Hii ni kweli kabisa...
Shule ya msingi, 1992 - Moshi, Kilimanjaro
Enzi hizo tulikuwa tunaenda shule na kuni. Asubuhi mstarini kila mwanafunzi anakaguliwa kuni ndo naingia darasani. Huna kuni ni adhabu.
Siku moja 'Joji mameno' (ndo jina lake la utani) kaja shule bila kuni. Akaja hivyohivyo mstarini huku anatabasamu kabisa. Sisi tunamuonea huruma maana mwalimu aliyekuwa zamu ndiyo alikuwa anashikilia rekodi ya kuwa mwalimu mkali kuliko wote, Mwalimu Msaki.
Dah ticha Msaki alikuwa anatumia mkono wa kushoto na akikasirika kabisa, anavua saa. Siku hii alivua saa kabisa halafu alikuwa na headboy anamfuata kwa nyuma huku kabeba burungutu la fimbo.
Mwalimu kufika kwa Joji akamuuliza kuni zake zilipo. Joji akaanza kujitetea, "mwalimu hakiyamungu vile nimekuja na kuni mwalimu. Sasa nilipofika niliziweka pale chini kwenye kona ili nikafagie kiwanja changu. Kurudi nikakuta imeibiwa mwalimu hata twende ukaone..."
Kumbe Joji kwa kujua hajaja na kuni, alienda hapo kwenye kona akaanza kupakanyaga na viatu, kisha akavua viatu akakanyaga peku hadi pakaonekana palikuwa pamepitiwa na watu wengi hivyo alivyofika pale na mwalimu akamwambia, "si unaona mwalimu hata nyayo zao hizi hapa walikuwa wanagombania kuni zangu."
.
.
.
Kama ulidhani Joji mameno alipona fimbo, na wewe mwalimu Msaki anakusubiria ofisini.
.
.
.
Dah by the way, RIP mwalimu Msaki.