steveachi
JF-Expert Member
- Nov 7, 2011
- 10,643
- 12,247
Nikiwa na mdogo ila nikijielewa tulikuwa tunacheza kombolela na wenzangu na mimi ndiye niliyekuwa nazinga.Ghafla wakati wenzangu wamekwenda kujificha nyumba ya jirani yetu kulikuwa na mwembe,basi pale chini ya ule mwembe akatokea kimtu kifupi sana kimevaa gauni la blue mithili ya big mack,ni cha kike kikiwa mguu mmoja na amesuka nyele mabutu mawili,alikuwa ananinyooshea mkono kwa ishara ya kuniita,nilipigwa na bumbuwazi sana na nikatoka nduki balaa kuwafuata wenzangu,nikawaelezea nilichokiona na tuliporudi ili na wao wahakikishe kikapotea,hadi leo nikiwa ni mtu mzima sikupata kitu kibaya chochote