Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kisa kingine nilikisikia kilitokea maeneo ya sumbawanga

Kuna mzee wamakamo alikua ni tajiri sana, pesa zake haweki benk na hata akienda kufanya manunuzi hua haweki kwenye wallet kuzistiri zisionekane yeye hua anazishikilia tu kama wanafunzi wanavyoshika vitini vyao mikononi

Siku moja kuna kosi la majambazi lilijipanga kwenda kumvamia

Walimkuta yuko nyumbani kwake ameshikilia pesa akipata upepo kwenye garden yake

Wakamnyooshea bastola na kumwambia atulie kimya kisha atoe kila kitu alichonacho

Yule mzee akachukua zile pesa akazibana kwenye kwapa lake huku akitetemeka kwa woga

majambazi wakamsisitiza kua anyanyue mikono juu, mzee akatii amri kwa kunyanyua mikono juu kisha pesa alizozibana kwapani zikaanguka chini majambazi wakaziokota

Wakamwambia tena "toa kila kitu ulichonacho"

Round hii unaambiwa mzee alichomoa kichwa chake akakishika mkononi halafu kile kichwa kikiwa mkononi kikatoa sauti ikisema

"sina chochote jamani nina kichwa tu
 
Kijiji kimoja mkoa X, mzee mmoja alipowaona kuku wa jirani wanashambulia mahindi shambani mwake akaamua kuwatimua kwa kuwapiga na mawe.
Alipoamka asubuhi akajikuta mguu mmoja umetoka uko pembeni hakuna damu wala nini, akiwa katika taharuki nini afanye akalala tena kuamka kesho yake mguu wa pili pia umetoka uko pembeni.
Mpaka leo huyo jamaa yuko na ameshakuwa mzee haelewi nini kilimkuta anatumia wheel chair, uchawi upo.
Mhhh hii chai Yaani mtu mguu utoke halafu apatwe na usingizi alale tena ?? You can't be serious mguu ukitoka huo usingizi utaupata wapi!?
 
Hiki ni kama nilivyosikia kinasimuliwa juzi Kati.

Kuna jamaa walikuwa wanatoka dar kuelekea Mtwara,wakiwa njiani wakafika Lindi maeneo ya mandawa kuna kimlima hivi gari ikazingua kitu kidogo cha kurekebisha waendelee na safari mmoja wao akabanwa na haja ndogo akasogea akajisaidia basi tenngeneza gari likagoma.Dereva akapigiwa simu na dereva mwenzake akamueleza mahali walipo huyo dereva akasikitika aisee mmeharibikiwa hapo msala.

Gari likagoma ikabidi walale saa nane usiku wakashangaa dogo kama ana miaka 6 akatokea akasimama mbele ya ile gari akacheka sana Kwa nguvu akapotea jamaa uoga ikabidi wachune Tu ndani ya gari wanajisaidia kwenye chupa saa 12 asubuhi akaja jamaa kama chizi hivi akawa anaizunguka ile gari akasikitika anaongea mmepata tabu sana anazunguka tu, akaondoka akaja mbibi akasimama akaawangalia akaondoka kukawa kumekucha sasa wanapiga hesabu wafungue kifaa kilicho haribika wapeleke Kwa fundi,mmoja wao akataka kujisaidia tena ikatokea sauti ya mzee hakuna kujisaidia hapo ondokeni haraka huyo mzee akatokea wakamwambia gari ni mbovu akasema gari sio mbovu ondokeni dereva kuwasha gari nzima wakaendelea na safari kumbe kosa ni jamaa alivyojisaidia bwana.
😁😁😁😁 Ancestors hao Kmmk show zao sio mbovu
 
Wakuu habari zenu, ni matumaini yangu kuwa hamjambo.

Leo nataka kuweka ushuhuda wangu kwa niliyoyashuhudia live juu ya nguvu za giza, kwa wasioamini nadhani uzi huu hautakuwa na thamani kwao, kama na wewe unao ushuhuda usisahau kushea nasi.

1. Ushuhuda wangu unaanzia mwaka 1992 nikiwa nafundisha shule X wilaya ya Sengerema, kuna mwalimu nilikuwa nafundisha naye kituo kimoja.

Siku hiyo kuna kamvua kalinyesha sana, baada ya kupungua mwalimu mwenzangu alimuagiza mtoto wake wa kiume aliyekuwa akisoma darasa la kwanza kwenda kuchuma maharage shambani.

Bahati mbaya mtoto akiwa shambani aligongwa/aliumwa na nyoka na kupeleka kifo, tulifanya taratibu za mazishi na kumsitiri mtoto huyo.

Cha kushangaza mwaka 2008 mtoto huyo alionekana akiwa uchi na nywele ndefu sana alikuja moja kwa moja nyumbani na kupitiliza ndani nyumbani kwao, alikuwa ameshakuwa baba mzima, nywele zilikuwa ndefu sana pamoja na mikono iliyofikia usawa wa magoti.

Watu walistaajabu sana lakini hakudumu sana alifariki baada ya kukaa uraiani kwa wiki mbili.

2. Ushuhuda wangu bado unabaki huko huko Sengerema katika kijiji cha Bubandwamhela.

Nikiwa nafundisha shule X, kuna binti kijijini aliyekuwa akisoma darasa la saba aliugua ghafla baada ya kutoka shuleni.

Wazazi wake walipompeleka hospitali daktari aliwaambia mtoto hana ugonjwa, wazazi waliamua kujiongeza na kumpeleka kwa mganga wa jadi.

Cha kushangaza kesho yake shangazi ya binti alikutwa kwa mganga akiwa uchi, huku akiweweseka na akili zimemruka, shangazi mtu alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini kwa kuwa serikali haiamini ushirikina aliachiwa huru, lakini hadi leo hii alishakuwa chizi. Binti yeye alipona kabisa.

3. Kisa cha tatu na mwisho ni hiki kilichotokea Liwale shule ya sekondari X nikiwa na walimu wenzangu ambao tulikuwa tunasoma chuo cha SAUT-Mtwara.

Tulipangiwa field katika wilaya ya Liwale ilikuwa mwaka 2009, mwanachuo mwenzetu akiwa zamu siku hiyo alikumbana na mtoto ambaye kwao iliaminika kuwa bibi yake alikuwa mtaalamu wa mambo ya giza.

Mwanafunzi huyo alichelewa kufika shule, mwalimu alipotaka kumuadhibu aligoma, wakasumbuana sana mwisho wa siku akamuadhibu yakaisha, jioni tukiwa uwanjani tunafanya mazoezi yule mwanachuo mwenzangu alianguka na kupoteza fahamu, ikawa jumla hadi kifo.

Kama na wewe umewahi kukutana/kushuhudia live ushirikina share nasi kisa chako watu tupate ilimu.

Mungu ni mwema siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nilimkuta jirani yangu [pisi kali-kumbe mchawi]..shambani kwangu saa 8 usiku,PUGU MWAKANGA!!!,,,aliponiona alistuka mno!!,,,nikamwambia ukitaka yaishie hapa,2malizane hapahapa!!,,,,akalala kifo chamende[alikuwa hana pichu],,,,,,,,NIKAMLELKEA MOTO!!!!,,,,,,,,,,,,,mpala leo nampelekea MOTO,,,asikwambie m2 kutokana na wachawi kuoga kwa miti shamba mbalimbali basi wana JOTO balaa!!!
 
Biashala ina mambo mengi ndugu uchawi ktk biashala upo nakupa kisa kimoja hivi miaka ya nyuma nilifanya biashala ya duka maeneo ya kwa mkandawile huko nikawa nikiweka mtaji biashala nauza vizuri ila hela jioni siioni nikajiongeza mana pale kulikuwa na waha wanauza hao mpk basi basi nikaenda sehemu kwa mzee mmoja kule Kunduchi yy ni marehemu kwa sasa akaniangalia nyota akasema inabidi kazi yako tuifanye siku ya j5 kulingana na ulivyo ila apatikane kuku mweupe ambaye tutatoa damu yake kweli nikaacha hela ya kuku pale nikaondoka siku nimefika akafanya mambo yake na akanichanja chale kadhaa mwilini yule mzee ni mha akaniambia nakupa hii azima kaiweke dukani kwako huyo ni jini atakuwa anakujazia bidhaa pale dukani na ndio wafanyabiashala wakubwa wanamtumia akanipa na masharti kadhaa basi nakumbuka nilikimbiza pale ila nilikuja kukosea sharti moja kila kitu kikafa ila tangu hapo hakuna ninachofanya kikaenda sawa tena mpk sasa
Na siku zotee kujitoa upande wa Giza ni kupoteza.

Binafsi niweke wazi Kuna DAWA ipo ni miti kadhaa unaweza kujitengenezea ni formular nimesahau jinsi ya kuitengeneza maana ni miaka mingi Sasa.

Hiyo DAWA unainyunyiza kwenye mafuta ya mgando ni kwa ajir ya kumnasa MWANAMKE YEYOTE UMTAKAE IPO IVIIII unachukua ki portion kidogo cha DAWA unajipaka kwenye kiganja cha mkononiiiii sharti inatakiwa UMGUSE KWA KUMSALIMIA MKONONI AU UMGUSE SEHEMU YEYOTE IWE BEGANI MKONONIIIII ONE TOUCH.

THEN YULE DADA ATAKUELEWA NA KUKUPENDA SANA SANAA SANAAAAAA ILA MAPENZI YA DAWA MWISHO WAKE HUWA NI MBAYA MNAWEZAA KUACHANA MPAKA MKASHANGAA

MAMBO YA DAWA NA USHIRIKINA NI YA KWENDA NAYO KWA TAHADHALII SANAA SANAAAAAA

Cc.
min -me
Monetary doctor
Mshana Jr
MENEMENE TEKERI NA PERESI
 
Na siku zotee kujitoa upande wa Giza ni kupoteza.

Binafsi niweke wazi Kuna DAWA ipo ni miti kadhaa unaweza kujitengenezea ni formular nimesahau jinsi ya kuitengeneza maana ni miaka mingi Sasa.

Hiyo DAWA unainyunyiza kwenye mafuta ya mgando ni kwa ajir ya kumnasa MWANAMKE YEYOTE UMTAKAE IPO IVIIII unachukua ki portion kidogo cha DAWA unajipaka kwenye kiganja cha mkononiiiii sharti inatakiwa UMGUSE KWA KUMSALIMIA MKONONI AU UMGUSE SEHEMU YEYOTE IWE BEGANI MKONONIIIII ONE TOUCH.

THEN YULE DADA ATAKUELEWA NA KUKUPENDA SANA SANAA SANAAAAAA ILA MAPENZI YA DAWA MWISHO WAKE HUWA NI MBAYA MNAWEZAA KUACHANA MPAKA MKASHANGAA

MAMBO YA DAWA NA USHIRIKINA NI YA KWENDA NAYO KWA TAHADHALII SANAA SANAAAAAA

Cc.
min -me
Monetary doctor
Mshana Jr
MENEMENE TEKERI NA PERESI
Bruh upo pande hizi pia
 
Na siku zotee kujitoa upande wa Giza ni kupoteza.

Binafsi niweke wazi Kuna DAWA ipo ni miti kadhaa unaweza kujitengenezea ni formular nimesahau jinsi ya kuitengeneza maana ni miaka mingi Sasa.

Hiyo DAWA unainyunyiza kwenye mafuta ya mgando ni kwa ajir ya kumnasa MWANAMKE YEYOTE UMTAKAE IPO IVIIII unachukua ki portion kidogo cha DAWA unajipaka kwenye kiganja cha mkononiiiii sharti inatakiwa UMGUSE KWA KUMSALIMIA MKONONI AU UMGUSE SEHEMU YEYOTE IWE BEGANI MKONONIIIII ONE TOUCH.

THEN YULE DADA ATAKUELEWA NA KUKUPENDA SANA SANAA SANAAAAAA ILA MAPENZI YA DAWA MWISHO WAKE HUWA NI MBAYA MNAWEZAA KUACHANA MPAKA MKASHANGAA

MAMBO YA DAWA NA USHIRIKINA NI YA KWENDA NAYO KWA TAHADHALII SANAA SANAAAAAA

Cc.
min -me
Monetary doctor
Mshana Jr
MENEMENE TEKERI NA PERESI
Huku nilipo kuna mpaka dawa ya kuweka mdomoni ukimuita mdada jina lake akiitika basi imeisha hiyo ni wewe utake kwenda kupiga au umsamehe
 
dah nmesoma sana ngoja na mimi ntoe kisa kilichosababisha niape kuwa sitakwenda kwa mganga tena kwenye maisha yangu.

ilikuwa 2002,tunatoka dar tunakwenda mkoa wa kigoma kwa wanojua bara bara enzi hizo wanajua ni jinsi gani kulikuwa na majambazi hasa ndani ya mapori ya Tabora,bahati haikuwa yetu mida ya saa 5 usiku wakati tupo road tukakuta bara bara imewekwa bonge la gogo mzee akataka kujitahid aligeuze ghafla walitokea watu wamebeba bunduki ndo kwa mara yangu ya kwanza kuone mtu kashka bunduki huku kajizungushia mkanda wa risasi mwilini bro wangu ile kuwaona tu akakata moto tuliokuwa hatujazmia tulikuwa watatu 3 mimi mzee na bimkubwa.

Tulichezea sana vitasa mzee alidhalilika mno mwisho wa siku walichukua mpka viatu nakumbuka viatu vyangu vya kitoto vya kuwaka taa,then wakaondoka mpka na gari tulikaa pale mpka saa 11 ndo tukapata msaada tukaenda polisi but hawakuwa na msaada mzee akapiga simu kigoma ikatumwa nauli tukaenda moja kwa moja mpka kwa baba yake(means babu),sasa babu yeye kila alivyokuwa anahadithiwa alikuwa anacheka mno hasa akimuangalia bro na ujanja wake ote et kazimia,upande wa baba yeye alikuwa na hasira mno alichokuwa anataka yeye ni wale watu awashikishe adabu hata kufa wafe basi ilivyofika usiku tukaelekea sehemu fulani inaitwa ujiji kwa mzee fulani alikuwa anaitwa juma njemba.

Nadhani kwa watu wa kigoma wanaweza kuwa wanamjua,akaelezewa kila kitu akasema hicho ni kitu kidogo sana,huku na yeye anacheka kisha akasema kuwa pale kwake kuna mbuzi alimchinja sababu ya sherwhe ya mwanae hvyo itatubidi tumtafutie mbuzi mwengne amreplace ili iwe kama malipo yake baba akakubali,kilichofata akawaita wajukuu zake walete (ubumba) ni udongo fulani hivi wa mfinyanzi kisha akawa anatengeneza kimdoli kidogo cha udongo kama vile vya kitoto toto,baada ya kukitengeneza akaanza kukiandika maneno yake kisha akakisimamisha chini,then akaanza kuongea maneno yake aliongea sana baada kama ya saa 1 akasema mtu yoyote ndani ya hichi chumba haruhusiwi kukimbia wala kupiga kelele kwani kwa kufanya hivyo ndo itakuwa kifo chake.

Basi aliendele kusema maneno yake ghafla yule mdoli pole pole alianza kukua na kuwa mkubwa pole pole,baada kama ya dakika arobaini alikuwa ni mkubwa kama binadamu mwenye mwili mkubwa alikuwa anamkono na kifua kikubwa na mrefu,kwa mara ya pili bro tena akazimia kwa mara ya pili mim mkojo ulishantoka natetemeka kama nmepatwa na dege dege,mwisho yule mdoli akaambiwa shtaka letu kisha akaambiwa nenda hivi vitu vinatakiwa leo leo,theb yule mtu akafungua mlango akatoka mbio alikuwa ni mwanaume lakini yupo uchi na ni mweusi tii kama mkaa mpka macho hakuwa na ichi kiini cheupe ye alikuwa na kiini cha moja kwa moja cha weusi,alivyoondoka tukaanza kumpepea na kumwagia maji bro alivyoshtuka yule mzee akatuambia kazi imeshakwisha kesho mtayapata majibu yenu.


Ilivyofika asubuhi tukapigiwa simu nakumbuka enzi hizo kulikuwa kuna buzz siyo hii tigo na hata simu zilikuwa za mezani,tukaambiwa kuwa kuna gari imepatikana Tabora yenye namba kama tuliyoripoti pamoja na vitu vingine,tukaanza safari na treni mpka tabora kufika kule tukakuta vitu vyetu na vingne vingi tu ila mzee alisema vyote vilikuwa vyetu hela zilikuwa kama 1m lakini zilipatikana 7m polisi hawakuchukua hata cent na hata walivyopewa walikataa kata kata hakikupotea hata kifungo kisha baada ya kuchukua tukaambiwa kuwa hao majambazi waliotuibia walikutwa msituni wakiwa wameuwawa wakasema wanahisi ni wanyama wakali ndo waliwauwa maana walikuwa wanaalama za meno makali milini mwao na kucha.

lakini wakashndwa kuelewa kama ni wanyama ndo waliwashambulia ni wanyama aina gani na kwanini hawakuwapiga hata risasi moja hao wanyama na wakati walikuwa na silaha nzito?Baada ya maelezo mengi mzee akawasha gari mpka kigoma stend ya kwanza mpka kwa yule mganga tulinunua mbuzi na zawadi nyingne nying lakini mzee aligoma hakutaka chochote zaidi ya mbuzi tu,basi tukampka mbuzi wake, akasema imebaki kazi moja tu na kazi yenyewe ni kumrudisha yule kiumbe(mdoli mtu)ili asitudhuru na sisi maana ni wetu hapo mdipo ilipokuwa mtihani maana kuna msharti mengi tulikosea plus kujisahau sasa akawa anatuandama sisi atuue dah kila mmoja nyumbani anaalama ya yule kiumbe yangu ni kungatwa skio na kula kipande nikipata mda ntawamalizia kisa changu but mpka leo mimi kwenda kwa waganga ni big no,but thanks god tulitoka salama


picha ya nilipongatwa kwenye skio ambyo ni alama ambayo sitaweza isahau mpka kifo

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah! Umetisha sana Mzee Baba.
 
Back
Top Bottom