mashuka collection
JF-Expert Member
- Apr 10, 2023
- 608
- 1,409
Pole sana ila ni vizuri ungenda kkkt unaposalia sababu huko wanakujua zaidi sikuhz dunia imeharibika sana uwezi kuamini kila mtu anaekuja kuomba msaada wengi matapeli.Kuna mwaka nilipitia msoto mkali nilikua mitaa ya ITV nikasema ngoja niende kanisa la lutheran lililopo karibu na ITV linaitwa usharika wa Mwenge.
Nikaingia pale ila sikumuona mlinzi nikamuona mmama upande wa kushoto nikamfuata kumbe kule ndo kuna ofisi za mchungaji nikamfuata akaniambia mchungaji.
Tukaongea wewe baada ya mazungumzo to be honest nilikua sina hata mia mfukoni akampigia mlinzi kwa pembeni akaongea nae baada ya muda akaniambia nimfuate mlinzi yaani yule nilimuomba tu nauli nilikua nimebanwa ila hakunisaidia japokua anafanya kazi kwenye ofisi ya mchungaji to be honest ana roho ngumu sana.
Nilipomfuata mlinzi akaanza nifokea nikamuomba samahani kwa kuingia bila kumjulisha eeh bwana akaendelea kunifokea tena kwa sauti nikamwambia hata kama nina shida usidhalilishe utu wangu nikaondoka.
Nilichojifunza ni ngumu sana kupata msaada kwenye kanisa la KKKT kama hawakujui yaani makanisa yao sio nyumba ya Mungu anymore.
Baraka za Mungu zipo katika maeneo madogo madogo na usiyoyatarajia mfano anaweza akaja mtu smart akakuambia hana hela ya kula wewe utambeza na hutampa ila ndo umesakosa baraka za Mungu hivyo
Pia umenda kanisa moja tu then unageneralize taasisi nzima ni wabaya!