Kama Unafanya Uzinzi Sahau Kufanikiwa Maisha (Labda kwa Kutumia Waganga au Utapeli)

Inategemeana... Kuna watu waaminifu na wana mwenza mmoja, ila huo msoto!

Wapo wengine wana madaraka makubwa na wazinzi hatari lakini maisha yanawaendea tu fresh na hawatumii ndagu
 
Haya yanayosemwq yapo ndgu zangu watafutaji..

Usijifananishe ww na elon mask ambaye hata ufanye vipi hamtokuja kufanana sasa wewe mtaftaji kama mimi ukijifanya unaendekeza sana ngono utaona matokeo yake.
 
Mi nasimama na imani kuwa ukizini kuna mapepo machafu utaondoka nayo.

Ila wanaposema sijui uzinzi ghalama sizani maana mpaka sasa sijawahi ghalamia utamu niseme ukweli
 
Wakuu salamu,
Leo naomba tujiambie ukweli mchungu ambao wengi watauchukia, lakini ndio ukweli halisi. Kama wewe ni mwanaume au mwanamke unayeendekeza uzinzi na ngono zembe, sahau kabisa habari ya kufanikiwa kimaisha kwa njia halali ya jasho lako.

Ukiona mtu ni mzinzi wa kutupwa na bado ana ukwasi mkubwa, chunguza vizuri mfumo wa maisha yake. Utakuta aidha anasafiri na ndagu za waganga wa kienyeji, anajihusisha na utapeli (scams), au anafanya biashara haramu. Mafanikio ya halali na uzinzi hazitangamani.

Hizi hapa ni sababu kuu kwanini uzinzi utakuacha maskini:

1. Unapoteza Kibali na Baraka: Kiimani, uzinzi unakuondolea neema na mikosi inakuandama.

2. Mabadilishano ya Nuksi: Kila unayezini naye hubadilishana naye mifumo ya nishati; unabeba laana na mikosi yake.

3. Ufujaji wa Mtaji: Hakuna uzinzi wa bure. Pesa za guest, mizinga, na usafiri zinamaliza akiba yako.

4. Kupoteza Focus: Akili inayowaza ngono kila saa haiwezi kubuni mawazo mapya ya biashara au uwekezaji.

Kama unataka utajiri unaodumu na wenye amani ya moyo, fanya toba, tulia na mwenzi mmoja, na uweke nguvu kwenye kazi.

Nawasilisha wakuu. Je, unaamini kuna mtu anazini sana na anafanikiwa kwa njia halali kabisa?
Tafuta hela wewe.
 
Mi naona hii ipo applicable kwenye kujitafuta. Lakini ukishajipata haiwork.
Tunaona marajiri wengi wanapiga machine hovyo na bado matajiri.
 
Kufanikiwa kuko palepale, cha kufahamu uzinzi ni gharama na wakati mwingine inaweza kula muda wako, ila kama utaweza kwenda navyo sawa bila kuathiri utafutaji wako lazima ufanikiwe.
Wanaohusisha na mambo ya kiimani ni katika kujiongezea mazingira ya kuaminika kwa jamii ili waweze kula vizuri hela (sadaka) za watu.​
 
Wakuu salamu,
Leo naomba tujiambie ukweli mchungu ambao wengi watauchukia, lakini ndio ukweli halisi. Kama wewe ni mwanaume au mwanamke unayeendekeza uzinzi na ngono zembe, sahau kabisa habari ya kufanikiwa kimaisha kwa njia halali ya jasho lako.

Ukiona mtu ni mzinzi wa kutupwa na bado ana ukwasi mkubwa, chunguza vizuri mfumo wa maisha yake. Utakuta aidha anasafiri na ndagu za waganga wa kienyeji, anajihusisha na utapeli (scams), au anafanya biashara haramu. Mafanikio ya halali na uzinzi hazitangamani.

Hizi hapa ni sababu kuu kwanini uzinzi utakuacha maskini:

1. Unapoteza Kibali na Baraka: Kiimani, uzinzi unakuondolea neema na mikosi inakuandama.

2. Mabadilishano ya Nuksi: Kila unayezini naye hubadilishana naye mifumo ya nishati; unabeba laana na mikosi yake.

3. Ufujaji wa Mtaji: Hakuna uzinzi wa bure. Pesa za guest, mizinga, na usafiri zinamaliza akiba yako.

4. Kupoteza Focus: Akili inayowaza ngono kila saa haiwezi kubuni mawazo mapya ya biashara au uwekezaji.

Kama unataka utajiri unaodumu na wenye amani ya moyo, fanya toba, tulia na mwenzi mmoja, na uweke nguvu kwenye kazi.

Nawasilisha wakuu. Je, unaamini kuna mtu anazini sana na anafanikiwa kwa njia halali kabisa?
Mbona kuna wanasiasa lukuki wamefanikiwa na wanakesha 24/7
 
Back
Top Bottom