Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Ni rahis sana kuchanganya uongo na ukweli na story ikawa kama ya ukweli.

Huyo jamaa alikung'ata sikio wakat umeelezea alikua na nguvu za kutosha za kuua majambazi na silaha zao. Wew enzi hizo na udogo wako ukapona khaaa...

Ni chai bila mkate tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kijana sio Kila Kitu unataka uelezewe kadri ya uelewa wako...


Chukua Basi/Ndege au Treni nenda Hadi kigoma pale Ujiji ulizia Hilo jina ( Juma Njemba Njemba )... Halafu urudi hapa jukwaani... Ili Sasa ujithibitishie haya yaliyozungumzwa nenda ukaibe ujiji pale posta maeneo ya wakina Suleiman Matola ( Kocha msaidizi wa Simba)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa na mdogo ila nikijielewa tulikuwa tunacheza kombolela na wenzangu na mimi ndiye niliyekuwa nazinga.Ghafla wakati wenzangu wamekwenda kujificha nyumba ya jirani yetu kulikuwa na mwembe,basi pale chini ya ule mwembe akatokea kimtu kifupi sana kimevaa gauni la blue mithili ya big mack,ni cha kike kikiwa mguu mmoja na amesuka nyele mabutu mawili,alikuwa ananinyooshea mkono kwa ishara ya kuniita,nilipigwa na bumbuwazi sana na nikatoka nduki balaa kuwafuata wenzangu,nikawaelezea nilichokiona na tuliporudi ili na wao wahakikishe kikapotea,hadi leo nikiwa ni mtu mzima sikupata kitu kibaya chochote
Mawenge ya utoto tu.
 
Asanteni sana kwa hadithi nzuri nimezisoma zote na hii imekuwa xmass ya pekee kwangu kwamba nasoma hadithi za uchawi karibu siku nzima!
Si haba uchawi upo naamini hilo, ila siishii hapo naamini katika nguvu zinazoshinda kila nguvu; nazo ni nguvu na mamlaka ya Yesu Kristo. Ukiweza kuwa na Yesu hao wachawi watakuogopa na hawataweza kujudhuru kwa namna yoyote. Lakini ukiwa bila Yesu au ukaenda kwa waganga, ndio umejipeleka shimoni mwenyewe. Mbarikiwe
 
Kipindi nasoma lutheran junior seminary morogoro tulikuwa tunatoka kila weekend kwenda vigodoro siku iyo tulienda chakaribu ila watu walikuwa wengi sasa kwenye vigodoro kuna watu wale wanauza vimishikaki na bublish na vimahindi vya kuchoma mmoja wao akamwambia rafiki yangu niliekuwa nae anunue chochote kiukweli hatukuwa na pesa ila yule jama akaforce sana ila ukweli hatuna kitu yule muuzaji sijui alifanya nini ila mkono wa kulia wa rafiki yangu ulipotea hiv hiv nikiwa naona kwa takribani dakika nne tunamuomba jamaa aurudishe ni ukweli hatuna kitu mpaka ukarudi baada ya hapo akatupa muhindi wa kuchoma aiseee sintokaa nisahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mzungu mmoja alikua kakaa sana Afrika(si unajua kasha adapt tabia za kibongo mpaka katuzidi wenyeji),Yuko na kijikampuni chake ametupatia Ajira ya masimango sana.Mtaliano yule alikua ana tabia ya kumtukana kila staff bila kuangalia umri wala cheo.Siku akiamka fresh mnapiga stori..

Kuna mzee ni msafishaji wa bustani.Anajiheshimu sana na watu wote tunamweshimu.Iko siku sikujua walipishana nini kiswahili na Mtaliana.Mzee alitukanwa sana.Matusi yote.

Mzee alishukuru kwa matusi akaondoka.Ila alimwambia nakupa week moja majibu utayapata.

Baada ya week Mzungu akivuka tu geti la kuingilia kazini anapata homa kali sana.Akipelekwa hospital mzima wa afya.Akipelekwa nyumbani mzima wa afya.Kosa ni kugusa maeneo ya kazini....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom