Uchaguzi 2020 Kama una mtoto Sekondari na unataka asome hadi Chuo Kikuu na huna uwezo kumlipia, linganisha sera uchague sahihi usije baadaye kujilaumu

Uchaguzi 2020 Kama una mtoto Sekondari na unataka asome hadi Chuo Kikuu na huna uwezo kumlipia, linganisha sera uchague sahihi usije baadaye kujilaumu

Duniahadaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2017
Posts
336
Reaction score
677
Vijana wengi wanaacha masomo ya Chuo Kikuu kwa sababu asilimia ndogo sana ndio hupata mikopo. Sera ya CCM ni kuwapa mikopo mayatima tu. Soma sera hii ya CHADEMA halafu fanya chaguo sahihi kwa ajili ya mwanao.

"Ugharamiaji wa elimu ya juu ndio changamoto kubwa kwenye elimu ya juu na hivyo kusababisha watu wenye sifa za kusoma kushindwa kupata ufadhili wa Serikali. Kwa muktadha huo Serikali ya CHADEMA inasema kuwa itahakikisha wale wote wenye sifa za kujiunga na vyuo vya kati, vyuo vya ufundi na vyuo vikuu wanapewa mikopo bila ya ubaguzi wowote". (Ukurasa wa 36)
 
Kwa kweli mfumo wa sasa wa mikopo umekuwa kama kucheza cheupe chekundu, kwa hili ccm hawatufai,
 
Eti kigezo cha "mtoto kupata mkopo tena mkopo sio hisani hapana mkopo"eti eti iwe ni yule ambae an are kodi ya kusoma shule tu za serkali kama amesoma private Hana sifa ya mkopo?

Eti kigezo cha mkopo ni mzazi kutokua na leseni ya biashara kama ulikua nayo mwanao Hana mkopo. Watu tunajiuliza hyu mtoto kwanini abaguliwe?Kwani mtoto akisomeshwa private si mzazi amekua ameisaidia serkali?kwani tena serikali ianze kumwadhibu?

Kwani hyu mzazi si ni mlipakodi?kwanini yeye abaguliwe kupata fursa or benefit za kodi yake kwa Taifa lake?
Kwanini kigezo cha mkopo isiwe ni maksi za wanafunzi ili as iwapo wa kumlaum mwenzake?
 
Inabidi ccm apite tena ili watanzania vilaza waendelee kuisoma namba, mfumo wa elimu uzidi kuharibika ili watu tupate fursa humo humo

CCM OYEEEEE
Tukiichagua CCM na mgombea wake mwaka huu, si tu Mungu atatushangaa ila hata Shetani atatushangaa kweli!

Huwezi kuwekewa mfumo mbovu wa elimu wa kibaguzi namna hii na kutamkiwa waziwazi Eti ukichagua mpinzani sahahu maendeleo wakati na wewe unalipa kodi alafu mwisho uchague Magufuli na CCM. Lazima Mungu na shetani wakuone wewe ni mjinga wa kutupwa!
 
Inabidi ccm apite tena ili watanzania vilaza waendelee kuisoma namba, mfumo wa elimu uzidi kuharibika ili watu tupate fursa humo humo

CCM OYEEEEE
MAENDELEO ni kodi zetu

Hazikusanywi kwa kadi za vyama vyetu

Tusipewe kwa rangi zetu

Kuchaguliwa/kuchagua ni haki yetu

Kodi ni pesa ya watanzania wote

Wasipochagua chama chako usiwachukie

Wasipokupenda, wakikukosoa, usiwakasirikie

Wanalipa kodi, wapewe maendeleo, Magufuli Usiwafokee wananchi.
 
Back
Top Bottom