Kama umewahi kutumia hivi vitu, wewe ni legend

Ngoja wahenga waje walete mrejesho mjarabu
 
Na tulio vaa chcchcchc tunaitwaje?
 
Kama uliwahi kutumia stendi ya mabasi ya kwenda mikoani ilipokuwa MNAZI MMOJA hapa Dar yatosha kusema wewe ni LEGEND pia
 
Mkuu umezisahau Chacha Cha tena tulikua tunachagua rangi ya kijani...hiyo Peugeot 505 ndio gari ndogo niliyopata Control nayo sana maana nilijifunzia kuendesha Isuzu injection ilikua tunapaki kwenye ka mlima kwa sababu ya kustua...
 
Dah hii ya nyerere kupigwa mtama tulikua tunajazwa sana upepo
 
Nawaza tu Peni za Bic au Speedo zipo kweli?

Zile juice za Samvita za pakti mnazikumbuka?

Dawa za meno Aha? juzi kati hapo walikuwa wanauza mpaka 50 wale waliweza
Maji ya pakti ya bakhresa
 
Nilisahau Mkuu halafu hapo kwenye Isuzu journey hiyo ilikua new model baada ya ile yenye tairi za mbele zimeingia ndani utasema inadondoka pale mbele ikatapo kona
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hiyo unayosema nishaijua
Hata mm nilikuwa naziogopa kupanda kwenye kona nahisi ni kama zigapindukq
Km wewe legend wa kkoo hiyo ISUZU ilipaki ilikuwa pale mtaa TANDAMTI karibu na msikiti wa idrisa pembezoni mwa OFISI YA STAR TIME miaka ya 2013 lilikuwa bovu lilikaa pale karibu miaka 3 au miwili hivi
Sema zile hazikuwa JOURNEY
zile nhisi zilikuwa modified kama unavyoona hizi TX hapa BODI ya kuchonga
 
Kuna Land Rover zilikua hazina automatic ignition zinaingizwa chuma kama bpedal ya baiskeli kwenye fan ya rejeta inazungusha kwa nguvu ndio ziwake ...ukiwa mzembe zinaeza vunja mkono... Kama kick ya Honda 110 ilikua na tabia hiyo nayo
Hizo LONDO za kupiga ENDEL km Jafongo za mchina toleo la kwanza
 
Kwenye kuchagua shule primary Mtihani starndard 7
Edhi hizo masomo matatu MAARIFA YA JAMII LUGHA na HESABU
Unachagua shule tatu uzipendazo
Forodhani chaguo la kwanza
Kibasira chaguo la pili
Kambangwa kipindi hicho ndo inaanza nikaiweka ya tatu

Asikwambie mtu edhi zetu DAR ES SALAAM nzima shure za SECONDARY ZA hazikuzidi 8
Na wanafunzi tulikuwa wengi balaa
kama kuna mtu humu kasoma JAMUHURI ya edhi hizo nakusalimu sana LEGEND mana ilikuwa shule ya MALEGEND wanasona lkn hawana uhakika kama watafanya paper ya TAIFA ya FORM 4 malegend wa edhi hizo watanielewa

Forodhani ni shule waliosoma BRO zangu nikawa naipenda sana hiyo SHULE
 
Hahahaaa nipo hapo kwenye kuvaa viatu vya Alichoki umenikumbusha mbali sana [emoji23][emoji23][emoji23]. Inshallah mtoto wa pili anakuja soon
Peni ya speedo ndio peni yangu pendwa ilikuwa unanifanya naandika mwandiko mzuri sana .
View attachment 2519123
 
Sikiza LEGEND
kama uliwekewa CHIPSI na tomato ya kwenye CHUPA ya kioo na ukashushia na hii juisi nakusalimu LEGEND
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…