Msimtenge baba, kuna mengi sana huenda hamyajui kati yenu, mama na baba yenu na hasa kati ya baba na mama yenu.
Sipendi sana kuandika personal issues ila nilipomuuguza baba yangu nilijifunza mengi, mengi sana. Mwanzo nilikuwa na notion ya baba kuwa kikwazo katika mambo mengi, ila alipokuwa karibu na mimi kwa zaidi ya miaka mitatu, nilijifunza mengi, hatukuwahi kukaa na kuongea kuhusu mama au maisha yao(baba yangu hakuwa talkative), ila kupitia hisia zangu nilijifunza mengi.
Msijiingize katika jambo lolote linalohusu wazazi, msiwabague wala kuwatenga. Ndoa ni jambo jema sana, ni taasisi kubwa inayoleta taifa imara, ila ina changamoto mob sana.