Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,680
- 2,779
Mpaka leo siwezi kuelezea kile kisa lakini mahisi inaweza kuhusishwa na uchawi
Nilikuwa na kawaida ya kurudi home usiku sana, siku hiyo nimerudi mida kama ya saa sita kasoro hivi, mida hii mtaani kwetu kumeshapoa sana, baada ya kufika home nikaenda kwenye dirisha la dogo kumpigia hodi afungue, kando ya kile chumba kuna vyoo na mabafu, jumla vyumba vinne, wakati namita dogo pale nikawa nasikia kutokea chooni kuna mtu kama anatawaza maana sauti ilitokea chooni (ambavyo ni kawaida tu)
Nikahisi tu kuna mtu, nikaendelea kuita na kugonga gonga dirisha, ghafla ule mlango ukawa unafunguliwa hivi, nikawa naangalia ni nani anatoka chooni, japo kulikuwa na kiza kidogo ila niliona mdada amevalia kanga usawa wa kifuani, ghafla ni kama tukawa tunaangaliana (kwa muda mfupi sana) akawa kama kashtuka kuniona, akarudi chooni haraka akiwa amebamiza mlango, nikawa namshangaa, nahisi ni kama alihisi mimi ni mwizi labda, mana dirishani halafu mida ile lazima kidogo mtu akikukuta atahamaki.
Kinachonishangaza ni kwamba, ule mlango ulibamizwa lakini hakufunga kwa ndani, kwa hiyo ukawa unafunguka taratibu, amini usiamini, mwangaza mdogo wa taa ya nje ya nyumba ya jirani iliwezesha kufahamu kama mule ndani kuna mtu ama la, lakini sikuona mtu, mlango ukiwa wazi kabisa, na mimi sikupepesha macho kutazama kwingine labda.
Nilishangaa sana, mwili ukaanza kusisimka, nikachoka mwili, mpaka naondoka home, sijawahi kuingia kile choo na yule dada sijawahi kumfahamu ni nani pale home, maana tulikuwa na nyumba tatu za kupangisha, sijui alitoka ipi kati ya hizo.