Kama una shida ni ngumu sana kupata msaada kwenye kanisa la KKKT kama hawakujui

Kama una shida ni ngumu sana kupata msaada kwenye kanisa la KKKT kama hawakujui

Mwaka 2017 nilipata mtoto wangu nikasema nikambatize, Huwa mimi n mtu naenda kanisani mara kwa mara ila sipendi utaratbu wetu wa LUTHERAN ule wa BAHASHA ya AHADI.

kwahiyo nikienda kanisani sinaga time na ile bahasha naenda natoa sadaka yangu kimya kimya nasepa.

Bwana imefika wakat wa kubatiza naenda pale naulizwa Bahasha yako ya Ahadi ni Namba Ngapi?

Nikasema SINA BAHASHA wakasema hatubatizi watoto wa msharika ambae hajasajiliwa kanisani na hana bahasha kwahyo katafute picha za pasport akanipa utaratbu wa kupata bahasha pale nikaondoka kufatilia.

Nikasajiliwa wakambatiza mwanangu, baada ya Pale 2017 kanisani naendaga kupitia Clip za youtube na Tik Tok.

Nikarudigi siku 1 kanisani kwenda kwenye bahasha namba yangu nikakuta washampa mtu mwingine.

Nitaenda kufatilia tena BAHASHA YA AHADI nikiwa nataka Kuoa, nikishaoa Tu tutakutana siku ya mazishi tena ntaenda kufungua bahasha ingine ya ajadi siku ya msiba.

Ki ufupi Kwenye Misaada Wakristo na Waislamu nawapa High Rate Waislamu.
 
Kuna katekista mmoja kama si wazee kumficha na kumtorosha kwa kasi ya ajabu asichezee kichapo toka kwa waombolezaji baada ya kukataa kuendelea na ibada ya mazishi kwa mtoto wa darasa la sita akidai alikuwa hahudhurii vipindi kanisani yeye na wazazi wake. Waombolezaji walidai kwani mtoto ana dhambi gani mpaka akataliwe kufanyiwa ibada ya maziko? Hata katoliki nao wana mtindo wa kujifanya kutotambua waumini wapatapo shida kwa vigezo vya ajabu ajabu.
 
Note
Unahaki ya kumnyima mtu msaada sio dhambi au kosa ila usidhalilishe utu wake kama hauna nia au hutaki kumsaidia

Kuna mwaka nilipitia msoto mkali nilikua mitaa ya ITV nikasema ngoja niende kanisa la lutheran lililopo karibu na ITV linaitwa usharika wa Mwenge.

Nikaingia pale ila sikumuona mlinzi nikamuona mmama upande wa kushoto nikamfuata kumbe kule ndo kuna ofisi za mchungaji nikamfuata akaniambia mchungaji.

Tukaongea wewe baada ya mazungumzo to be honest nilikua sina hata mia mfukoni akampigia mlinzi kwa pembeni akaongea nae baada ya muda akaniambia nimfuate mlinzi yaani yule nilimuomba tu nauli nilikua nimebanwa ila hakunisaidia japokua anafanya kazi kwenye ofisi ya mchungaji to be honest ana roho ngumu sana.

Nilipomfuata mlinzi akaanza nifokea nikamuomba samahani kwa kuingia bila kumjulisha eeh bwana akaendelea kunifokea tena kwa sauti nikamwambia hata kama nina shida usidhalilishe utu wangu nikaondoka.

Nilichojifunza ni ngumu sana kupata msaada kwenye kanisa la KKKT kama hawakujui yaani makanisa yao sio nyumba ya Mungu anymore.

Baraka za Mungu zipo katika maeneo madogo madogo na usiyoyatarajia mfano anaweza akaja mtu smart akakuambia hana hela ya kula wewe utambeza na hutampa ila ndo umesakosa baraka za Mungu hivyo
Easy;
Basi nenda kaombe msaada kanisa la Catholic.
 
Nishasaidiwa na waislamu lakini sio wakristo, na hawa KKKT,RC na madhehebu haya makubwa ndio usilogwe kwenda omba msaada.

Msaada ukipata shida heri uonde kwenye vile vikanisa vya mabati mabati wale watakusaidia mpka utashangaa.
 
msiktini pia uwe na jina la kiislam mkuu...nakukumbusha tu

sio kweli ndugu yangu angalia You-tube utaona mchungaji (pastor) huko Nigeria alikuwa anasafiri giza likaingia kabla hajafika alipotarajia akaenda kanisani akajitambulisha kuwa yeye ni pastor na akaomba alale hapo kanisani lakini mchingaji mwenzake alimkatalia. Akaondoka akaenda msikitini akaomba alale hapo wakamkubalia na chakula akapewa..kwa hivyo sio kweli kwamba eti wanaosaidiwa msikitini ni waislam tu sio kweli. Cheki hiio link hapa chini utaona hiyo video huyo mchungaji anawasimulia waumini wake kanisani namna kanisa lingine lilivyo mtreat na jinsi alivyosaidiwa msikitini.

View: https://youtu.be/lSlUlgQCXfQ?si=uAtlrsCGp8iiYTMa

Uislamu ndio dini ya kweli na wakristo wengi wanakiri mara nyingi kupendezwa na mambo mengi ya uislamu ila tu mnaogopeshwa na viongozi wenu huko makanisani au western media kuwa waislam ni magaidi au wanafuga majini ili msiwakimbie huko makanisani mkaisha kwani wao wanategemea sadaka zenu ili waishi.
 
Ila twende mbele turudi nyuma, ndugu zetu wafilisti wana utu sana, unaweza kupata hifadhi ya kulala msikitini kuliko kanisani na huo ndo ukweli

Nimeshuhudia misikiti mingi watu wanalala asubuhi wanaenda kujitafuta ila sio makanisani
Msikitini hakuna kitu cha kuiba mule sana sana labda ung'oe feni au mikeka. Kanisani kuna vitu vya thamani kubwa
 
We kama huna dini ni wewe.
Usiwalaumu watu kuamini dini zao.
Hekima ni kutodhihirisha upumbavu wako.
 
Well muislam anamsaidia muislam mwenzake hilo linajulikana wazi ila Mkristo anamsaidia yeyote bila kujali imani yake muhimu sababu za msaada ziwe za msingi kitu ambacho hata Muislam hamsaidii muislam mwenzake kama hana sababu za msingi na akili zenu mmeshazi-set tukienda kuomba msaada kwa asiye mwenzetu hatutasaidiwa so huu utafiti hauwezi kutoa majibu sahihi,nani ameenda kuomba msaada kwa jirani yake mkristo hakusaidiwa?siyo umfuate yeyote tu njiani eti sababu anazo signs za Ukristo umuombe msaada hata wewe na uislam wako unaojiona nao mzuri sana kwa njia hii hutatoa na hutoi msaada.

Jitokee leo hapo ulipo nenda kwa unayedhani ni muislam jifanye mkristo kamuombe msaada from no where uone kama utasaidiwa.msaada anatoa yeyote inazingatiwa ni ana huruma kiasi gani ndani ya nafsi yake na anamiliki nini haizingatiwi dini,huyo aliye-post post hiyo alikupaka mafuta kwa mgongo wa chupa tu acheni kufarijiana ujinga.
 
You said petty issue lakini nakuwekea andiko hapa uone how petty it is....

Ufunuo wa Yohana 22:18 - 19

Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

Halafu soma hili...

Marko 16:16
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
MImi nasema ima kubatizwa mtoto au mtu mzima hiyo ni kitu minor mno kwenye Imani!
 
Note
Unahaki ya kumnyima mtu msaada sio dhambi au kosa ila usidhalilishe utu wake kama hauna nia au hutaki kumsaidia

Kuna mwaka nilipitia msoto mkali nilikua mitaa ya ITV nikasema ngoja niende kanisa la lutheran lililopo karibu na ITV linaitwa usharika wa Mwenge.

Nikaingia pale ila sikumuona mlinzi nikamuona mmama upande wa kushoto nikamfuata kumbe kule ndo kuna ofisi za mchungaji nikamfuata akaniambia mchungaji.

Tukaongea wewe baada ya mazungumzo to be honest nilikua sina hata mia mfukoni akampigia mlinzi kwa pembeni akaongea nae baada ya muda akaniambia nimfuate mlinzi yaani yule nilimuomba tu nauli nilikua nimebanwa ila hakunisaidia japokua anafanya kazi kwenye ofisi ya mchungaji to be honest ana roho ngumu sana.

Nilipomfuata mlinzi akaanza nifokea nikamuomba samahani kwa kuingia bila kumjulisha eeh bwana akaendelea kunifokea tena kwa sauti nikamwambia hata kama nina shida usidhalilishe utu wangu nikaondoka.

Nilichojifunza ni ngumu sana kupata msaada kwenye kanisa la KKKT kama hawakujui yaani makanisa yao sio nyumba ya Mungu anymore.

Baraka za Mungu zipo katika maeneo madogo madogo na usiyoyatarajia mfano anaweza akaja mtu smart akakuambia hana hela ya kula wewe utambeza na hutampa ila ndo umesakosa baraka za Mungu hivyo
Pole sana ndugu, Samehe, songa mbele na mshukuru Mungu!
 
Nishasaidiwa na waislamu lakini sio wakristo, na hawa KKKT,RC na madhehebu haya makubwa ndio usilogwe kwenda omba msaada.

Msaada ukipata shida heri uonde kwenye vile vikanisa vya mabati mabati wale watakusaidia mpka utashangaa.
Bahati mbaya sana wapo watakaoamini maneno haya.

Nikuulize,ulipata changamoto gani ya kimaisha au kiimani kiasi ukawa unahitaji msaada kwenye hayo makanisa?
 
Ila waislam bwana, naona sijui ndo dini yao

Maeneo ya mjini wakiona jeneza linapita unasikia " ngoja tukapate dhawabu" apo anaunga tela
Mojawapo ya wajibu wa Muislam kwa muislam mwenzie ni kumzika pale anapofariki. Hivyo unapomuona muislam anashiriki kwenye mazishi ya mtu asiyemjua basi ujue anatimiza wajibu wake kama muislam
 
Tuna kalili maandiko na kanuni za dini zet, lakini hatuna UTU
Iko hivi ,sisi binadamu kabla ya kufunzwa chochote cha kidini tunazo nafsi ndani mwetu zenye huruma na zisizokuwa na huruma so kama mtu hana roho ya huruma hata kama akawa ni mchungaji sijui padre sheikh atheist etc ni hawezi kutoa msaada labda kama ana kitu ata-earn kutokana na msaada huo,umaarufu maslahi etc.

Lakini ukiwa na roho ya huruma hata atheist anasaidia utasema huyu ni dini gani?utasaidia yeyote popote kwa sababu unasukumwa na nafsi yako na hii hata wasiomkiri Mungu wanaifanya,kusema eti muislam ana msaada zaidi ya mkristo kauli hii atakaeielewa ni mtu mpumbavu mwenye degree ya ujinga sababu utakuta hata yeye kama hakupewa moyo wa huruma anashangalia tu kinafiki na ndiyo wengi wapo ktk huu uzi.
 
Back
Top Bottom