Kuna siku, nimeenda morogoro kwenye hoteli fulani .
Sasa nilipoingia chumbani, nakuta ndala zipo kama "papa na nguru" yaani tofauti tofauti. Ikabidi nimuulize muhudumu, nikamwambia
Hotel yenu ni kubwa na inapokea watalii kibao na watu wenye hadhi kubwa, kwanini basi mnafanya hivi ndala zinakua za namna hii.?!
Akaniomba samahani sana, akasema wameamua kufanya hivyo baada yakua wakipata hasara ya kununua ndala mara kwa mara.
Maana wateja wengine hua wanaondoka nazo kabisa.
Nikamwambia nahitaji ndala zilizosawa sitaki ndala zilizotofautiana, 150,000 niliyolipa ni kubwa. Ndio akaenda nibadilishia akaleta zilizo fanana.
Ukweli sikuamini kabisa hio sababu aliyoitoa, niliona huenda alikua anatania.
Sasa leo baada ya kusoma hij thread, ndio nimeelewa sasa.