zipalapwata
JF-Expert Member
- Oct 19, 2016
- 290
- 156
Uzi mzuri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na kukuthibitishia ninacho kuambia kuna biashara nimeamua kutuma M7 Kati ya hizo M7; 1.3M ni tiketi ya ndege; 500k kula na kulala lakini Faida yake ambayo iko projected ni 6M. Nitaleta ushuhuda suni
Elezea
@Jebel @raymageHivi kama mtu unatokea Dodoma na ninataka kwenda mnadani huko Kondoa (usingidani) kwa siku moja na kurudi Dom siku hiyo hiyo? Ninataka kwenda kuona tu kwanza.
@Jebel @raymage
Hapa ndo kuna ufanyaji biashara kijima. Mengine mdau nakushukuru sanaNi kwa nini huo uzito wa nyama haupatikani wewe muuzaji ukiwepo ili kujiridhisha kuwa ndiyo wenyewe?
Mkuu upo sahihi. Hili wazo lako ndo linatoa suluhisho la kudumu. Hata mimi naona ili ufaidike na hii kitu bora kufuga seriously kisasa. Pia hao mabepari wakikuelewa kwamba uko njema hawatakushikia chini kama hawa wachuuzi wengine na wanaweza kuwa wanakufuata wenyewe shambani.Nilienda Soga kiwandani kwa kweli wale watu wamejipanga and they mean business. Ila kuna new strategy ambayo wamekuja nayo kwamba wameanzisha centres huko huko za kununua, hivyo ile adha ya kusafirisha wamempunguzia supplier ila hapa naona hapa kutakuwa na changamoto kwasababu wenyeji wakishalijua hili soko hawatahitaji kutuuzia tena sisi watu wa kati ambao tutaenda kuuza kiwandani. Hapo ndipo linalokuja lile wazo langu la kuanzisha shamba la ufugaji, hamna namna nyingine.
Shukrani mkuuHapana ndugu MtanzaniaOG minadani wanaenda asubuhi sana kwani baadhi ya vijiji viko mbali kutoka Kondoa mjini. Ni vema uka plan kwenda na kulala siku moja, gharama ya Kondoa ni nafuu sana. Guest+Msosi budget haizidi 6500/=. Goodluck
Mkuu upo sahihi. Hili wazo lako ndo linatoa suluhisho la kudumu. Hata mimi naona ili ufaidike na hii kitu bora kufuga seriously kisasa. Pia hao mabepari wakikuelewa kwamba uko njema hawatakushikia chini kama hawa wachuuzi wengine na wanaweza kuwa wanakufuata wenyewe shambani.
Jomba mbona unapaniki? Hapo nimekatisha tamaa kivipi? Umeandika waraka mrefu pumba tupu kwasababu ya kupaniki. Soma vizuri uelewe nilichoandika acha kukurupuka. Mtu kuwa mchuuzi sio tusi wala kashfa. Ni kazi kama kazi zingine. Au wewe ndo wale wanaodhani kuitwa mkulima ni kudharaulika? .... Relax bro...Ndugu hakuna mtu anayetamani kuwa mchuuzi, na hawa unaowaita wachuuzi hii ni hatua mojawapo kuelekea hatua nyingine. Sote hatuwezi kuanza na hatua ya kufuga kisasa. Mtu anayefanya uchuuzi huu inabidi umtie moyo na kumshauri kama una mawazo ya kumaogeza mbele huu ni “Ubuntu”.
Nitakupa mfano, Mimi nimeanza na huu unaouita uchuuzi ila kutokana na uchuuzi huu nimejifunza mengi na hadi sasa natarajia kufungua ranch yangu ambayo nitaiendesha kisasa zaidi, nimeshanunua mashamba kibaha na kutia uzio, kujenga mabanda n.k. Nikirejea nchini itakuwa ni actualization tu.
Nashauri Watanzania tushauriane, kupeane maarifa sahihi, tusaidiane huu ndo Utanzania. Tusikatishane tamaa kwani kwa kufanya hivi hatuwezi kufika mbali.
Jamaa umetoa connection ya ukweliHabarini Waungwana!
Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.
Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.
BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.
A. Upatikanaji wake
Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.
Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.
B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.
C. Bei ya mbuzi
Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.
D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.
E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.
F. Changamoto zake
Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
- Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
- Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
- Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
- Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
G. Malipo
Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?
Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.
ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.
Mimi hapa...Niko nimeanzaKuna mtu ameshaanza kufanya hii tuungane..?
Ahsante sana ndugu, Mungu akubariki kwa kutupa uhalisiaMimi hapa...Niko nimeanza
Naomba na wengine wasome hapa kama hawatojali..kwa sasa mbuzi wako juu sana,ni high season wakulima wana pesa za mbaazi na dengu wanaringa hawauzii njaa..mbuzi mpk 150k kwa mbuzi mmoja na kondoo pia bei ndo ziko hvyoo....Mimi nilikua na kiasi nkaongezewa ila mpk mda huu nazunguka minadani bado sijafanya kutafura unafuu maana hakuna mbuzi wa 50k may be vile vidogo Sanaa..
Wanaofanya kwa sasa ni wazoefu tu wa business wanalinda mitaji yao na wao kwa kua wengi wanajua biashara at least wanapata faida japo kidogo sana na advantage kubwa wao huku wengi wana mini yao hvyo hawagharamii malazi plus msosi...kwa mgeni kama sisi ukiingia kichwa kichwa itakula kwako uanze laumu watu...Mimi toka Alhamis nazunguka na pesa yangu naogopa nisije nkachoma bure na kutafuta mchawi..
Msimu mzuri wa kuanza hii biashara kwa huku Kondoa ni December may be utafute chimbo lingine ila kwa huku nimeogopa..December to April mbuzi mkubwa kabisaa unampata mpk elf 60 ambae kwa sasa wanauzwa laki na 50!!!
Kaka jebel alieleza vzr kule juu namimi nakazia umakini msiseme hamjaambiwa!!
Ahsanteni
Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app