Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Mpaka leo siwezi kuelezea kile kisa lakini mahisi inaweza kuhusishwa na uchawi

Nilikuwa na kawaida ya kurudi home usiku sana, siku hiyo nimerudi mida kama ya saa sita kasoro hivi, mida hii mtaani kwetu kumeshapoa sana, baada ya kufika home nikaenda kwenye dirisha la dogo kumpigia hodi afungue, kando ya kile chumba kuna vyoo na mabafu, jumla vyumba vinne, wakati namita dogo pale nikawa nasikia kutokea chooni kuna mtu kama anatawaza maana sauti ilitokea chooni (ambavyo ni kawaida tu)

Nikahisi tu kuna mtu, nikaendelea kuita na kugonga gonga dirisha, ghafla ule mlango ukawa unafunguliwa hivi, nikawa naangalia ni nani anatoka chooni, japo kulikuwa na kiza kidogo ila niliona mdada amevalia kanga usawa wa kifuani, ghafla ni kama tukawa tunaangaliana (kwa muda mfupi sana) akawa kama kashtuka kuniona, akarudi chooni haraka akiwa amebamiza mlango, nikawa namshangaa, nahisi ni kama alihisi mimi ni mwizi labda, mana dirishani halafu mida ile lazima kidogo mtu akikukuta atahamaki.

Kinachonishangaza ni kwamba, ule mlango ulibamizwa lakini hakufunga kwa ndani, kwa hiyo ukawa unafunguka taratibu, amini usiamini, mwangaza mdogo wa taa ya nje ya nyumba ya jirani iliwezesha kufahamu kama mule ndani kuna mtu ama la, lakini sikuona mtu, mlango ukiwa wazi kabisa, na mimi sikupepesha macho kutazama kwingine labda.

Nilishangaa sana, mwili ukaanza kusisimka, nikachoka mwili, mpaka naondoka home, sijawahi kuingia kile choo na yule dada sijawahi kumfahamu ni nani pale home, maana tulikuwa na nyumba tatu za kupangisha, sijui alitoka ipi kati ya hizo.
 
Hii nakubali mzee mwenzangu, moja ya code ni kwamba uchawi wa kiswahili hauuwezi uchawi wa kizungu.

Kuna nyumba tulipanga kama group tukiwa tunasoma elimu ya ufundi stadi fani ya umeme miaka ya 2000s

Kumbe bwana ile nyumba dalali alitulengesha kwa kuwa alikuwa na shida ya hela.
Nyumba ilishakuwa abondened miaka kibao kutokana na mauzauza yaliyokuwa yanawatokea watu..

Baada ya kuhamia..
Mara msikie joto mara baridi,mara vyombo vinaangushwa mtu hammuoni,mara hatua za mtu, misonyoo na mengineyo ya kukera bahati nzuri alikuwa haguswi mtu.

Ikumbukwe vituko vyote hivyo ni kwa mchana tu....
Balaa la usiku hasa wakati wa kulala katikati ya usingizi mnaweza kusikia kama watu wanakimbia kwenye bati mwanzo wa nyumba mpaka mwisho kama cherehani rrrrrrraaaaahhhhh.....

Kuna muhuni akatoa wazo la hilo la uchawi wa kizungu, kwamba tuconnect waya wa LIVE wa umeme kwenye bati ukipitia kwenye switch, ya kwamba vishindo vikianza ile rrraaaaaahhh tunawasha..
Assee tukafanikiwa, ila kilichotokea pale kijijini kama wangejua ni sisi wangetula nyama.....
Kulitokea nini
 
Elezea vzuri mkuu
 
Biashala ina mambo mengi ndugu uchawi ktk biashala upo nakupa kisa kimoja hivi miaka ya nyuma nilifanya biashala ya duka maeneo ya kwa mkandawile huko nikawa nikiweka mtaji biashala nauza vizuri ila hela jioni siioni nikajiongeza mana pale kulikuwa na waha wanauza hao mpk basi basi nikaenda sehemu kwa mzee mmoja kule Kunduchi yy ni marehemu kwa sasa akaniangalia nyota akasema inabidi kazi yako tuifanye siku ya j5 kulingana na ulivyo ila apatikane kuku mweupe ambaye tutatoa damu yake kweli nikaacha hela ya kuku pale nikaondoka siku nimefika akafanya mambo yake na akanichanja chale kadhaa mwilini yule mzee ni mha akaniambia nakupa hii azima kaiweke dukani kwako huyo ni jini atakuwa anakujazia bidhaa pale dukani na ndio wafanyabiashala wakubwa wanamtumia akanipa na masharti kadhaa basi nakumbuka nilikimbiza pale ila nilikuja kukosea sharti moja kila kitu kikafa ila tangu hapo hakuna ninachofanya kikaenda sawa tena mpk sasa
Huyo mzee alikuwa anaitwa Turashashe, bilashaka
 
hapo ni hata sijakusoma mkuu!!

yaan mwaka 1992 ndio ushuhuda wako wa kwanza ukiwa unafundisha shule X

halafu ushuhuda wako wa mwisho ni mwaka 2009 ukiwa field liwale wakati huo inasoma chuo cha sauti mtwara

hoja yangu sasa, yaani ulianza kufundisha kabla haujawa mwl?
Hujui watu Huwa wanajiendeleza ndugu. Jiongeze kwwnye kufikiria
 
Mimi ninamiaka 7 naumwa kitu kisichoeleweka. Nashangaa zamani watu walikua wananipenda hata nilipokua naongea walipenda kunisikiliza pia walipenda kuwa karibu na mimi ,lakini baada ya kuanza kupata matatizo rafiki ote wamekimbia ,hata nikikaa kwenye seat ya gari hakuna atakae tamani kukaa na mimi na ata akikaa anaweza kuhama, ninaweza nikawa napita njiani mtu akanikwepa yaani akabadirisha njia kisa mimi na hapo hatujuani, yaani nina nyota ya kutengwa na watu kila nitakachofanya lazima nifeli, kuhusu ugonjwa wangu mtu hawezi ujua hadi nimwambie au awe ndugu wa karibu, na kila nikitaka kwenda hospital usiku kabla ya kwenda nakua muoga sana yaani napata sonona, mpaka sasa sijapona ,sijui nini shida
 
Wakuu habari zenu, ni matumaini yangu kuwa hamjambo.

Leo nataka kuweka ushuhuda wangu kwa niliyoyashuhudia live juu ya nguvu za giza, kwa wasioamini nadhani uzi huu hautakuwa na thamani kwao, kama na wewe unao ushuhuda usisahau kushea nasi.

1. Ushuhuda wangu unaanzia mwaka 1992 nikiwa nafundisha shule X wilaya ya Sengerema, kuna mwalimu nilikuwa nafundisha naye kituo kimoja.

Siku hiyo kuna kamvua kalinyesha sana, baada ya kupungua mwalimu mwenzangu alimuagiza mtoto wake wa kiume aliyekuwa akisoma darasa la kwanza kwenda kuchuma maharage shambani.

Bahati mbaya mtoto akiwa shambani aligongwa/aliumwa na nyoka na kupeleka kifo, tulifanya taratibu za mazishi na kumsitiri mtoto huyo.

Cha kushangaza mwaka 2008 mtoto huyo alionekana akiwa uchi na nywele ndefu sana alikuja moja kwa moja nyumbani na kupitiliza ndani nyumbani kwao, alikuwa ameshakuwa baba mzima, nywele zilikuwa ndefu sana pamoja na mikono iliyofikia usawa wa magoti.

Watu walistaajabu sana lakini hakudumu sana alifariki baada ya kukaa uraiani kwa wiki mbili.

2. Ushuhuda wangu bado unabaki huko huko Sengerema katika kijiji cha Bubandwamhela.

Nikiwa nafundisha shule X, kuna binti kijijini aliyekuwa akisoma darasa la saba aliugua ghafla baada ya kutoka shuleni.

Wazazi wake walipompeleka hospitali daktari aliwaambia mtoto hana ugonjwa, wazazi waliamua kujiongeza na kumpeleka kwa mganga wa jadi.

Cha kushangaza kesho yake shangazi ya binti alikutwa kwa mganga akiwa uchi, huku akiweweseka na akili zimemruka, shangazi mtu alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini kwa kuwa serikali haiamini ushirikina aliachiwa huru, lakini hadi leo hii alishakuwa chizi. Binti yeye alipona kabisa.

3. Kisa cha tatu na mwisho ni hiki kilichotokea Liwale shule ya sekondari X nikiwa na walimu wenzangu ambao tulikuwa tunasoma chuo cha SAUT-Mtwara.

Tulipangiwa field katika wilaya ya Liwale ilikuwa mwaka 2009, mwanachuo mwenzetu akiwa zamu siku hiyo alikumbana na mtoto ambaye kwao iliaminika kuwa bibi yake alikuwa mtaalamu wa mambo ya giza.

Mwanafunzi huyo alichelewa kufika shule, mwalimu alipotaka kumuadhibu aligoma, wakasumbuana sana mwisho wa siku akamuadhibu yakaisha, jioni tukiwa uwanjani tunafanya mazoezi yule mwanachuo mwenzangu alianguka na kupoteza fahamu, ikawa jumla hadi kifo.

Kama na wewe umewahi kukutana/kushuhudia live ushirikina share nasi kisa chako watu tupate ilimu.

Mungu ni mwema siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni ishara ya wewe kujikita kwenye ushirikina, kuna nguvu fulani ya giza inakuita. Hujapata dalili zozote za kusikia mtu anakuita usiku ama kuota ndoto unachapa demu mkali kishenzi na ukiamka unakuta kitanda kimeloa tu?
 
Mimi ninamiaka 7 naumwa kitu kisichoeleweka. Nashangaa zamani watu walikua wananipenda hata nilipokua naongea walipenda kunisikiliza pia walipenda kuwa karibu na mimi ,lakini baada ya kuanza kupata matatizo rafiki ote wamekimbia ,hata nikikaa kwenye seat ya gari hakuna atakae tamani kukaa na mimi na ata akikaa anaweza kuhama, ninaweza nikawa napita njiani mtu akanikwepa yaani akabadirisha njia kisa mimi na hapo hatujuani, yaani nina nyota ya kutengwa na watu kila nitakachofanya lazima nifeli, kuhusu ugonjwa wangu mtu hawezi ujua hadi nimwambie au awe ndugu wa karibu, na kila nikitaka kwenda hospital usiku kabla ya kwenda nakua muoga sana yaani napata sonona, mpaka sasa sijapona ,sijui nini shida
Mchawi wetu wa JF Mshana Jr ebu njoo umsaidie kiumbe huyu anateseka mno.
 
Mimi ninamiaka 7 naumwa kitu kisichoeleweka. Nashangaa zamani watu walikua wananipenda hata nilipokua naongea walipenda kunisikiliza pia walipenda kuwa karibu na mimi ,lakini baada ya kuanza kupata matatizo rafiki ote wamekimbia ,hata nikikaa kwenye seat ya gari hakuna atakae tamani kukaa na mimi na ata akikaa anaweza kuhama, ninaweza nikawa napita njiani mtu akanikwepa yaani akabadirisha njia kisa mimi na hapo hatujuani, yaani nina nyota ya kutengwa na watu kila nitakachofanya lazima nifeli, kuhusu ugonjwa wangu mtu hawezi ujua hadi nimwambie au awe ndugu wa karibu, na kila nikitaka kwenda hospital usiku kabla ya kwenda nakua muoga sana yaani napata sonona, mpaka sasa sijapona ,sijui nini shida
Bado kidogo, usife Moyo
 
Juzi nimekaa mahali napunga upepo kumbe pembeni kuna makaburi.
Mi nna yangu nakula vyombo vyangu napata upepo nikamuona maza mmoja mbele yangu.hawa dizaini ushungi style na baibui lake.
Mwanzoni sikumtilia maanani,badae nikaanza kushtuka huyu maza vp maana alikua anataja maneno ya qurani kwa uchungu sana,
Anapiga magoti anaamka anaendelea mi napiga chabo tu yaani kitendo amepanda juu ya hilo tuta kamyanyua mikono juu mi nageuka tu nipige funda bia yangu namaliza nimeishia kuskia akbaru.
Kapotea pale aliposimama.
Ebo nikapangusa uso labda naota wapi.
Nikazunguruka labda nimuone anaondoka.
Wapi.
Alizama pale juu aliposimama kwenye lile tuta la mumewe.
Nilitoka baru haraka sana.
 
Hii nakubali mzee mwenzangu, moja ya code ni kwamba uchawi wa kiswahili hauuwezi uchawi wa kizungu.

Kuna nyumba tulipanga kama group tukiwa tunasoma elimu ya ufundi stadi fani ya umeme miaka ya 2000s

Kumbe bwana ile nyumba dalali alitulengesha kwa kuwa alikuwa na shida ya hela.
Nyumba ilishakuwa abondened miaka kibao kutokana na mauzauza yaliyokuwa yanawatokea watu..

Baada ya kuhamia..
Mara msikie joto mara baridi,mara vyombo vinaangushwa mtu hammuoni,mara hatua za mtu, misonyoo na mengineyo ya kukera bahati nzuri alikuwa haguswi mtu.

Ikumbukwe vituko vyote hivyo ni kwa mchana tu....
Balaa la usiku hasa wakati wa kulala katikati ya usingizi mnaweza kusikia kama watu wanakimbia kwenye bati mwanzo wa nyumba mpaka mwisho kama cherehani rrrrrrraaaaahhhhh.....

Kuna muhuni akatoa wazo la hilo la uchawi wa kizungu, kwamba tuconnect waya wa LIVE wa umeme kwenye bati ukipitia kwenye switch, ya kwamba vishindo vikianza ile rrraaaaaahhh tunawasha..
Assee tukafanikiwa, ila kilichotokea pale kijijini kama wangejua ni sisi wangetula nyama.....
Kulikuwa na panya buku humo maybe
 
Back
Top Bottom