Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Huyo kijana anaonekana hajui chochote kinachoendelea nje ya Tanzania achilia mbali SA. Ni kijana anaeonekana hajatoka. Hawa ni wale vijana wa Tunduma pale mpakani ambao wengi wao hupewa story mbili tatu na watu wanaotoka SA, kisha wao huichukua hiyo story na kuwasimulia wenzao kama hivi bila kujua kwamba katika wasimuliwaji kuna wale ambao wanafahamu kindaki ndaki kile wanachosimulia pengine zaidi yao wao. So mtu kama huyo ni wa kumuelewa na kumpuuza tu.
Tunduma watu wamechangamka sana mkuu labda utaje mji mwingine na kumbuka Tunduma watu wanatoka sana aisee..
 
Kila kazi ya maana ilimradi umelizika nayo haya maswala color job na physical hayana maaana kabisa, mbona mwanvita alikuwa sa anafanya kazi voda na alikuwa anavuta kibunda kwani hakuna wsa wanaoweza kufanya?
Hiki ulichoandika hapa, ndicho nilichoandika mimi katika thread huko juu. Sasa akaja kijana asiejua kinachoendelea nje ya Tz na kuanza kunipinga kana kwamba yeye anaijua dunia kuliko watu wengine.
 
Sana aisee siku napanda basi kutoka cape kuja Pretoria ku clear mambo ya passport nilisema Asante Mungu maana mikononi mwa patrol ya police nimenusurika mara tatu
Mikononi mwa gangs mara mbili mbaya Moja haikuwa mbaya sana
Usiku mbaya Woodstock kwa walioko Cape town wanapajua
Pretoria yenyewe amanusura nizichange vibaya aliniokoa jamaa mmoja m colored kwa kunipa info late sana nikala bus kwenda Joz kulala park station three days
Park station penyewe ilibidi nipigane na wamalawi vibaya sana wao wakijua mi mmalawi na watz wanajua mi mrundi basi tafrani kwa kweli kurudi tz nilishukuru na yes lilikuwa tanuru la moto
🤣🤣🤣🤣
 
Hiki ulichoandika hapa, ndicho nilichoandika mimi katika thread huko juu. Sasa akaja kijana asiejua kinachoendelea nje ya Tz na kuanza kunipinga kana kwamba yeye anaijua dunia kuliko watu wengine.
Tatizo watu wanajua sana hata wasivyovijua, Yaani ni kama mtu aliyesoma mpaka ngazi ya degree na bado akashindwa kujua alichosoma
 
Ukiwa bado fresh panda train achana na hizo daladala wanazoziita tax.

Train zimepita location zote muhimu.
Mkuu Dr Matola PhD ushauri unaompa jamaa yetu ni mzuri. Lakini huo wa kuhusu train kwa sasa ni kama haufai. Toka corona ilipoisha ule usafiri wa train umesimama maeneo mengi sana. Mfano train ya kutoka jozi hadi PTA kwa sasa hamna. Hata ile ya kuelekea Tembisa na baadhi ya maeneo ambayo wanaishi wageni wengi hamna.

So cha kufanya hapo akiwa mgeni apande tax, ila asikae mbele. Ni ikiwezekana awe na nauli yake ya kueneo, wakianza tu kuchangishana ampasie mtu wa pembeni yake chap chap kabla hajakabidhiwa yeye mzigo wa hela apeleke mbele. Kuna watu wanatabia. Wakati wa kukusanya kwenye siti, jitu linatoa hela kubwa na kukutupia wewe ndo uzitume mbele. Kisha badala lidai change yake lenyewe, linakotolea macho wewe ulietuma hela mbele ndo upige kelele kuomba change alafu uligee. So kuepusha ujinga huu ni vizuri mtu anawahi yeye kuwapokeza wa pembeni yake wazitume mbele. Hasa ukiwa new comer ndo kabisa watakuzingua ile kinoma noma cause wanajua utashindwa kujitetea.
 
Hivi mkuu kuna kitu kuhusu passport huwa sijapata majibu kabisa... mtu mwenye passport ya nchi nyingine anawezaje kuitumia kama alishawahi kuwa na passport ya TZ? finger prints si zitaleta shida wakati wa kuvuka?
Ninachofahamu mimi ukiwa na passport ya nchi nyingine alaf ukatumia details zile zile ulizotumia kwa passport ya mwanzo itakuwa rahisi mno kukukamata. Ila huyu mwana aliechukua kitabu cha Malawi aliondoka bongo kitambo kabla hatujaingia kwenye SADC, alaf kipindi kile passport nyingi hazikuwa kwenye system hivyo kuwa rahisi mtu kumiliki passport mpaka 2 au 3 za nchi tofauti.
 
Ninachofahamu mimi ukiwa na passport ya nchi nyingine alaf ukatumia details zile zile ulizotumia kwa passport ya mwanzo itakuwa rahisi mno kukukamata. Ila huyu mwana aliechukua kitabu cha Malawi aliondoka bongo kitambo kabla hatujaingia kwenye SADC, alaf kipindi kile passport nyingi hazikuwa kwenye system hivyo kuwa rahisi mtu kumiliki passport mpaka 2 au 3 za nchi tofauti.
Enzi za kitabu cha kijani?
 
2001 mbali sana. Miaka 23 iliyopita.
Mwaka 2012 akaenda katika ofisi za uhamiaji ya Malawi, akajifanya yeye Mmalawi na kupewa passport kama kawa 🤣🤣🤣. Naweza kusema kuwa kwa dunia ya leo ukiijua lugha ya nchi fulani kwa ufasaha, na kukariri vijijini fulan vya nchi husika.

Basi uwezekano wa kukubaliwa kuwa wewe ni raia wa nchi husika ni mkubwa sana. Popote pale.
 
Back
Top Bottom