Niliingia kwenye choo cha uma mahali fulani, wakati naendelea na kukata gogo, nikasikia sauti kwenye choo cha jirani yangu akisema " halo, mambo vipi", kwa sauti ya kukereka nikajibu "niko poa" naye akaendelea kuongea "unafanya nini? Nikajibu "nafanya kile unachokifanya wewe", akaendelea "naweza kuja hapo", kwa hasira nikajibu "hapana, usije nipo bize sana kwa sasa" sauti hiyo ya choo cha jirani yangu ikasema "mshikaji ee nitakupigia baadaye, kuna mpuuzi mmoja mlango unaofuata anajibu maswali yangu yote, hatuelewani,,,,, hapo ndipo utakapojua kiherehere maana yake nini