Ni 2016 nilivyokuwa nime maliza kidato Cha 4 nikaona Kwa muda ambao nasubiria matokeo niende mgodini, mahesabu yangu yalikuwa kama nikifanikiwa huko basi mambo ya shule naachana nayo.
Nikapata wazo kabla ya kwenda mgodini niende kwanza Kwa mganga maana stori zilizo kuwepo ni kwamba ukienda Kwa mganga akakusafishia njia inakuwa ni rahisi kufanikiwa huko, ikabidi nifunge safari mpaka singida kiyomboi huko alikuwepo mtaalam ambaye alikuwa amevuma Kwa wakati huo.
Nilivyo fika akaniambia gharama ni laki mbili tu, nikampa laki akaniambia hiyo laki nyingine nitaenda kumalizia siku nitakapo rudi kutoa shukrani, hapo hapo akaanza kuniangalizia kutumia vifaa vyake, Baada ya hapo akanipeleka sehemu Kuna kama msitu flani hivi tukaingia kati kati, tulivyo fika mle akaniambia nikae chini huku nimevaa shuka tu jeusi akaniambia baada ya muda utaona kamba mazingira haya utaichukua uje nayo nyumbani, yeye akawa ameondoka.
Niliendelea kukaa pale huku nikiangaza huku na kule Ili nione kamba lakini wapi, nikiwa nimesha kaa muda mrefu mara akaja nyoka mkubwa nilipo kuwa na akawa ananisogelea taratibu huku katoa ulimi, ilibidi nikimbie Kwa woga mpaka nyumbani Kwa mganga nikamueleza hilo tukio, alinifokea sana na akataka kunifukuza kwake, kiukweli yule nyoka kumbe ndo kamba yenyewe ndo alicho maanisha mganga.
Nilimsihi mganga anisamehe na mwisho akanisamehe, kesho yake akanipeleka sehemu tena Kuna mlima mkubwa ni sehemu ambayo watu hupita wakati wanaenda mashamba ya mbali, tukiwa tupo chini bondeni kabisa mganga akaniambia Anza kupanda hii barabara na upite katikati yake mpata utakapo fika mwisho, mganga yeye akawa ametoweka nikaanza kupanda taratibu, nikiwa kati kati ya mlima niliona farasi wa 4 wakubwa kama tembo Wana shuka Kwa kasi ya ajabu huku nyuma Yao Kuna vumbi jingi mno, nilijikaza Ili nisiwapishe lakini nikashindwa nilijikuta najirusha pembeni, muda ule ule ndani ya saa Ile Ile nilijikuta Niko nyumbani kwetu Morogoro tena ndani ya chumba changu.
Nikiwa natafakari hapo nikabanwa na haja ndogo, nikawa nimeinuka kwenda bafuni kukojoa, Ile tu natoa uume nikojoe nikaona mabadiliko nikawa nimejiangalia nikakuta Sina korodani ni uume tu, nilishituka sana nikawa na hofu ya ajabu, kesho yake ilibidi nirudi tena singida, nilivyo fika huwezi amini nyumba ya yule mganga sikuikuta na Kila niliye mwuliza alisema huyo Mzee alisha hama siku nyingi , ilibidi nikae sehemu nikihisi labda naota ila ukweli haikuwa ndoto ni ukweli.
Mpaka Leo Sina korodani na siwezi kushiriki tendo, naishi maisha ya huzuni sana na Sioni hata faida ya elimu niliyo nayo Wala mshahara ninao upata, najuta sana maamuzi niliyo yafanya yame geuka msiba wa milele maishani mwangu, Na hakuna ndugu yangu hata mmoja anaye jua hiki kitu nahofia kuwaeleza japo huwa nasikia wakiniongelea kuwa Mimi ni hanisi mana hawanioni nikijihusisha na mambo ya Wanawake.
C&C