Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Wale wakimya nchi zenye upweke ndo zinatufaaa, maana ukitoka kazini ni kujifungia ndani, mwenye uzi endelea kushusha nondo watu tujilipue maana bongo hali ni tete
Mimi nashangaa sana kumbe watu kujazana kariakoo na kupigiana kelele kwao ni faraja, au kukaa vijiweni kubishana mpira kutwa mzima wanaenjoy sana.

Tuko tofauti sana, Mimi Bongo yenyewe nikiwa sina issue huwa sitoki ndani kabisa hata siku kadhaa namaliza mambo yangu online.
 
Roho mbaya watz tumefundishwa na CCM
 
Hapo ni Kwa mji gani!? Vancouver ama Toronto!?
 
Ila hata kibongo bongo ni cheap pia.....
Ukiambiwa ukafanye hizo kazi. Kule moshi au Arusha huwezi kukubali. Ila Ukiambiwa uende ukafanye same job USA au UK unawahi ndukiii...

Ila haya maisha Jaman dah basi tu.
True,thus wanaotaka mkoa ndio ufanikiwa ndio hawa machinga, bodaboda, wauza kahawa,mayai,karanga,matunda, maduka.
 
Kuliko kupoteza mda kutembeza bahasha ukitegemea kuokota kazi.
Kula kozi fupi ya ubaharia uza Shamba ingia Canada, korea kusini, Dubai, omba kozi ya kuendelea na kozi ya ubaharia Ili upate viza, piga shule kamata meli.
NB ubaharia ni wito, ni hobby, ni adventure ni Kazi ya kijana miaka 30 kushuka chini au miaka 50 kwenda juu ambae alishamaliza kuzaa. Hii Kazi ni kukaa mbali na familia.
Kazi ya kukaza moyo ukiwa mtoto wa Mama achana na Kazi hii, kuna mikondo huko utaomba poo ushuke.
 
Usa zipo kampuni za usafirishaji hizi Kazi za udereva usa na canada ufanywa na wakuja yaani maforegner wahindi, malatino, waafrika huwezi kuta mzawa mtoto wa Kizungu anasukuma malori ni wachache.
Zipo kampuni unaingia nao ubia wao wanakulipia kozi za udereva na kupewa posho makubaliano kama upo na document fully, then baada ya kozi wanakuajiri kwa kukulipa posho au nusu mshahara, hadi deni lao liishe, then unakuwa huru kuendelea nao au kutoendelea. Ukikiuka taratibu unafungwa au la unawalipa gharama zao unaachana nao.
Wenzetu wameseti mifumo ya maisha tangu unazaliwa hadi unakufa unapita wapi unatoka wapi. Mifumo yao inawapush watu wao kutimiza ndoto zao.
Masikini hawakosekani zipo fact, uteja, kutofata miongozo, mitindo ya maisha, ulemavu wa viungo, ulemavu wa fikra, nk.
Watz hawafanikiwi nje sababu wanajisahau
 
Us labda kama umeipata Akira Ubalozi WA Tanzania huko au Umoja wa Mataifa. Ile ni nchi ambayo inakuhitaji uwe na Hela Ili utoboe sio nchi ya kwenda kutafuta maisha. Ukiumwa wanaangalia bima yako ni ya aina Gani ndio waanze kukutibu.
 
Kazi za ubaharia Dubai unazipateje kwa wakala au unafanyeje
 
Us labda kama umeipata Akira Ubalozi WA Tanzania huko au Umoja wa Mataifa. Ile ni nchi ambayo inakuhitaji uwe na Hela Ili utoboe sio nchi ya kwenda kutafuta maisha. Ukiumwa wanaangalia bima yako ni ya aina Gani ndio waanze kukutibu.

Hivi nani anawapa hizo story?

Kuna watu wenye asili ya tanzania zaidi ya 50k USA (ballpark number), unadhani wote wanafanya kazi ubalozini?

Diaspora wa US ndo wanaongoza kutuma hela bongo, unadhani zote zinatoka ubalozini? Kama hizo nchi zingine watu wakienda wanafanya vizuri wangeongoza kutuma hela wao. This fact alone dismantles your point.

Nchi yeyote inampa mtu matibabu tokana na hali yake, kama huna bima utapata huduma ya wasio na bima. Watu kila siku wanakuja kujifungulia US unadhani wana bima za kupata matibau au wanagomewa kujifungua?

Watu wanafika US leo na kesho wanaanza kazi za kujikimu na kutuma kwa ndugu zao bongo. Huko Asia watu wanakaa miaka na bado hawana kazi mwishoe wanakua punda.

Sipo hapa kuwaambia watu wapi kwa kwenda, but they ought to choose wisely, it's not by chance watu wa mataifa yote kujazana hapa.

Umewahi kusikia wamarekani wengi wanaenda kuishi China, Korea au Europe? Exactly. Ila unajua kuna wageni wangapi hapa. Umewahi kusikia a US town in China au Korea? Ila karibu kila nchi ina town yake in the US. It's not by chance my friend. There's a reason US ni superpower.

Wasomali hawataki kwenda Saudi Arabia au middle East wote wanakuja USA. Ukienda Minnesota imekua Somalia kabisa hadi congress woman wa pale ni msomali. Umewahi kusikia mwanasiasa mwenye asili ya nje china, japan au Korea? That the point, US ndo nchi pekee ambayo mtu yeyote anaweza kuwa yeyote so long as you're willing to put in the work.

Nipo around mazee.
 
Kama unaenda kukaa huko sawa ila kama unataka kwenda nje kutafuta Hela halafu urudi kufanya Mambo makubwa US sio nchi ya kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…