Kuna mama mmoja mume wake alikua akimtesa sana kwa kubadilisha michepuko, akaamua kwenda kwa mganga, mganga alimpa yule mama dawa za kila aina bila mafanikio, basi mganga nae akaona mwanaume kboko hapa nimeshindwa ila jinsi ya kumwambia bibie nimeshindwa hakumtamkia bali alimwambia amlete koboko ili wamtengenezee dawa. Yule mganga akiwa na hakika mwanamama hawezi kumkamata huyo nyoka. Bibie alianza kuzungukia mashimo ya nyoka porin moja baada ya jingine, na alifankiwa kumkamata koboko kwa kuweka unga katika chungu na koboko alipoingia ndani ya chungu alkifunika na kumpelekea mganga. Mganga hakuamin alipofunua chungu na alikimbia sana huku akimtukana yule mama, akisema kama umeweza kukamata koboko, mumeo anakushindwaje?
[emoji28][emoji28][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]