Kama una ndoto za kuanzisha biashara anza kwanza kutafuta wazo la biashara kabla ya mtaji au tafuta vyote kwa wakati mmoja

Bodhichitta

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
315
Reaction score
762
Aslaam,

Kutokana na changamoto za Maisha ambazo hutufanya kawaza kutafuta ridhiki kila kukicha, wengi tumejikuta kujikita Mawazo yetu kwenye kufanya biashara ili tuweze kujikwamua katika mambo mbalimbali ya kimaisha hasa kwenye Nyanja za maendeleo.

Imekuwa kawaida yetu mtu anapowaza kujiajiri katika biashara jambo la kwanza hufikiria mtaji, na huenda akachukua mda mrefu saana kukusanya mtaji na hatimae kuupata.

Lakini baada ya kuupata mtaji kimbembe huja pale anapojiuliza nifanye biashara gani kwa ule mtaji aliopata.

Wengi wanapofikia kwenye hatua hii hukwama na wengine hujikuta wanachukua mda mrefu kiasi kwamba kile kiasi huenda wakatumia kwenye matumizi mengine tofauti na biashara au kufanyia jambo ambalo nje ya biashara.

Binafsi nashauri kabla hujaanza harakati za kutafuta mtaji anza kwanza kutafuta wazo la biashara then ukilipata uchanganue vizuri ili ujue ni kiasi gani unaweza kuanza nacho kwenye hilo wazo lako la biashara.

Imekuwa kawaida humu kwenye JF kusikia mtu anasema(ikiwemo na mimi mwenyewe) nina kiasi flani nifanye biashara gani, lakini imekuwa mara chache saana kusikia mtu akisema nina wazo flani nahitaji mtaji kiasi gani kukamilisha.

Hii inaonesha kwamba ni rahisi kupata mtaji kuliko wazo la biashara kwa wale ambao ni mara yao ya kwanza kuingia kwenye biashara.

Na pia si vibaya kushirikishana baadhi ya Mawazo ya biashara na uzoefu kwa wale ambao wamefanikisha kwenye baadhi ya biashara zao ili kuonyesha njia kwa wengine
 
Naweka kambi hapa kusikiliza mawazo tofauti tofauti, litakaloingia kwenye mfumo wangu naruka nalo
 
Back
Top Bottom