Kama umewahi kutumia hivi vitu, wewe ni legend

Apo kwenye vinywaji umesahau kuweka zile juis sjui ice cream za SANVITA 😁😁
 
Hizo Raba zilikuwa zinaitwa Abeid Mziba kwasababu Mziba alikuwa anazitumia wakati akicheza Yanga. Yes nimezivaa sana shule zilisuluhisha mgogoro na wazazi maanake Raba za kawaida nilikuwa nazichanq mpirani.

Kabla ya hizo raba, DH, Maradona...kulikuwa na "chachacha" na "saa sita utanikoma"...maviatu fulani ya mpira "rubber/plastic" ikifika mchana wa jua kali yanaunguza ile mbaya
 
Kama ulishashuhudia DDC MLIMANI PARK wakipiga pale Magomeni kondoa na Baba ya mziki Juwata Jazz pale Ilala, pls njoo huku lingusenguse tufurahiye maisha!
Sema VIBE la MSONDO lilikuwa linaendeleaga pale ILALA mpk pale TX MOSHI alivyofariki
Ila DDC MLIMANI PARK kondoa waliacha kupiga tangu mwishoni mwa miaka ya 2000 hivi
Juwata sijacheza ila msondo na DDC kama kawa

VIJANA JAZZ kinondoni nimetimba sana edhi hizo TWANAPEPETA inaanza anza mana ndio lilikuwa la kiwanaja cha NYUMBAMI
Kama kuna malegend tulicheza VIBE la VIJANA JAZZ ingawa edhi hizo niilikuwa YOUNG sana nawasalimu sanq
 
Mifuko ya unga kuwa mifuko ya kubebea daftari, hio ipo hadi leo anaebisha agonge like wala hatupewi tuzo
 
Unatumiaje neno EDHI? Una maana ya ENZI? Unatokea mtaa gani?
 
Unatumiaje neno EDHI? Una maana ya ENZI? Unatokea mtaa gani?
Ha ha mkuu ni ENZI
hizo swagwaz tu
Tunakumbushana MACHECKBOB wa zamani
Vipaji vyetu vya Kucheza mpila vilipatikana kwenye UMITASHUMTA
Mkuu umecheza UMITASHUMTA wewe
Edhi ya MCHAKAMCHAKA chinja
Edhi hizo tulikuwa WAZARENDO haswa wa nchi yetu kusoma shule pamoja na watoto wa VIGOGO ilikuwa kawaida sana
Bro wangu mkubwa kapiga TAMBAZA na MTOTO WA MKUU WA MAJESHI EDHI HIZO

natoke MBINGU IFAKARA KILOMBERO nalima ndizi huku mkuu
 
Vijana jazz-masimango,,ngapulila,mwisho wa mwezi,wifi zangu(kida waziri)
 
Kama umepitia vyote hivyo ila kukusoma shule ambaya kwa siku moja mwanafunzi unaagizwa uje na mbolea, fagio, kuni, kopo la kumwagilia bustani, huku umebeba mfuko wa madaftari aina ya rambo na humo ndani kuna madaftari, bakuli, parachichi, muana na uketo(mahindi ya kukaanga) halafu uko peku na shati zima lina kifungo kimoja BASI kasome bado sio ligend
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…