Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nikiwa na mdogo ila nikijielewa tulikuwa tunacheza kombolela na wenzangu na mimi ndiye niliyekuwa nazinga.Ghafla wakati wenzangu wamekwenda kujificha nyumba ya jirani yetu kulikuwa na mwembe,basi pale chini ya ule mwembe akatokea kimtu kifupi sana kimevaa gauni la blue mithili ya big mack,ni cha kike kikiwa mguu mmoja na amesuka nyele mabutu mawili,alikuwa ananinyooshea mkono kwa ishara ya kuniita,nilipigwa na bumbuwazi sana na nikatoka nduki balaa kuwafuata wenzangu,nikawaelezea nilichokiona na tuliporudi ili na wao wahakikishe kikapotea,hadi leo nikiwa ni mtu mzima sikupata kitu kibaya chochote
 
Miaka ya 1980 mwisho kuelekea 90 Wilya ya Kasulu na vijiji vyake mambo ya ujambazi na ushirikina yalishamiri sana, nakumbuka wananchi walianzisha kampeni ya kubomoa na kuchoma moto nyumba zilizodhaniwa wenyewe kuwa wahirikina au majambazi, nakumbuka kuna nyumba ya mama mmoja ilipobomolewa kulikuwa na mtungi sebuleni haukuvunjika licha ya kupigwa mawe, mtu mmoja akaenda kuubinua kama anamwaga Maji kulimwagika viungo vya watoto wadogo, vichwa, mikono na miguu! Yule mama alipigwa mawe aise kama sio msaada wa polisi angekufa!

Kisa cha pili miaka ya 90 pale Kasulu kulikuwa na mfanyabiashara Mkubwa majambazi walivamia dukani kwake aise walizunguka mle dukani usiku mzima mpaka asubuhi kulipokucha wakakutwa ndani hawajatoka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujasiri wa kuvuka moto? Kabla ya kuuvuka mliamini ni moto wa aina gani?. Maana ujasiri wa kupambana na moto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh mkuu mbona haya ni maajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha mkuu hizi ni kamba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yeah hyo ni nature kikiundwa kitu ni lazma kirudishwe na wengi huwa wana feli hapo sababu kubwa huwaga ni chuki na zile hasira za kitu alichofanyiwa ila baada ya tukio wengi huwa wanashindwa kurejesha kiumbe husika katka hali ya kawaida kwani kinavyoondoka na kinavyorudi mziki wake unakuwaga mzito na mhusika mkuu anayetakiwa kukirudisha ni ww mwenyewe mhusika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umechanjiwa au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…