Hii imetutokea kwetu baada ya mtoto kwenda kusoma USA mambo ya engineering kaishia kuwa DJ wa maclub.
Leo naona vijana wengi wamemaliza shule na kuwa na ndoto za kusoma vyuo ambavyo wajafika mfano wa mikoani wana ndoto ya kusoma jiji la Dar na wengine mikoa fulani.Tuje kwa hawa watoto wenye ndoto ya kusoma nchi za watu sasa.
Mtoto usipomchunguza kwa makini unaweza kujikuta umepoteza vitu hivi viwili kupoteza ada au kuja natabia zengine. kwenye kupoteza ada hapa wengi ni wale wanaokwenda kusoma china naona wengi wanaishia kuwa wafanyabiashara ni bora kutambua kuliko kupoteza pesa kumbe mtoto unajua anasoma fani fulani kumbe kanogewa na biashara.
Kuja na tabia zengine kitu ambacho mtoto huko alipo uwezi kujua uhuru wake mfano nchi ambazo zenye sera kama itikadi za imani kali, .Mfano kuna mzee mmoja miaka ya nyuma alimpeleka mtoto wake USA kusoma na kipindi cha zamani kulikuwa hakuna whatsapp wala mambo ya kutumiana picha mitandaoni aliporudi kaja na matatuu mwili mzima.
mnaweza kuongeza mengine