Kama umewahi kutumia hivi vitu, wewe ni legend

Chiblak

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2014
Posts
662
Reaction score
921
Vyombo vya usafiri

1. DCM (Japo siku hizi bado chache zipo)
2. Mabasi ya Leyland
3. Chai maharage hii mnakaa mnatazamana Kama mnacheza draft
4. Peugeot
5. Datsun N.k
Nb: zilikua ndio luxury pindi hizo, nyingine ongeza.

Vyakula
1. Sambusa za ubwabwa ( shuleni)
2. Kachori za chachandu ya machicha ya Nazi
3. Koni za kwenye vikopo vya bati
Nyingine mtaongeza wadau.

Vinywaji
1. Juice ya kutengenezwa kutokana na unga wa kwenye vipakti, siku hz zipo jusi cola lakini hz zilikua noma pakti moja inatolewa ndoo mbili au tatu afu zinawekwa barafu...kumbuka hyo ni sikukuu wakubwa wanapiga soda watoto mnaishi na hzo ndude af mna enjoy sana.
2. Kuna soda flani ilikua ya njano inatengenezwa na kampuni ya coca nadhani jina nimeisahau
3. Chai ya chai jaba Nk.

Mavazi and accessories
1. Suruali za kodrai zikipigwa jua zinawakawaka Kama gold ya geita, sikuuu mnaeza jikuta mtaa mzima mmevaa Aina moja.
2. Magauni ya spesheli.
3. Njumu flani za mpira Kuna wajomba wameenda nazo Hadi shule zipo kama raba flani
4. Mifuko ya sports
5. Viroba vya unga kufanywa mfuko wa kubebea daftari

N.k
Matusi na matukano hasa ya wazazi
1. Nyau kasoro mkia ww
2. Nyambafu
3. Macho kumchuzi ww
4. Shenzi type

Ongezeeni na ya kwenu maana nimekumbuka nimecheka sana
 
Hizo Raba zilikuwa zinaitwa Abeid Mziba kwasababu Mziba alikuwa anazitumia wakati akicheza Yanga. Yes nimezivaa sana shule zilisuluhisha mgogoro na wazazi maanake Raba za kawaida nilikuwa nazichanq mpirani.
 
Hapo kwenye usafiri kam haujaweka LAND ROVER a.k.a LONDO na ISUZU JOUNEY
ujakamilisha list ya usafiri wa gari mapafu ya mbwa anatumia babu mpk mjukuu
images (58).jpeg
images (57).jpeg
 
Aàaah land Rover imetafuta uhuru,land Rover imempiga nduli...kweli land Rover chuma
Kuna Land Rover zilikua hazina automatic ignition zinaingizwa chuma kama bpedal ya baiskeli kwenye fan ya rejeta inazungusha kwa nguvu ndio ziwake ...ukiwa mzembe zinaeza vunja mkono... Kama kick ya Honda 110 ilikua na tabia hiyo nayo
 
Kama umewahi kusoma gazeti liitwalo Mfanyakazi basi inabidi uwe kwako!

Kama uliwahi kuwaona O-level students wa Tambaza hama kwenu haraka.

Kama Uliwahi kusikia shule ya sekondari Forodhani hupaswi kuendelea kumtegemea babako.

Kama uliwahi kunywa juice ya sun vita basi wewe mkongwe.

Kama uliwahi kuhadithiwa kuwa Nyerere aliwahi kupigwa mtama na bodyguard wake basi unapaswa uwe na wajukuu...
 
Inaitwa hendeli
 
[emoji23][emoji23][emoji23] risasi ikapita juu dah [emoji119]
 
Kama ushawahi kula askirim (ice cream) za vijiti uwe una watoto watatu na zaidi

Kama unajua maana ya peremende uwe na wajukuu wawili

Kwa miaka ya 2000 kama ulivaa viatu vya alichoki hakikisha unatakiw uwe na na watoto wawili

Kama ulishawahi kunywa soda inaitwa Fahari unatakiwa uwe na wajukuu sasa

Kama ulishiriki uchaguzi wa kwanza wa Demokrasia jiandae kufa tu ushakula chumvi nyingi hii awamu ya sita na mnakuwa wajuaji sana humu ndani.
 
Kama umewahi kusoma gazeti liitwalo Mfanyakazi basi inabidi uwe kwako!

Kama uliwahi kuwaona O-level students wa Tambaza hama kwenu haraka.

Kama Uliwahi kusikia shule ya sekondari Forodhani hupaswi kuendelea kumtegemea babako.

Kama uliwahi kunywa juice ya sun vita basi wewe mkongwe.

Kama uliwahi kuhadithiwa kuwa Nyerere aliwahi kupigwa mtama na bodyguard wake basi unapaswa uwe na wajukuu...
Tumetoka mbalii🤣🤣🤣
 
Kama ushawahi kula askirim (ice cream) za vijiti uwe una watoto watatu na zaidi

Kama unajua maana ya peremende uwe na wajukuu wawili

Kwa miaka ya 2000 kama ulivaa viatu vya alichoki hakikisha unatakiw uwe na na watoto wawili

Kama ulishawahi kunywa soda inaitwa Fahari unatakiwa uwe na wajukuu sasa

Kama ulishiriki uchaguzi wa kwanza wa Demokrasia jiandae kufa tu ushakula chumvi nyingi hii awamu ya sita na mnakuwa wajuaji sana humu ndani.
Vile vipipi vya gololi vina rangi
 
Back
Top Bottom