Biashara ya kuweka kwenye maduka imekaa kitapeli sana, unakuta umebahatika kupata mtaji wa million tano ukisema utafute Frame, unapita zaidi ya laki mbili, Frame yenyewe ukishaifungua utakutana na maafisa njaa kali wa halmashauri na TRA na wengine kibao ili ufunge ufurisike,
Jikite kwenye ujuzi brother tafuta niche unayoipenda ya ufundi then jua ndani nje, namaanisha jua mpaka uhakikishe hakuna mtu mwingine anayejua zaidi yako, then ukimaliza hiyo hela yako ndogo uliyonayo, ndio iwe kama toools au starting point.
Nimesema haya kwasababu nimemkuta kijana fundi simu anaingiza 60,000-100,000/= kwa siku, nimeshangaa kwasabu nimemkuta na microscope, TV kubwa, pamoja na vifaa basi mteja akifika pale anaifanyia diagnosis kwa kutumia microscope n.k watu wamemuamini sana na kazi zimemzidia, katika kushare story yake alianza kwanza kutafuta ujuzi then akainvest kununua spare za simu kwahiyo anauza spare na kuzibadilisha...
Mwingine ni fundi umeme wa magari, hapa nisiongee sana, ni darasa la saba tu lakini pia kufungua duka la spare za magari na bado ni fundi.
Mwingine ni fundi wa kuchomelea na aluminium kajiset barabarani, yupo na work shop nilishangaa anatengeneza vifaa vya chuma vyote unavyovijua wewe ,kuanzia jembe, toroli, pilau za tractor n.k
You see? Find niche then wekeza muda wako woote, jifunze tafuta source mbali mbali mtandaoni kuwa guru katika eneo moja.
Huo ndio ukombozi kwa vijana.