Kama una shida ni ngumu sana kupata msaada kwenye kanisa la KKKT kama hawakujui

Matapeli + wauaji wengi hutumia maeneo ya kanisa kufanya nia zao ovu.
Ulisikia yule mtu alimuua padri huko Karatu miezi kadhaa nyuma?
Unataka watumishi/wachungaji wacheke na kila mtu anayekuja kanisani wakiuliwa/kuibiwa nani alaumiwe?
 
Wewe una chuki zako binafsi...Aliyekushusha utu ni huyo uliyekutana nae na sio kanisa
 
Matapeli + wauaji wengi hutumia maeneo ya kanisa kufanya nia zao ovu.
Ulisikia yule mtu alimuua padri huko Karatu miezi kadhaa nyuma?
Unataka watumishi/wachungaji wacheke na kila mtu anayekuja kanisani wakiuliwa/kuibiwa nani alaumiwe?
Upendo wa kweli haupimwi kwa watu unaowaju bali kwa usiowajua
 
Ndo maana europe makanisa hayana watu sitakaa nimsahau yule mlinzi hivi unamfokeaje mtu mwenye shida
Nilijiuliza utu uko wapi

Tokea siku hiyo nikasema sitakaa nikanyage kanisani mpaka sahivi sina dini tena
Sasa mlinz anaeza kuwa hata dhehebu lingne au dini nyingine,ww uctuchafulie kanisa letu,sema hiyo siku ilkua mbaya tu kwako,kuna cku unaamka inakuwa mbaya kuanzia asbuh mpaka kulala,ila watu wema sio lazima wawe makanisani ,unaweza kuwakuta watu wema bar au hata sehemu nyingne za dhambi na ushangazwe na utu wao.sasa ww ukakariri kanisan pole
 
Umeeleza vizuri ila huku mwishoni ndo ulipoanza kuvuruga
 
Ningesema nimeenda kutoa sadaka na maombi ningefanyiwa
Yani kwa akili zako uende Msimbazi center utapewa hostel ulale bure na ule bure canteen kisa wewe ni Mkristo au Mkatoliki?

Taasisi Mara nyingi hazitowi msaada individual, huwa zinatowa msaada kwa magroup yenye uhitaji wa shida Fulani.

Kwa mfano kuna taasisi ya Waislamu inafadhili upasuwaji bure kwa watu wenye matatizo ya mtoto wa jicho, taasisi inacover gharama za upasuwaji ambazo si chini ya million 3, na hao siyo waislamu hawa wachezaji bao, pesa zinatoka overseas.

Agha Khan ni hospitali ya taasisi ya kiislamu, nenda na mandevu yako pale uwaambie huna uwezo unahitaji matibabu uone.
 
Usiingie nyumba ya mtu bila kubisha hodi.
 
Kwa utapeli uliojaa mjini, siwezi kuwalaumu, huwezi kutoa msaada wa pesa kwa kila MTU anayedai ana "shida"! Utathibitisha vipi? Kuwa mpole, toa maelekezo ya kutosha.
 
Bro mbona unabadilisha mada
Unafananisha afgha khan na kanisa unavituko

Kanisan ni sehemu watu wanapeleka mizigo yao ni kazi ya kanisa kuwatua ndo maana ya kanisa

Tofautisha kwenda kuomba unafuu na mtu ana shida ya dharura
 
Kwa utapeli uliojaa mjini, siwezi kuwalaumu, huwezi kutoa msaada wa pesa kwa kila MTU anayedai ana "shida"! Utathibitisha vipi? Kuwa mpole, toa maelekezo ya kutosha.
Yaani husaiidii watu kwa sababu ya utapeli
Kusaidia ni moyo ila kama huna huo moyo utatafuta visingizio vingi sana

Kuna yule mmama alikua na madeni na ilikua watoto wake wanaenda utumwani akishindwa kulipa na akenda kwa elisha
Elisha hakumpa hata mia ila alimsaidia kwa kumpa neno

Kazi ya kuwapa watu neno na likawasaidia ndo wako waliokua wanaonfuata Yesu na kumwambia sema neno tu

Sasa kama kanisa ni mwili wa kristo na halijui hili ndo maana ukienda ulaya makinisa yapo tupu kwa mambo haya haya
 
Bro mbona unabadilisha mada
Unafananisha afgha khan na kanisa unavituko

Kanisan ni sehemu watu wanapeleka mizigo yao ni kazi ya kanisa kuwatua ndo maana ya kanisa

Tofautisha kwenda kuomba unafuu na mtu ana shida ya dharura
Agha Khan ni taasisi ya kidini ya kiislamu, labda hujui hilo.
 
Agha Khan ni taasisi ya kidini ya kiislamu, labda hujui hilo.
Sasa sio msikiti alafu usijione una akili kwa mambo ya kawaida sana
Mimi nilishaenda kwenye sherehe yao yule kiongozi wao wa agha khan kama dhehebu la waislamu na kiongozi wa agha khan zote duniani alivyokuja pale diamond jubilee nilipewa tenda kwenye ile shuhuli yao kwa hiyo usinione ni lofa
 
Bahati mbaya sana wapo watakaoamini maneno haya.

Nikuulize,ulipata changamoto gani ya kimaisha au kiimani kiasi ukawa unahitaji msaada kwenye hayo makanisa?
makanisa si kwa ajili ya changamoto za kiimani tu.

Mwili ndio wenye changamoto, hatuishi kwa imani,hatuli imani,hatuvai imani,hatutembelei imani. Tafakari kisha Chukua Hatua.
 
makanisa si kwa ajili ya changamoto za kiimani tu.

Mwili ndio wenye changamoto, hatuishi kwa imani,hatuli imani,hatuvai imani,hatutembelei imani. Tafakari kisha Chukua Hatua.
Sikuhukumu,lakini humo niliko-bold sijui kama unaijua imani yako kisawa sawa.

Tukirudi kwenye mada pale juu kama nilikusoma vizuri ulijipambanua kama m-KKKT,je wakati unakutana na hii changamoto ulikuwa na ushiriki wowote kama mwanakanisa?jumuia etc,hili Kanisa ni taasisi haliwezi tu kuwa linasaidia kila anayeingia kuomba msaada eti kwa sababu ana njaa huku akionekana wazi ana mikono miwili na miguu miwili ishara ana uwezo wa kujitafutia(hiyo nafasi ya unaohisi walikunyima msaada kaa wewe jipime ungefanya ulichotaka ufanyiwe?) kama una ulemavu wowote sawa.

Kanisa lina utaratibu wake,siwezi kutoka mbio mbio kwenda kuomba msaada usiokuwa wa kiroho Kanisani huku nikiacha kwenda kwa mwanaushirika mwenzangu kumlilia shida na ktk situation kama hii kama yeye hana nitaenda kwa mwenyekiti au katibu wa jumuia yangu yeye ataliwakilisha kwenye jumuia nitapata msaada (mimi Mkatoliki jumuia yangu inafanya haya ikithibitika kweli mwanajumia ana shida)

Jenga utaratibu wa kushiriki na wenzako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…