Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Mpaka leo siwezi kuelezea kile kisa lakini mahisi inaweza kuhusishwa na uchawi

Nilikuwa na kawaida ya kurudi home usiku sana, siku hiyo nimerudi mida kama ya saa sita kasoro hivi, mida hii mtaani kwetu kumeshapoa sana, baada ya kufika home nikaenda kwenye dirisha la dogo kumpigia hodi afungue, kando ya kile chumba kuna vyoo na mabafu, jumla vyumba vinne, wakati namita dogo pale nikawa nasikia kutokea chooni kuna mtu kama anatawaza maana sauti ilitokea chooni (ambavyo ni kawaida tu)

Nikahisi tu kuna mtu, nikaendelea kuita na kugonga gonga dirisha, ghafla ule mlango ukawa unafunguliwa hivi, nikawa naangalia ni nani anatoka chooni, japo kulikuwa na kiza kidogo ila niliona mdada amevalia kanga usawa wa kifuani, ghafla ni kama tukawa tunaangaliana (kwa muda mfupi sana) akawa kama kashtuka kuniona, akarudi chooni haraka akiwa amebamiza mlango, nikawa namshangaa, nahisi ni kama alihisi mimi ni mwizi labda, mana dirishani halafu mida ile lazima kidogo mtu akikukuta atahamaki.

Kinachonishangaza ni kwamba, ule mlango ulibamizwa lakini hakufunga kwa ndani, kwa hiyo ukawa unafunguka taratibu, amini usiamini, mwangaza mdogo wa taa ya nje ya nyumba ya jirani iliwezesha kufahamu kama mule ndani kuna mtu ama la, lakini sikuona mtu, mlango ukiwa wazi kabisa, na mimi sikupepesha macho kutazama kwingine labda.

Nilishangaa sana, mwili ukaanza kusisimka, nikachoka mwili, mpaka naondoka home, sijawahi kuingia kile choo na yule dada sijawahi kumfahamu ni nani pale home, maana tulikuwa na nyumba tatu za kupangisha, sijui alitoka ipi kati ya hizo.
 
Kulitokea nini
 
Elezea vzuri mkuu
 
Huyo mzee alikuwa anaitwa Turashashe, bilashaka
 
Hujui watu Huwa wanajiendeleza ndugu. Jiongeze kwwnye kufikiria
 
Mimi ninamiaka 7 naumwa kitu kisichoeleweka. Nashangaa zamani watu walikua wananipenda hata nilipokua naongea walipenda kunisikiliza pia walipenda kuwa karibu na mimi ,lakini baada ya kuanza kupata matatizo rafiki ote wamekimbia ,hata nikikaa kwenye seat ya gari hakuna atakae tamani kukaa na mimi na ata akikaa anaweza kuhama, ninaweza nikawa napita njiani mtu akanikwepa yaani akabadirisha njia kisa mimi na hapo hatujuani, yaani nina nyota ya kutengwa na watu kila nitakachofanya lazima nifeli, kuhusu ugonjwa wangu mtu hawezi ujua hadi nimwambie au awe ndugu wa karibu, na kila nikitaka kwenda hospital usiku kabla ya kwenda nakua muoga sana yaani napata sonona, mpaka sasa sijapona ,sijui nini shida
 
Hii ni ishara ya wewe kujikita kwenye ushirikina, kuna nguvu fulani ya giza inakuita. Hujapata dalili zozote za kusikia mtu anakuita usiku ama kuota ndoto unachapa demu mkali kishenzi na ukiamka unakuta kitanda kimeloa tu?
 
Mchawi wetu wa JF Mshana Jr ebu njoo umsaidie kiumbe huyu anateseka mno.
 
Bado kidogo, usife Moyo
 
Juzi nimekaa mahali napunga upepo kumbe pembeni kuna makaburi.
Mi nna yangu nakula vyombo vyangu napata upepo nikamuona maza mmoja mbele yangu.hawa dizaini ushungi style na baibui lake.
Mwanzoni sikumtilia maanani,badae nikaanza kushtuka huyu maza vp maana alikua anataja maneno ya qurani kwa uchungu sana,
Anapiga magoti anaamka anaendelea mi napiga chabo tu yaani kitendo amepanda juu ya hilo tuta kamyanyua mikono juu mi nageuka tu nipige funda bia yangu namaliza nimeishia kuskia akbaru.
Kapotea pale aliposimama.
Ebo nikapangusa uso labda naota wapi.
Nikazunguruka labda nimuone anaondoka.
Wapi.
Alizama pale juu aliposimama kwenye lile tuta la mumewe.
Nilitoka baru haraka sana.
 
Kulikuwa na panya buku humo maybe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…