Kama una mtaji usiweke kwenye biashara ya Frame/maduka, fanya hivi

Kama una mtaji usiweke kwenye biashara ya Frame/maduka, fanya hivi

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
2,317
Reaction score
7,808
Biashara ya kuweka kwenye maduka imekaa kitapeli sana, unakuta umebahatika kupata mtaji wa million tano ukisema utafute Frame, unapita zaidi ya laki mbili, Frame yenyewe ukishaifungua utakutana na maafisa njaa kali wa halmashauri na TRA na wengine kibao ili ufunge ufurisike,

Jikite kwenye ujuzi brother tafuta niche unayoipenda ya ufundi then jua ndani nje, namaanisha jua mpaka uhakikishe hakuna mtu mwingine anayejua zaidi yako, then ukimaliza hiyo hela yako ndogo uliyonayo, ndio iwe kama toools au starting point.

Nimesema haya kwasababu nimemkuta kijana fundi simu anaingiza 60,000-100,000/= kwa siku, nimeshangaa kwasabu nimemkuta na microscope, TV kubwa, pamoja na vifaa basi mteja akifika pale anaifanyia diagnosis kwa kutumia microscope n.k watu wamemuamini sana na kazi zimemzidia, katika kushare story yake alianza kwanza kutafuta ujuzi then akainvest kununua spare za simu kwahiyo anauza spare na kuzibadilisha...

Mwingine ni fundi umeme wa magari, hapa nisiongee sana, ni darasa la saba tu lakini pia kufungua duka la spare za magari na bado ni fundi.

Mwingine ni fundi wa kuchomelea na aluminium kajiset barabarani, yupo na work shop nilishangaa anatengeneza vifaa vya chuma vyote unavyovijua wewe ,kuanzia jembe, toroli, pilau za tractor n.k

You see? Find niche then wekeza muda wako woote, jifunze tafuta source mbali mbali mtandaoni kuwa guru katika eneo moja.

Huo ndio ukombozi kwa vijana.
 
Kweli mkuu kuna kipindi niliacha chuo pale udom ile pesa ya boom nikaenda veta kusoma graphics design na sasa nainjoi kiufupi nimeamini Mungu anaweza kukufanyia miuujiza..
Katika watu walio fanyiwa miujiza mimi nambari.moja jamani..

Nimefanyiwa maajabu
Hii ni maajabu kweli Mungu anashangaza
 
Kweli mkuu kuna kipindi niliacha chuo pale udom ile pesa ya boom nikaenda veta kusoma graphics design na sasa nainjoi kiufupi nimeamini Mungu anaweza kukufanyia miuujiza..
Katika watu walio fanyiwa miujiza mimi nambari.moja jamani..

Nimefanyiwa maajabu
Hii ni maajabu kweli Mungu anashangaza
Smart brain, rudi chuo hahaha

Ninachofikiri mimi elimu yetu inamuandaa kijana kufanya vitu vikubwa pasipo kumpa msingi mzuri, mfano mtu anasoma cybersecurity always utategemea kampuni ili kufanya kazi bila hizo kampuni, huna kazi za kufanya , the same na data science or whatever but graphics design, ukichanganya na motion graphics, 3d n.k kazi zinahitajika na wengi so kila mmoja na chaguo lake
 
Fani ndio kila kitu
Ujeuri na kiburi nilivyowahi kufanya ni kwasababu ya fani.

Naam unafukuzwa kazi lakini unatafutwa urudi Kwa kubembelezwa.

Kisha unawapa masharti yako na wanatii.

Watu wengi wanaumia kwakuwa wanachofanya kinafanywa na wengi

Bro,CV ya kwenye makaratasi ni kibali kinachokupitisha au kukuvusha kwenda sehemu husika ,but ujuzi,ujuzi,ujuzi.

UJUZI NI KILA KITU.

Zamani kidogo wakati najitafuta,nilikuwa nalipwa take home 650k,ilikuwa haikidhi malengo kama mwanaume mwenye mke na mtoto mdogo kipindi hicho.

Lakini Kwa mara ya Kwanza nilishika Milioni 35 Kwa kufanya kazi ya wiki mbili tu kwenye kampuni moja ambayo miezi michache ilinipeleka Japan nikatengeneza pesa ,nasisitiza UJUZI ndiyo maana ya MAISHA
 
Back
Top Bottom