Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Na kukuthibitishia ninacho kuambia kuna biashara nimeamua kutuma M7 Kati ya hizo M7; 1.3M ni tiketi ya ndege; 500k kula na kulala lakini Faida yake ambayo iko projected ni 6M. Nitaleta ushuhuda suni



Elezea

Umetuma hela umekaa unasubiri faida safi sana
 
Hivi kama mtu unatokea Dodoma na ninataka kwenda mnadani huko Kondoa (usingidani) kwa siku moja na kurudi Dom siku hiyo hiyo? Ninataka kwenda kuona tu kwanza.
 
@Jebel @raymage

Hapana ndugu MtanzaniaOG minadani wanaenda asubuhi sana kwani baadhi ya vijiji viko mbali kutoka Kondoa mjini. Ni vema uka plan kwenda na kulala siku moja, gharama ya Kondoa ni nafuu sana. Guest+Msosi budget haizidi 6500/=. Goodluck
 
Ni kwa nini huo uzito wa nyama haupatikani wewe muuzaji ukiwepo ili kujiridhisha kuwa ndiyo wenyewe?
Hapa ndo kuna ufanyaji biashara kijima. Mengine mdau nakushukuru sana
 
Mkuu upo sahihi. Hili wazo lako ndo linatoa suluhisho la kudumu. Hata mimi naona ili ufaidike na hii kitu bora kufuga seriously kisasa. Pia hao mabepari wakikuelewa kwamba uko njema hawatakushikia chini kama hawa wachuuzi wengine na wanaweza kuwa wanakufuata wenyewe shambani.
 
Hapana ndugu MtanzaniaOG minadani wanaenda asubuhi sana kwani baadhi ya vijiji viko mbali kutoka Kondoa mjini. Ni vema uka plan kwenda na kulala siku moja, gharama ya Kondoa ni nafuu sana. Guest+Msosi budget haizidi 6500/=. Goodluck
Shukrani mkuu
 

Ndugu hakuna mtu anayetamani kuwa mchuuzi, na hawa unaowaita wachuuzi hii ni hatua mojawapo kuelekea hatua nyingine. Sote hatuwezi kuanza na hatua ya kufuga kisasa. Mtu anayefanya uchuuzi huu inabidi umtie moyo na kumshauri kama una mawazo ya kumaogeza mbele huu ni “Ubuntu”.

Nitakupa mfano, Mimi nimeanza na huu unaouita uchuuzi ila kutokana na uchuuzi huu nimejifunza mengi na hadi sasa natarajia kufungua ranch yangu ambayo nitaiendesha kisasa zaidi, nimeshanunua mashamba kibaha na kutia uzio, kujenga mabanda n.k. Nikirejea nchini itakuwa ni actualization tu.

Nashauri Watanzania tushauriane, kupeane maarifa sahihi, tusaidiane huu ndo Utanzania. Tusikatishane tamaa kwani kwa kufanya hivi hatuwezi kufika mbali.
 
Jomba mbona unapaniki? Hapo nimekatisha tamaa kivipi? Umeandika waraka mrefu pumba tupu kwasababu ya kupaniki. Soma vizuri uelewe nilichoandika acha kukurupuka. Mtu kuwa mchuuzi sio tusi wala kashfa. Ni kazi kama kazi zingine. Au wewe ndo wale wanaodhani kuitwa mkulima ni kudharaulika? .... Relax bro...
 
Jamaa umetoa connection ya ukweli
 
HONGERA SANA NA UMENIFUNGUA KWA KWELI KWENYE BIASHARA YAANI KUMBE TUNAKAA TU KUNA BIASHARA ZINGINE KAMA HIZI
 
Kuna mtu ameshaanza kufanya hii tuungane..?
Mimi hapa...Niko nimeanza

Naomba na wengine wasome hapa kama hawatojali..kwa sasa mbuzi wako juu sana,ni high season wakulima wana pesa za mbaazi na dengu wanaringa hawauzii njaa..mbuzi mpk 150k kwa mbuzi mmoja na kondoo pia bei ndo ziko hvyoo....Mimi nilikua na kiasi nkaongezewa ila mpk mda huu nazunguka minadani bado sijafanya kutafura unafuu maana hakuna mbuzi wa 50k may be vile vidogo Sanaa..

Wanaofanya kwa sasa ni wazoefu tu wa business wanalinda mitaji yao na wao kwa kua wengi wanajua biashara at least wanapata faida japo kidogo sana na advantage kubwa wao huku wengi wana mini yao hvyo hawagharamii malazi plus msosi...kwa mgeni kama sisi ukiingia kichwa kichwa itakula kwako uanze laumu watu...Mimi toka Alhamis nazunguka na pesa yangu naogopa nisije nkachoma bure na kutafuta mchawi..
Msimu mzuri wa kuanza hii biashara kwa huku Kondoa ni December may be utafute chimbo lingine ila kwa huku nimeogopa..December to April mbuzi mkubwa kabisaa unampata mpk elf 60 ambae kwa sasa wanauzwa laki na 50!!!
Kaka jebel alieleza vzr kule juu namimi nakazia umakini msiseme hamjaambiwa!!
Ahsanteni

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Ahsante sana ndugu, Mungu akubariki kwa kutupa uhalisia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…