Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nikiwa na mdogo ila nikijielewa tulikuwa tunacheza kombolela na wenzangu na mimi ndiye niliyekuwa nazinga.Ghafla wakati wenzangu wamekwenda kujificha nyumba ya jirani yetu kulikuwa na mwembe,basi pale chini ya ule mwembe akatokea kimtu kifupi sana kimevaa gauni la blue mithili ya big mack,ni cha kike kikiwa mguu mmoja na amesuka nyele mabutu mawili,alikuwa ananinyooshea mkono kwa ishara ya kuniita,nilipigwa na bumbuwazi sana na nikatoka nduki balaa kuwafuata wenzangu,nikawaelezea nilichokiona na tuliporudi ili na wao wahakikishe kikapotea,hadi leo nikiwa ni mtu mzima sikupata kitu kibaya chochote
 
Miaka ya 1980 mwisho kuelekea 90 Wilya ya Kasulu na vijiji vyake mambo ya ujambazi na ushirikina yalishamiri sana, nakumbuka wananchi walianzisha kampeni ya kubomoa na kuchoma moto nyumba zilizodhaniwa wenyewe kuwa wahirikina au majambazi, nakumbuka kuna nyumba ya mama mmoja ilipobomolewa kulikuwa na mtungi sebuleni haukuvunjika licha ya kupigwa mawe, mtu mmoja akaenda kuubinua kama anamwaga Maji kulimwagika viungo vya watoto wadogo, vichwa, mikono na miguu! Yule mama alipigwa mawe aise kama sio msaada wa polisi angekufa!

Kisa cha pili miaka ya 90 pale Kasulu kulikuwa na mfanyabiashara Mkubwa majambazi walivamia dukani kwake aise walizunguka mle dukani usiku mzima mpaka asubuhi kulipokucha wakakutwa ndani hawajatoka!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma tunatoka mererani usiku wa manane tuko na pikipiki almaarufu baja tullikutakana na moto mkubwa ukiwa umetanda barabarani kama vile unavuka ,tulikuwa sita tukajishauri sana lakini kwasababu tulikuwa wengi tulipata ujasiri wa kupita ila cha kushangaza tulivuka na hatukuungua wala kuhisi chochote kuangalia nyuma baada ya kuvuka moto uko vile vile
Ujasiri wa kuvuka moto? Kabla ya kuuvuka mliamini ni moto wa aina gani?. Maana ujasiri wa kupambana na moto?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma tunatoka mererani usiku wa manane tuko na pikipiki almaarufu baja tullikutakana na moto mkubwa ukiwa umetanda barabarani kama vile unavuka ,tulikuwa sita tukajishauri sana lakini kwasababu tulikuwa wengi tulipata ujasiri wa kupita ila cha kushangaza tulivuka na hatukuungua wala kuhisi chochote kuangalia nyuma baada ya kuvuka moto uko vile vile
Duuh mkuu mbona haya ni maajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa kingine nilikisikia kilitokea maeneo ya sumbawanga

Kuna mzee wamakamo alikua ni tajiri sana, pesa zake haweki benk na hata akienda kufanya manunuzi hua haweki kwenye wallet kuzistiri zisionekane yeye hua anazishikilia tu kama wanafunzi wanavyoshika vitini vyao mikononi

Siku moja kuna kosi la majambazi lilijipanga kwenda kumvamia

Walimkuta yuko nyumbani kwake ameshikilia pesa akipata upepo kwenye garden yake

Wakamnyooshea bastola na kumwambia atulie kimya kisha atoe kila kitu alichonacho

Yule mzee akachukua zile pesa akazibana kwenye kwapa lake huku akitetemeka kwa woga

majambazi wakamsisitiza kua anyanyue mikono juu, mzee akatii amri kwa kunyanyua mikono juu kisha pesa alizozibana kwapani zikaanguka chini majambazi wakaziokota

Wakamwambia tena "toa kila kitu ulichonacho"

Round hii unaambiwa mzee alichomoa kichwa chake akakishika mkononi halafu kile kichwa kikiwa mkononi kikatoa sauti ikisema "sina chochote jamani nina kichwa tu hapa"
Hahahaha mkuu hizi ni kamba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisimuliwaga ; Kwamba ukienda kwa mganga labda ili kumdhuru mtu ukitaka auwawe na simba/Nyoka etc dawa ya kuunda simba inakua (labda) kama punje za mahindi unawekewa mkononi unasema maneno basi yule kiumbe anatokea akishaenda kumdhuru mlengwa jukumu lako kama muunda Killing machine yule kiumbe akirudi ukuwekee unga mkononi alambe anabadilika anarudi kama zile punje za awali.
wengi wao wanashindwa wanaishia kufa kwa ajili (unaambiwa) kiumbe kinaporudi huko kama ni Simba basi amefura anahasira na madamu mdomoni ,kitu cha kutisha ule ujasiri wa kukaa utulie aje alambe unga unakutoka ukikimbia ndio anakutafuna na wewe, imagine nyoka anavyofoka vile unaanzaje kukaa[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
yeah hyo ni nature kikiundwa kitu ni lazma kirudishwe na wengi huwa wana feli hapo sababu kubwa huwaga ni chuki na zile hasira za kitu alichofanyiwa ila baada ya tukio wengi huwa wanashindwa kurejesha kiumbe husika katka hali ya kawaida kwani kinavyoondoka na kinavyorudi mziki wake unakuwaga mzito na mhusika mkuu anayetakiwa kukirudisha ni ww mwenyewe mhusika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nitaandika vitu vichache tu
_Nimewahi kuwaona usiku wachawi wakicheza ngoma nje ya nyumba niliyopanga
_Nimeona misukule sana,Sana mingine ilikua inaiba mboga usiku,yenyewe inaiba Nyama &Unga wa ugali ama ulaxe kiporo asubuhi hukuti
_Nimewahi kumshuhudia mzee maarufu mtaani kila siku hua anabeba ndoo moja ya Unga pamoja na madumu mawili ya baiskerli anapeleka ktk nyumba moja hivi kila siku saa 12 jioni kumbe anafuga misukule mingi mno,Sasa niliwahi kumfumania ametoka kuwanga saa 11 jioni kachelewa kurudi kwake tukapishana naenda kuoga ametoka nyuma ya mwembe
_Nimewahi kua karibu na mchawi mkongwe kiasi Cha kutaka kununua Misukule
Bei hutofautiana maximum 3,00,0000per kichwa Bei huzid kutokana na nguvu matumizi na nyota ya msukule

_Nimeshakutana na waganga&wachawi wengi njiapanda wakiwa katika shughuli zao usiku mnene
_Nimefanikiwa kujua lugha za kichawi
Mshirika_Mchawi
Kijakazi_Maukule
_Nimefanikiwa kufahamu viongozi kadhaa was kichawi na kupiga nao stori
_Nimefanikiwa pia kurogwa na kutumiwa jini


Sent using Jamii Forums mobile app
Umechanjiwa au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom