Hivi kwani siku hizi majukumu ya mwanamke kwenye ndoa hayaonekani au
Yani wewe mke akupikie, akufulie, akulee, akuzalie na akulelee watoto wako, akupe unyumba na vingine vingi halafu bado uone hastahili mali zako sasa unataka umpe kitu gani
Hizo mahari mnazotoa anachukua mke au wanachukua wazazi/walezi wake na umeshajiuliza ni kwanini kwenye jamii zetu mwanamke anatolewa mahari
Yani ukitoa huduma ya kiuchumi kuna kipi kingine mwanaume anachoweza kumpa mwanamke, maana mkae mkijua hizi kampeni zenu za kataa ndoa kisa kukimbia majukumu yenu hamuwakomoi wanawake, bali mnazidi kufanya wanawake wasione umuhimu wenu na hili limeshaanza hivi sasa kwa baadhi ya wanawake
Hayo mapungufu ya kibinadamu kwenye ndoa huwa yapo tu, hata wanaume mna mapungufu yenu ila ni vile ya kwenu mnayaona madogo hivyo mnalazimisha yavumiliwe, ila ya wanawake mnayaona makubwa hivyo mnaona hawastahili kuvumiliwa