Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

* Habari zenu *
Ndugu zangu ninapenda kuwataarifu kuwa siku ya jumatatu kijana mwenzenu ntachukua jiko. Japo imekua ghafla hili ni jambo la kheri la kumpendeza mungu niliamua kuchukua uwamuzi huu baada ya kuona mama yangu akipata shida kupikia kuni hivyo keshokutwa ntachukua jiko la gesi na kumpelekea nyumbani
*sitaki mother apate tabu*
 
*KWA STAILI HII WIZI HAUTAISHA TZ*
*Katika zoezi la kupata vitambulisho vya shule mpiga picha alimwambia mwalimu mkuu kuwa kwa kila picha gharama yake ni sh.500, mwalimu mkuu akamwambia mwalimu wa darasa awaambie wanafunzi walete sh.1000 kwa ajili ya picha, mwalimu wa darasa akawaambia wanafunzi mkawaambie wazazi wenu wawape sh.1500 ya picha, mwanafunzi alipofika nyumbani akamwambia mamake tumeambiwa tupeleke sh.2000 ya picha shuleni, mama akamfuata baba akamwambia mtoto kaambiwa apeleke sh. 5000 ya picha shuleni nipe haraka nimpe maana wamesema mwisho kesho...!!!!!.Dah Magufuli Anayo Kazi*
 
Kama utakipenda kimoja njoo PM tuzungumze biashara
1. Freezer aina ya Boss Tsh250000. Haina mlango wa mtungi wa gesi
.
2. Feni ya chini Tsh 15000/=. Inawaka kwa machale.. yaeza kukaa hadi masaa 2 haijaanza kuzunguka
,
3. Pasi ya umeme aina ya Phillips. Tsh 12000/=, haishiki moto kabisa hata ikae nusu saa kwny umeme na kidude cha kuregulate moto kimeharbika..

4. Meza ya plastic Tsh 75000/= ina miguu 3 na mmoja mfupi kidg.

5. Vikombe vya udongo Dozen 1 Tsh 25000/= ila vilipata ajali kidg.. vimekatika mikono na vingne vimetoboka chini
6.Redio ya caset lkini haina transiforma bei 34000
7.Flat scren bei 50000 kioo kimepasuka na haina rimot control na batan zime haribika fasta nichek [emoji41]
8.Simu aina ya Sumsung s7 edge 470000/= ilidondokea kwenye maji ikapiga shot, kitufe cha kuwashia hakipo na hata ukiweka kingine haiwaki, ni simu nzuri bora na ya kisasa!
9.Kamera aina ya sony mp 16 bei 62500/= haina lens, ni mbovu hata mafundi hawaitaki kama spea.
10.Bajaji aina ya tvs, bei 1400000/= haina matairi, viti wala usukani! Imetumika miaka 8 na inadaiwa kodi ya miaka 2!

Karibuni, bidhaa ni nyingi sana, zipo za aina tofauti tofauti kama magari, ndege, treni, meli, maparashuti, vifaru, n.k vyote hivyo vikiwa katika hali mbaya sana, (ikumbukwe hizi ni toys za watoto zilizotumika huko uswahilini na kutupwa kwenye majalala)
kama kawaida chawa hawakosekanagi kuharibu threads za watu
 
JINSI YA KURUDISHA UPYA NGUO YAKO ILIYOCHAKAA AU KUPAUKA!!!

WATU wengi hukosa raha haswa pale nguo zao wanazozipenda zinapochakaa au kupauka;;

Fanya kama ifuatavyo
1:chemsha maji yachemke kwa (100C°)
2:weka nguo yako kisha iache ichemke ndani ya dakika50
3:itoe nguo yako!!
4:weka mafuta,kitunguu,nyanya na chumvi kidogo
5:chukua nguo yako,iweke na ukoroge kisha ufunikie!!
Ona unavyonifatilia kwa makini,kama nguo imepauka kanunue nyingine kwani madukani zimeisha??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Vita baridi ni nini?

Vita baridi no pale ambapo we we na baba yako mnabishana kuhusu mpira yeye anasema Giroud mkali kuliko messi..halafu we we ukajisahau ukadhani upo kibandani unaropoka "msikieni huyu matako" [emoji23] [emoji23]
Hahahaha
 
JINSI YA KURUDISHA UPYA NGUO YAKO ILIYOCHAKAA AU KUPAUKA!!!

WATU wengi hukosa raha haswa pale nguo zao wanazozipenda zinapochakaa au kupauka;;

Fanya kama ifuatavyo
1:chemsha maji yachemke kwa (100C°)
2:weka nguo yako kisha iache ichemke ndani ya dakika50
3:itoe nguo yako!!
4:weka mafuta,kitunguu,nyanya na chumvi kidogo
5:chukua nguo yako,iweke na ukoroge kisha ufunikie!!
Ona unavyonifatilia kwa makini,kama nguo imepauka kanunue nyingine kwani madukani zimeisha??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahaha we jamaaa ujue unaonekana
 
Naomba siku yangu ya kufa ikifika nife kimya kimya usingizini kama marehemu babu yangu...

Sio kufa napiga mikelele kama wale abiria wake waliokuwemo kwenye gari lake hapo alipopitiwa na kifo usingizini nyuma ya usukani
 
Jamaa alienda kanisani ku confess makosa yake kwa mchungaji..

Jamaa: Mchungaji nimekuja ku confess dhambi zangu, nimelala nje ya ndoa na binti wa miaka 18 aliyekuwa bikira.

Mchungaji: Kata ndimu 10 ukamue kikombeni ... changanya na maji ya limau 10 humo kikombeni kisha unywe.

Jamaa: Hii ndio itaniondeshea dhambi zangu?

Mchungaji: Hapana... itaondoa hilo tabasamu lako hapo usoni kwako
 
Lala uache dirisha wazi usiku wa leo....

Mbu 1400 watabonyeza likes
Mbu 510 watacomment
Mbu 210 watashare event kwenye page zao

Mbu mmoja atajibu mualiko
Mbu laki moja watahudhuria
 
Back
Top Bottom