Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
- Thread starter
- #301
Haujui ulisemalo mkuu.Mimi nikimbilia mbele abiria wakinipa nauli naziacha sizipokei.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haujui ulisemalo mkuu.Mimi nikimbilia mbele abiria wakinipa nauli naziacha sizipokei.
South africa
South africa lazima nijeee tu...
Ni kweli mkuu, kuna maeneo mengine ni hatari kwa train, haswa Capetown waxhosa wanakukaba mchana kweupee na watu wanaona 🤣🤣🤣Train sawa, lkn kuna route za location nyingine ni hatari, ile route ya Philip to Kyalitsha huko wee kukabwa nnjennje, route ya usalama zaidi niya Wyneburg, Bellville to Strand na ile ya Miuzngburg, na kuna hii inayo pita Levi's town to UniBell nayo ipo kimya mchana nayo ni hataree
Karibu South bingwaSouth africa
South africa lazima nijeee tu...
Sijakuelewa mkuu
Mtu kadakwa huko ndio oda hyo anarudishwa nyumbani jana tuSijakuelewa mkuu
Foreigner kuishi location ni uzembe uliopitiliza.Ni kweli mkuu, kuna maeneo mengine ni hatari kwa train, haswa Capetown waxhosa wanakukaba mchana kweupee na watu wanaona 🤣🤣🤣
Utaelewa tu, kaburu kaamuwa kunyosha rula.Sijakuelewa mkuu
Kweli mkuu. Maisha hayo ya kujitupa location washakuwa nayo wamalawi. Baadhi ya ndugu zetu wameshashtuka.Foreigner kuishi location ni uzembe uliopitiliza.
Ni bora mkashare nyumba watu kadhaa mnachanga kodi mnamlipa mwenye mjengo au home finder kuliko kukaa location Langa, Gugu letu na Khayelitsha kwa sababu bei ya nyumba ni kitonga wakati risk ni kubwa sana, watu smart kichwani hawafanyi ujinga huo, bora hata ujichanganye na Warangi woodstock na advantage ya wood stock unakwenda town kwa mguu tu upandi treni wala tax.
Kikubwa kama upo na watu waelewa mna mishe zenu kipato cha uhakika hata wanne mnachukuwa appartment moja mnashare kodi tena sea point kabisa au Camps bay unadinda na wapopo.Kweli mkuu. Maisha hayo ya kujitupa location washakuwa nayo wamalawi. Baadhi ya ndugu zetu wameshashtuka.
Ukishindwa kulipa kodi hata kwa Waislamu Athlone basi bora urudi Bongo tu kiwanja hukiwezi.Kweli mkuu. Maisha hayo ya kujitupa location washakuwa nayo wamalawi. Baadhi ya ndugu zetu wameshashtuka.
Huku kupata work permit mwa mtu mwenye documents tokea home kuna wepesi?? Mfano natoka sahivi naenda nina passport na balance mfukoni hata ya kunikimu kwa miezi 6 au zaidi....karatasi za shule pia zipoo, ukifika kule hizo permits na nini kuna uzito kiasi gani mbaka ukae sawa maybe??🧑🦯➡️Kikubwa kama upo na watu waelewa mna mishe zenu kipato cha uhakika hata wanne mnachukuwa appartment moja mnashare kodi tena sea point kabisa au Camps bay unadinda na wapopo.
Botswana life ngumu sana sasa hivi na wao wanakimbia.Hivi bado kuna watu wanaujinga wa kwenda South Africa kutafuta maisha? Si Bora uende Botswana
Namba 5.Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.
Nianze kwa kusema kuwa dunia ina mengi, na kamwe hauwezi kuyajua kama haujaambiwa au kuyaona. Ndio maana waswahili wanamsemo wao unaosema "tembea uyaone". Hii haimaanishi kwamba utembee uyaone magorofa, magari au barabara, bali uone mambo mapya ambayo hapo kabla ya kutembea ulikuwa haujawahi kuyaona au kuyasikia popote.
Sasa leo ningependa nije na mada inayowatahadharisha ndugu zangu wabongo, ili kuwafungua macho na akili ya kujua yale ambayo hapo kabla walikuwa hawajayajua kuhusu South Africa, Dzonga, Afrika borwa, Afrika kusini, bondeni, Kaburu na kila jina linalotambulisha taifa hili.
Ni mambo sita tu ambayo ningependa kukutahadharisha nayo, uyazingatie kabla ya safari. Ila kama kuna mengine ya kuongezea basi wenzangu ambao wako humu pia wataongezea mengine katika comment. Na uzi wangu wa leo unajikita katika mambo yaliopo ndani ya mipaka ya South tu. Kuhusu changamoto zingine za njiani kabla ya kufika South nk, hizo sintozizungumzia kwa sasa. Maana thread za changamoto hizo zipo nyingi na mimi nishawahi kuandika moja.
Tuendelee hapo chini na yale unayotakiwa kuzingatia.
1. Hakikisha una document zote muhimu zinazohitajika safarini. Na kama uliambiwa kuwa gharama ya safari ni laki tatu, basi uandae angalau laki nne, ili moja uiweke pembeni itakusadia mbele ya safari. Kumbuka kuna dharura njiani, dola au rand kupanda nk.
2. Wakati unapanga safari, jitahidi kwanza ujue kingereza. Na kama una kichwa kizito cha kujifunza ngeli, basi upambane ujue hata salam, kuomba kitu au kuaga. South ni nchi inayoongea lugha 11. Ambapo lugha 9 ni za wenyeji na 2 za wazungu. Lakini lugha ya taifa na ambayo inapewa kipaumbele zaidi ni English.
Sasa ukijua English, hata kama hauna elimu ya maaana, uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa ukilinganisha na wale ambao hawajui English. Ndomaana wazimbabwe wamedhibiti kazi nyingi na haswa zinazomilikiwa na wazungu, maana wao English kwao ni kama maji na mtungi, halafu wanaongea British safi kuliko waafrika wengine. Kutokujua English kumewanyima watu wengi (haswa kutoka bongo) fursa za kazi, hivyo kusababisha wengine kuamua kufanya deal hatari, halali na zisizo halali ili mradi mtu aishi.
3. Kabla ya kuanza safari hakikisha una address au contacts za wenyeji wako zaidi ya mmoja. Nchi hii kuna watu wengi wameuwawa, wameibiwa, wamekamatwa na kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kukimbiwa au kuzimiwa simu na wenyeji wao kabla ya kuingia au baada ya kuingia South. Na hii sio kwa wabongo tu, bali ni nchi zote za East Africa watu wana tabia za kuwaingiza maboya ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba waje tu watawapokea na kuwafanyia mpango wa kuishi, lakini ndugu, jamaa au marafiki hao wanapoingia tu mwenyeji huzima simu, hubadili namba nk. Hivyo ukiwa na address au namba za sim zaidi ya 3, itakusaidia ku deal na mwingine baada ya mmoja au wawili wa mwanzo kukuzimia simu.
4. Usiwaze kwamba utafanya kazi fulani tu, bali wewe ujiandae kufanya kazi yoyote (ya halali) kujiingizia kipato. Hili swala la watu kuja huku wakiandaa akili, na saikolojia zao za kichwa kwamba anakuja kufanya kazi fulani tu. Ndio limesababisha baadhi ya wabongo kupoteza mwelekeo wa maisha, na kujikuta wanajitupa katika biashara hatari na zisizokuwa halali.
5. Usilete usela mavi usiokuwa na maana. Vijana wengi waliotaka kuleta usela wa Mbagala, Mburahati, Manzese, Temeke, Tandika nk tumewazika wakiwa bado wadogo. Hii ni kwa sababu huku watu hawana muda wa kukimbizana na mwizi wajichoshe. Ukileta usela mavi, watu wanakutafutia target, wanafumua ubongo, kazi imekwisha. yumbani watu wanarudisha nguo au maiti na kesi hamna. Pia usije kwa lengo la kutafuta na kufanya starehe kupitiliza mpaka ukasahau kilichokuleta. Maana kama starehe hata bongo zipo na umeziacha, kama mademu bongo wapo na umewaacha, kama tungi pia bongo lipo umeliacha. So focus kwa kile kilichokufanya utafute nauli uje. Sio kuendekeza kulewa na chupi za Kaburu utapotea mazima na hakuna mtu atakaekurudisha katika chanel yako tena.
6. Ukifika hapa kama wewe ni mpya usikimbilie kukaa kiti cha mbele katika daladala (tax), hata kama imejaa na imebaki siti moja ya mbele, ni bora usubiri nyingine alafu ndio upande. Hii ni kwa sababu huku majimbo mengi daladala zao hakuna kondakta anaezunguka ndani ya daladala kuomba nauli. So ukisema unakimbilia mbele kukaa na dereva, utashangaa watu wanakusanya hela zote huko nyuma, alaf wanakutupia wewe ndio uhesabu na kama kuna mtu ametoa hela kubwa umrudishie chenji, na ikiwa pungufu uhakikishe waliokupa wanazieneza. Dereva yeye hupokea nauli ambayo imeshahesabiwa tayari na iwe imetimia. Ikipungua hata sh hamsini basi ataanza na wewe uliepokea hela kabla ya kuendelea na waliopo ndani ya gari. Pia asilimia kubwa ya madereva wa hapa wana silaha mbali mbali ndani ya gari zao, kama sio bunduki basi fimbo inayofanana na mkia wa taa. So hela yake isipoenea na wewe ndo New comer (mpya) haujui lugha, basi imekula kwako. Hata ujitetee kwa English yako ya kuunga unga hatokuelewa. Naomba niishie hapa.
Yah mnakaa wanne au watano, kila mtu anapiga mishe zake mnakutana usiku tu if it's necessary.Kikubwa kama upo na watu waelewa mna mishe zenu kipato cha uhakika hata wanne mnachukuwa appartment moja mnashare kodi tena sea point kabisa au Camps bay unadinda na wapopo.
Naam kama ukishindwa kulipa kodi ndogo tu ya mwezi inamaana wewe hauna maana ya kuendelea kuishi katika nchi dume kama hii. Bora urudi bongo mapema ukawe bodaboda tu.Ukishindwa kulipa kodi hata kwa Waislamu Athlone basi bora urudi Bongo tu kiwanja hukiwezi.
Ninachofahamu mimi viza ya work permit unaipata ubalozini. Hapa ni zile viza za kuingia na kutoka (visitor).Huku kupata work permit mwa mtu mwenye documents tokea home kuna wepesi?? Mfano natoka sahivi naenda nina passport na balance mfukoni hata ya kunikimu kwa miezi 6 au zaidi....karatasi za shule pia zipoo, ukifika kule hizo permits na nini kuna uzito kiasi gani mbaka ukae sawa maybe??🧑🦯➡️
Kweli mkuu, hali imekuwa ngumu kila sehemu. Wewe ukitoka South na kukimbilia Botswana, wenzako wanatoka Botswana na kukimbilia South.Botswana life ngumu sana sasa hivi na wao wanakimbia.