Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Idea nzuri lakini inahtaji uwe fighter sana. Vimichakato vyake usiwe mtoto wa mama. Kuna watoto wa mama hata mbuzi wanaogopa kushika

Umenikumbisha miaka fulani huko tumefika gairo kununua kuku vijijini Dogo wa kimara akawa kuku akikimbia tunasema mkimbize au chukua huyo kuku umfunge miguu anasema hawa hawang’ati kweli mbona wakali mwanaume huyo
 
Umenikumbisha miaka fulani huko tumefika gairo kununua kuku vijijini Dogo wa kimara akawa kuku akikimbia tunasema mkimbize au chukua huyo kuku umfunge miguu anasema hawa hawang’ati kweli mbona wakali mwanaume huyo
Hawa watu wamjini wanaitwa mmea wa viazi mchipsi wakimaanisha viazi vinautwa mchipis
 
Wazo zuri sana, ahsante mkuu.
Ila hapo kwenye viwanda kuchinja na kuwataarifu kg (uzito wa mifugo yenu) ndio wanapotengeneza super profit.

Ni kama mabenki wanapopeleka pesa BoT, hua wanapewa taarifa tu kwamba zimepungua kadhaa, wanakatwa huko huko juu kwa juu na hauwezi kuthibitisha kwa vile unakua haupo eneo la tukio wakati wa kuhesabu.
Najaribu kuwaza wakichukua kg moja moja tu kwa kila mbuzi, wanapata pesa nzuri tu.

Lakini mtu akiamua kuweka mfumo imara wa ujusanyaji huko vijijini kwa uhakika wa hiki soko, anaweza asiajiriwe na akapiga pesa ndefu tu.

mrangi pitia huku!
 
Unaweza ukahisi umeandika kwa kupoteza muda ila ukweli ni kuwa kuna watu tayari umewapa wazo zuri sana la biashara na soon wataanza kulifanyia kazi. Hongera sana mkuu kwa hili wazo una roho ya kitajiri na utafanikiwa sana maishani mwako.
Mkuu yuko vizuri ana roho ya kitajiri,

Naamini kuna mtu anafanikiwa kwa kupitia uzi huu.

Ikipendeza yeyote anayefanikiwa kupitia mawazo ya watu kama hawa walete mrejesho ikiwezekana kutoa hata shukrani tu inatosha sana, Mwisho wa siku tuzo ya heshima itolewe.
 
Soko la kondoo lenyewe likojee boss wangu..
 
Nje ya mada kidogo. Pamoja na kulipa ushuru huu wote, ukipata kafaida ka eg sh laki moja na ukaamua kumtumia mama yako mgonjwa kijijini akatibiwe, basi unatakiwa kilipa tena tozo ya muamula! Na mama yako anapokwenda kutoa fedha nako analipa! Na akienda hospital nako anakwenda kulipa! Kweli kweli inabidi wananchi tuamke sasa tukiwashe kwa sababu hakuna mtawala atakaye tuonea huruma. Wao wako busy kutumbua hizi fedha wanazokata kwa maskini.
 
[emoji3516]
MKUU,
NIMEFURAHISHWA NA UKARIMU WAKO NA KUWA WEWE SI MCHOYO WA TAARIFA.

MIMI NAOMBA UNIPE MWONGOZO WA NAMNA ULIVYOPATA AJIRA NJE YA NCHI,
NA NI NCHI GANI.
 
Hongera mkuu kwa wazo zuri la biashara.


Niliwahi kufanya biashara inayofanana na hii ya mbuzi
Nilikuwa nanunua nguruwe wilaya ya Chato napeleka Mwanza ( uwanja wa fisi )
Ilikua biashara nzuri na changamoto ni kama zinafanana
Nilipata changamoto zaidi kwenye usafiri na ukusanyaji wa nguruwe lakini soko lilikuwa la uhakika na faida haikosekani.

Umenikumbusha mbali sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…