Kama una shida ni ngumu sana kupata msaada kwenye kanisa la KKKT kama hawakujui

Pole sana ila ni vizuri ungenda kkkt unaposalia sababu huko wanakujua zaidi sikuhz dunia imeharibika sana uwezi kuamini kila mtu anaekuja kuomba msaada wengi matapeli.
Pia umenda kanisa moja tu then unageneralize taasisi nzima ni wabaya!
 
Mimi ni KKKT nimebatizwa 2001 na kupata kipaimara 2009 ila binabsi naunga mkono hili kanisa ni kirusi wachungaji na viongozi wa kanisa hawana upendo wa Mungu wana roho mbaya na wapo kimaslahi.

Usharika tu wa hapa KKKT kinyerezi kumuona mchungaji utaratibu mwingi na masharti kibao kama unataka kumwona Rais wa nchi....

nimewaachia kanisa lao.
 
Huo ndo ukweli
 
Uko sawa ila utajiitaje mkrosto na sio mshirika na mwanafunzi wa kristo. Pambana tu na hali Yako.
 
Ndo maana europe makanisa hayana watu sitakaa nimsahau yule mlinzi hivi unamfokeaje mtu mwenye shida
Nilijiuliza utu uko wapi
Tokea siku hiyo nikasema sitakaa nikanyage kanisani mpaka sahivi sina dini tena
We una matatizo Yako tu na kanisa. Una generalize mtazamo wako Kwa tukio moja ambalo inawezekana wewe pia ulizingua.
 
Mkuu pole sana kwa kudandia mtumbwi wa vibwengo.

Asilimia kubwa (yaweza kua wote) ya waumini wa hilo Kanisa wanatokea mkoa ambao watu wake wanaijua pesa sana hivo sio rahisi kusaidiwa.
 
Makanisa mengi ya wakristo kama huna hela na hawakujui utaonekana takataka tu
Usiende kanisani ili watu wakuone, nenda ukutane na Mungu wako . Hao unaowaona kanisani wana mizigo Yao mizito moyoni
 
Huo ndo ukweli
Umechelewa kulijua hili unajua kila kanisa lina vijana.....sasa kanisa kwenye mambo yao wanawatumia tu vijana watakavyo ila hao vijana wakipata changamoto za hapa na pale wakisema walikimbilie kanisa ambalo wanaamini ndio mkombozi wao kwa kuwa face viongozi wakiwemo mchungaji hapo ndipo utaona kivumbiiii.........

Mwisho wa siku ukijua nao ni binadamu kama sisi na madhaifu yao kama roho mbaya na husda unapotezea na kuendelea na life lako huku ukiendelea kumuomba Mungu wako.

Sijakanyaga kanisani tangu 2019(at 23 yrs age) na sitegemei kukanyaga sehemu za watu wabinafsi tena kama kanisani.
 
Kuna siku nilimsikia omba omba akiwa anaongea na mafundi kuhusu finishing ya nyumba yale Kigamboni. Na yupo kwenye wheelchair..

Mimi nategemea busara na upole wa mwenye nyumba mjini. Kutoka siku hiyo nikajiambia sitatoa hela kwa omba omba barabarani kamwe.
 
Wewe dini ikitajwa na kuhusishwa Kinacho kuuma ni nini?
 
Jifunze kutoka kwa marais wetu wa kikristo hapa Tanzania, ulinganishe!
 
Wataalam watasema ni tangazo ila ndo ukweli
 
Kanisa lolote halitoi msaada kwa mtu wasiemjua
 
Shetan ndio mungu na mungu ndie shetani ukimuomb shetan fasta tu kakupa ila mwombe mungu hapo atapitia kwanza cv yako ulizin wap nanani? Kwanin? Had kuja kupata ushakata tamaa au ushapata
 
Kanisa lolote halitoi msaada kwa mtu wasiemjua
Me nilikuwa msharika na nafahamika na bahasha ya sadaka nilikuwa nayo hadi kwenye majumuiya yao ya mchongo naenda na yalikuwa yanaanza saa 12 kamili asubuhi jumamos you can imagine weekend unaamka saa 11 ili uende jumuiya

Na walinitosa washenz wale na kuniambia nifanye maombi wakati wao wakiwa na shida zao mbio kuchangisha washarika.

KKKT muamala mbele kama huna muamala kaa kushoto ndivyo yesu wao alivyowafundisha.
 
Ungeenda umevaa nguo za CHADEMA. Hilo kanisa ni tawi la chama. Hujaona majuzi wamemnunulia Askofu mstaafu gari za la zaidi ya 300m? Hilo kanisa usiende ukiwa choka mbaya.
 
Hapana mimi kwa experience nimewahi kuona mtu mkristo akipewa msaada msikitini jirani na napoishi.
Nadhani hukuwahi kupata habari za ajira zinavyotolewa NSSF ile ya Ramadhan Dau. Kama ungelisikia hata kidogo huku ukiwa na ndugu yako ambaye amehitimu na sifa zote za kuajiriwa pale, ungeifuta kauli yako
NB: Chukua sampuli chache za ajira za makampuni ya S.S. Bakhre

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…