Watu wengine wajinga sana,
Jana nimekaa na jamaa seat jirani kwenye basi tokea tunaanza safari kutoka Dar ubungo terminal tunaenda Morogoro
Jamaa ananunua vitu anakula hanikaribishi hapo tupo kibaha akanunua korosho hata kusema karibu Hakuna, ,
tulipofika Chalinze akaenda kununua nyama choma, mara mahindi ya kuchemsha ,
mara ndizi za kuiva , karanga mara hiki mara kile na anashushia tu juice na maji mwenyewe haniulizagi kitu wala kusema karibu. Mimi nipo zangu tu nasoma magezeti na kuchat ktk mitandao ya kijamii, ...
Tumefika Mikese nimetoa power bank yangu nataka kuchaji simu,, kumbe naye simu yake imezima charge.
eti ndio akaniuliza hiyo ni power bank??
mimi nikamjibu hapana ni embe dodo.
Hakunisemesha tena mpaka tumefika tumefika Morogoro .
Tumeshuka Morogoro msamvu stand terminal tumeshuka wote kumbe naye anaelekea Mazimbu akaniuliza tena kumbe tupo safari moja ya Mazimbu ??
nikamjibu hapana hatupo pamoja mi naelekea Gongolamboto ...
Hakunisemesha tena..!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji34] [emoji34] [emoji34] [emoji34]