Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

973237775afbe064aad874c89bfa6a24.jpg
. [emoji41]
 
Pana jirani yangu nimetoka kumuona muhimbili amejeruhiwa kichwani na mkewe nikamuuliza tatizo akasema yeye alikuwa penye ibada nikashangaa sana ibada tu mkeo akupige akajibu ndio nikauliza ilikuwaje
"Dear God thank you for mercy for grace and for joy now I have faith " nikamuuliza hivyo tu akajibu ndio niliomba hivyo. Basi muda wa kutizama wagonjwa ulivyoisha nikampakia shemeji njiani namuuliza ilikuwaje ndio akasema jamaa karibu mara ya tano anamvizia akidhani amelala anapiga magoti na kuanza kuwataja taja majina hao wanawake wake shemeji kweli nikashindwa kuvumilia nikampiga rungu kichwani. Nilishindwa kucheka ila hapa tupo kwa Ras simba na ada tayari nimemlipia.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] mie nitamwongezea na dictionary kabisa siyo kwa ubashite huo[emoji23] [emoji23]
 
*Manzi anakupenda balaa.. Anasubiri wewe tu umwambie ili muanze maisha matamu. Tatizo moja linajitokeza, we ni domo zege* [emoji134]♂[emoji134]♂[emoji134]♂
[emoji134]♂
*Unajikakamua usiku huo, unamtumia meseji kuwa unakitu kitamu sana cha kumwambia. Demu anakujibu kwa bashasha, niambie. Unakaa kimya dakika 10. Anatuma txt ingine kuomba umwambie.*
*Unaamua kughairi kumwambia kwa madai ni jambo la kipuuzi sana hasa kwa umri wenu. Ila demu anakusisitizia umwambie. Anakopa hadi salio na kukupigia akiomba umwambie hivyohivyo. Unaamua kumwambia kuwa utamwambia kesho Manzi hana jinsi, anaamua kutry to sleep with broken heart.*
*Kesho yake mtoto anajipara balaa. Tena anachagua saa 2 usiku ambapo tayari wazee wake wamelala. Mnakutana maeneo fulani ambapo watu si rahisi kuwaona. Unaanza porojo zako. Mara leo tumekula nyanya chungu, mara ukila dengu ukijamba ushuzi unanuka balaa. Hujakaa vizuri unaanza kuhadithia mkesha wa mwaka mpya. Mwishowe manzi anakuuliza jana ulitaka kuniambia nini? Tena huku kalegeza macho nadhani hata ubongo pia utakuwa umelegea. Chance pekee ambayo kamanda kama mimi nadokoa tu! Nafunga goli la kunyanyulia kombe*
*Unakaa kimya dakika kadhaa. Manzi pumzi zinapishana huku akili yake inawaza maneno matamu utakayoyamwaga. Na kweli, kimya kingi kina mshindo. Domo zege unaamua kufunguka uliyotaka kumwambia.*
*Unaanza kwa kumtaja. Naye anaitika kwa heshima. Unamwambia hili jambo ni la kipuuzi sababu ya umri wenu kutoruhusiwa na wazazi wenu na hata dini. Demu anakurekebisha, anakwambia hamna kitu cha kipuuzi kama tutaridhiana. Unafurahi kwa kukupa ahueni ya kuzidi kutiririka. Basi unaendelea kwa kumuita tena jina lake.*
*Unamwambia jambo nililotaka kukwambia.*
*Hapo unatulia kwa sekunde kadhaa kama vile MaMC wanavotaka kumtangaza Miss World. Binti Kimoyo kinaenda paa paa paa mpaka kitisheti kinafunuka*
*Unamalizia kwa kusema, naomba uniibie peni kwenye duka lenu*
*Kiukweli usipopigwa kofi na Malaika, utapigwa konzi na Shetani*
[emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] da golden chance kama hzo huwa hazitupati watu kama cc, nngekuwa mie hapo nmeshamaliza game

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je wajua?
Mtu mwenye bahati duniani Babu yake alikuwa rais, bibi yake alikuwa first lady
Baba yake alikuwa rais, mama yake alikuwa first lady

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

Jamii Forums mobile app
 
Mlevi alipanda daladala, konda akamwambia tabia yako ya ulevi huwezi kwenda PEPONI. Mlevi akajibu kumbe mnaenda PEPONI, nishusheni Mimi nakwenda Mbagala......[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

Jamii Forums mobile app
 
SONG: JELA
ARTISTS: AVEVA & KABURU Feat HANS POPE
PRODUCER: TAKUKURU
STUDIO: JPM RECORDS

Tangu Tufungwe Siku Ya Tatu Imefikaa
Bora Leo Hii Hans Pope Umefikaaa
Tupe Ripot Za Usajili Msimbazii
Twasikia Ngoma Amebaki Jangwaniiii

Kusema Kweli Mambo Sasa Magumuuu
Haruna Naye Hapokei Hata Simu
Si Unamkumbuka Yule Tambwe Mabaoooo
Naye Kabaki Yani Yanga Warohooo

Kwa Hali Hiyo Ubingwa Hatupati Tenaa
Na Mwaka Huu Watabeba Mapemaa
Mo Afanye Ile Mipango Yetuuu
Japo Tushike Nafasi Ya Tatuu

Hiv Ni Kipi Hasa Kisa Na Mkasa
Kilichofanya Mpaka Sasa Mko Hapa
Nimesikia Eti Mmeiba Pesaa

Hiyo Ni Kweli Hatuwez Kubishaaaa

CHORUS

Hiiiiiiiiii Iiiiiiiiii
Pole Saaaaanaaaa
Hiiiiiiii Iiiiiiiii
Nyamaza Acha Kuliaaaaaa x2

Yani hiiii iiiiihhh mavugo anakusabahiiiiiiiiiiiiiii

yani iiiih iiiih iiiih Manara na kichuya wanakupa hii.....

[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji377] [emoji377] [emoji377] [emoji125] [emoji125]
[emoji2] [emoji2] [emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*BOSS anamwambia sekretari wake*:
*Wiki hii tutaenda wote Serena Hotel kwenye mkutano fanya mipango yote.*

SEKRETARI (anamuaga mumewe):
Tunaenda na bosi Serena hotel kwenye mkutano for 1 week.

MUME (anampigia mpango wa kando):
Mambo safi, wife anaenda kikazi Serena, jitayarishe tujipe raha for 1 week

(Mpango wa kando) anamwambia mwanafunzi wake wa tution:
wiki hii nina kazi fulani hakuna tution mpaka week ijayo.

MWANAFUNZI anampigia simu sugar daddy wake ambaye ndo (BOSS):
Dear hakuna tution wiki hii nakuja kwako.....

BOSS anamwambia sekretari wake:
Siendi Serena tena coz mjukuu wangu atanitembelea.

SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Serena

MUME (anampigia Mpango):
dah! mpenzi, huyu fala haendi tena. Shit! So hadi next time plz

Mpango wa kando a.k.a teacher (anampigia mwanafunzi):
Darasa kama kawaida sorry for the earlier message.

MWANAFUNZI: darling tution
inaendelea kumbe, so nakuja wiki ijayo!!

BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya serena iko palepale......

HOW DO YOU HELP THESE PEOPLE?

*Mnasemanga Food chain mnakosea hii sijui tuiite nini???*

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Food web
 
Mchungaji leo kajipendekeza kumuita kijana mmoja mtanashati utufungulie ibada kwa maombi, watu wote wakafumba macho na jamaa akaanza! EE GOD TAZAMA WANAO TUKO FITI KISHENZI, HAMNA NOMA WALA NDUMBA, AMANI MWANZO MWISHO, YANI MZUKA ILE MBAYA. MWANAO ALIDEDI MSALABANI KISA MAWENGE YETU CC MAJITA, NAJUA UNATUPIGANIA KICHIZI, YANI GOD NIMEKUBALI WEWE NI JEMBE NA MSHUA WA WOTE, AMEN .Mchungaji hoi, KUMBE JAMAA ALISHA VUTA CHA TARIME MARA‍
 
Je wajua?
Mtu mwenye bahati duniani Babu yake alikuwa rais, bibi yake alikuwa first lady
Baba yake alikuwa rais, mama yake alikuwa first lady

[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

Jamii Forums mobile app
=wakili msomi fatma karume


sent from iPhone 7+ using jamii forums mobile app
 
Back
Top Bottom