chuo kabisa lakini wanachokipata huko kituoni ni mateso na Vijana ni Wahanga wa huu utawala uliopo ma matumaini yapo kwa Chadema . Wanawakatisha sana tamaa na wanavhekwa tu Vijana na Wazee wasiojielewa Mawakala wa CCM
 
iko wazi chadema inajiendesha kwa mkopo, mtakopa wapi pesa ya kumlisha huyo wakala,

halafu mawakala wa chadema wanaona aibu kichizi sijui kwanini..

nadhani wanajijua kua hawana umuhimu na CCM mbona haina na wala hawababaiki 🐒
Nioneshe kituo ambacho CCM hakuna wakala tafadhali.
 
Chadema wanafeli mawakala wamekata tamaa wameacha vituo wazi.
 
ukweli ni kwamba chadema mmeshindwa kujitambua na kuvaa utu kama chama haiwezekani umuweke wakala bila hata chakula cha mchana kisha umwambie atafute chakula cha shilingi elfu tatu eti utamrejeshea pesa yake

baadhi ya makibu wenu wa chama wameaibika vibaya mno kwa kweli
 
Chadema wanafeli mawakala wamekata tamaa wameacha vituo wazi.
Hawajafeli bado kama wataamua kuwezesha hata hizi kampeni na kuwasihi mawakala walioapa kurejea vituoni na kuwalipa posho. Yaani uchaguzi ulikuwa ni mwepesi sana lakini wamejichanganya sana kushindwa kuhudumia mawakala ?
 
Hawajafeli bado kama wataamua kuwezesha hata hizi kampeni na kuwasihi mawakala walioapa kurejea vituoni na kuwalipa posho. Yaani uchaguzi ulikuwa ni mwepesi sana lakini wamejichanganya sana kushindwa kuhudumia mawakala ?
wameshachemka wameonyesha wazi kwa wananchi wao ni watu wa kutafuna ruzuku pekee hayo ndio malengo yao kama chama na sio kingine kwa watanzania

kama chama makini walipaswa kujipambanua katika huu uchaguzi mdogo hiki ni kipimo tosha kwa watanzania
 
Erythrocytes: CHADEMA ikikomaa, itashinda uchaguzi.
 
Kipimo cha chamade cha upinzani kusema tunachukua nchi ni kwenye huu uchaguzi, kwani huu uchaguzi ndio wenye kuonyesha uhai wa chamade kwani upo ngazi ya chini kabisa ngazi ya shina, ambapo ukija kwenye uhalisia hapa CCM ndio wapo vizuri wanaheshimu kupita maelezo ni sehemu ambayo mafungu yanaenda kupita maelezo ukija kwa wapinzani uku ngazi ya shina pamesahaulika balaa

Mfano CDM ya katibu mkuu Dr slaa iliamini sana uku kwenye mashina na alisimamia kuijenga sana sote mashahidi tuliona bendela na matawi ya CDM hata vijijini uko na uchaguzi kama hizi paliwaka moto ila leo hii

Hiyo CDM kwenye mashina haipo kabisa imebakia mijini tu tena baadhi ya maeneo ndio ipo ila iko ishajifia ofisi hazipo wanachama wamepoteana so suala la kuchukua inchi kwenye box la kura tusiongopeane kwa dalili za sasa hakuna hata mwakani wabunge wa ccm watarudi wengi sana kwani uku kwenye mashina CDM imepoteana ukweli tuseme
 
Halafu mkitoka hapo John Mnyika ana akili sana.

Nani anajukumu la kuhakikisha chama kina wakala kwenye kila kituo ni wapiga kura au chama cha siasa.

Nani anatakiwa kuwaambia chama hajapewa posho ni wapiga kura au wakala husika na kama mmejipanga payments zao mngetaka kujua distribution zake.

Viongozi wenu wakuu wako nje ya nchi uchaguzi huu, hawana hata mikakati zaidi ya kuwaachia wapuuzi kuwaaxhia mada za kijinga. Ikiwa wao wamejipanga kupinga uchaguzi tu.

Inataka uwe hamnazo kweli kweli kuwa mfuasi wa chama mfu kama CDM, yaani ni chama hovyo kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…