Wala hatumnyooshi mkuu yeye mwenyewe ndio amekuja kuelewa uzeeni kwanini tunafanya hivyo na anajutia, na wala si kwamba eti mama yetu ndio alitulisha sumu bali sisi watoto tulikuwa tunajionea wenyewe kwamba baba anatafuta na ndiye anayetuhudumia lakini hakuwa na muda na sisi na mara nyingi alikuwa anachelewa bila sababu, kwahiyo kilichobaki na sisi tunamtumia tu pesa kama alivyokuwa anafanya yeye
Lakini hakuna ile bond kati ya baba na watoto, kwamba tunaweza kuenda kumtembelea mara kwa mara na kukaa naye kuongea naye, na hatuwezi kujilazimisha sababu yeye ndiye alishindwa kuitengeneza hiyo bond
Ndio maana nasema wanaume jifunzeni kutenga muda mwingi wa kukaa na wake zenu na watoto wenu hao ndio mtabaki nao hadi uzeeni, hiyo michepuko mnayoihonga leo au hao washikaji mnaokesha nao baa leo wala hawatakuwepo na ninyi uzeeni, yani mtu unataka ujanani ule raha na wengine kisha uzeeni uje uwape shida wengine halafu uanze kumtupia lawama mkeo kuwa kawalisha sumu watoto bila kujua kwamba hao watoto nao wana akili na mambo mengine wanajionea
Sent from my S6 using
JamiiForums mobile app